Wazo la leo: CCM bado inapendwa, na inazidi...

Hawa wameamka wanajitambua wao ni nani na CCM ni nini? Wnajua kinachoendelea na pia wanajua, kujua tu kinachoendelea si hoja, hoja ni kujua namna ya kukabiriana na kinachoendelea.

Hawa wanasema CCM wezi na wababe kwa hiyo hawana imani na CCM. Kundi hili la kusema CCM wezi ni kundi ambalo lina watu wengi ambao hawaendi kupiga kula kwa sababu wanajua CCM watatumia vyombo vya DOLA kama POLISI UWT na JWTZ kupiga mkwara na hata kuua ili waibe wadanganyena kushinda.
Kundi linalosema CCM ni wezi linakua kwa kasi sana na ndugu zangu wa CCM wanapenda sana kukua kwake. Hata hivyo kundi hili ni bomu la kuleta kilio kwa CCM kwa sababu siku ukiona kundi hili,ghafla, limeacha kunennepa linakonda! Mwisho wa mwisho wa CCM utatimia papo hapo.

Wote tunatakiwa tufungue macho tuone kitu halisi kinachoendelea kwa wakati huu.

Mambo ya ushindi kwa kishindo yatasemwa tu huko vyumbani na vimada wao wakiwa wamepakazwa kizuzuzuzu.
pia kuna kuna kundi linaloona upinzani haujasema kitu wao watafanyaje, kusema tu ccm wezi haitoshi!

 
Porojo na kubwabwaja bila mpango, unafikiri kukiwa kuna vyama vingi kuna kuoenda chama> hizo ni fikra za kizamani sana.

Tanzania imedhihirika kuwa hakichaguliwi chama anaechaguliwa ni mwanachama. Na ushahidi mzuri ni Slaa, alikataaliwa kuwa mgombea na CCM kwa mapungufu waliyoyaona kwake, akaondoka na kwenda kugombea kupitia chadema akachaguliwa.

Shibuda hali kadhalika. Mrema ni hivyo hivyo.

Kikwete alipochaguliwa Urais siamini kama ni wana CCM tu waliomchaguwa, nna uhakika wa vyama vingine na wasi na vyama pia walimpa kura zao.

Uchaguzi huu wa juzi umekuwa ni pigo kubwa sana kwa UKAWA na nnadiriki kusema imekuwa UKIWA, nilitegemea watapata angalau 30% lakini wapiiii? wananshangaza!


Kakojoe ukalale Tezi jike.
 
Porojo na kubwabwaja bila mpango, unafikiri kukiwa kuna vyama vingi kuna kuoenda chama> hizo ni fikra za kizamani sana.

Tanzania imedhihirika kuwa hakichaguliwi chama anaechaguliwa ni mwanachama. Na ushahidi mzuri ni Slaa, alikataaliwa kuwa mgombea na CCM kwa mapungufu waliyoyaona kwake, akaondoka na kwenda kugombea kupitia chadema akachaguliwa.

Shibuda hali kadhalika. Mrema ni hivyo hivyo.

Kikwete alipochaguliwa Urais siamini kama ni wana CCM tu waliomchaguwa, nna uhakika wa vyama vingine na wasi na vyama pia walimpa kura zao.

Uchaguzi huu wa juzi umekuwa ni pigo kubwa sana kwa UKAWA na nnadiriki kusema imekuwa UKIWA, nilitegemea watapata angalau 30% lakini wapiiii? wananshangaza!

Kwa faida yako humu jukwaani kuna mtu kauliza lazima tuuane kila uchaguzi? Majibu ni haya hapa chini
Hii kitu nimekuwa nikiipigia kelele sana humu jamvini. Lakini ukiangalia sababu hasa ni hiki chama tawala. Kwa sehemu kubwa viongozi wa hiki chama wamegeuza uongozi ni kama ajira, hivyo kuona cheo ni kama sehemu ya kufanikisha malengo yao ya kimaisha. Kitu ambacho hawakukitegemea ni mabadiliko. Wengi wa viongozi hawa wamefanya mambo mengi mazuri na mabaya kupitia dhamana zao, sasa inapotokea watu wengine kutaka kuingia na wakati wao wanaona ni nafasi zao za kudumu, kwanza wanajua maisha yatakuwa magumu kwao kwani hawana pa kwenda au cha kufanya bila madaraka, na mambo yao mabaya yatavuja na hatimaye kushusha hadhi zao katika jamii, kumbuka wanapokuwa kwenye nafasi hizi huwa miungu watu hapo unategemea nini?

Sasa kwanini mauaji yanatokea? Wale waliopo madarakani hawapo tayari kuukubali ukweli wa mabadiliko na wale wanaoyataka mabadiliko hawako tayari kuona tena wale wakongwe wakiyazuia. Kwa bahati mbaya sana kutokana na mfumo mkongwe kuachia rushwa kutamalaki, baadhi ya askari polisi hasa walio wengi wameutumia udhaifu wa mfumo huu kwa kushirikiana na walio madarakani kujipatia vipato ambavyo sio halali na kupelekea kuwa matajiri kwa njia haramu. Sasa unaona kabisa umma umeanza kujitambua sasa ndio wanaungana walioko madarakani na polisi waliojinufaisha kwa mfumo huu mbovu kuhakikisha wengine hawaingii madarakani kwani hofu yao mambo mengi ya wizi walioufanya yatabainika na hatimaye mkono wa sheria kuchukua hatua.

Ninachokiona hapa ni machafuko huko mbeleni, kwani polisi hawatendi haki dhidi ya umma kwa kushirikiana na watawala wa sasa au chama tawala, na umma nao unazidi kukosa imani na watawala waliopo pamoja na jeshi la polisi kwani umma sasa umeamini kabisa watawala na jeshi la polisi hawako tayari kuona mabadiliko. Mifano ya watawala kutokukubali mabadiliko ni mingi, rejea mizengwe ya bunge la katiba, uchaguzi huu wa serekali za mitaa kufanyika kwa mizengwe mingi. Na sasa tutegemee mambo mabaya zaidi na hila zaidi kwani uchaguzi huu unazidi kuwatia hofu juu ya hatima yao. Nadhani ni busara tu ndio itatuoa hapa lakini kwa uhalisia ninaouna na ujinga wa watawala wa kiafrika, machafuko ni lazima.
 
ccm.png
 
Kukataliwa!

Kukataliwa kuko kwa aina nyingi. Mtu anaweza kutikisa kichwa, anaweza kunyosha mkono kupinga, na anaweza kusema 'hapana'. Lakini pia mtu anaweza kukupigia kura ya kukukataa. Panapokuwa na ushindani na mtu mmoja akapiga kura ya kumkubali mwingine kimsingi amepiga kura ya kukukataa wewe. Na ukiona watu wengi wanazidi kukukataa kila wanapoulizwa swali lazima ujihoji.


Mwanzoni kulikuwa na watu mia wanaulizwa; 99 wakakukubali wewe; walipoulizwa tena, 90 wakakukubali; walipoulizwa tena ikawa 88, mara wakawa 75, mara wakawa 65. Sasa ni "ni kweli" bado unakubaliwa na "wengi" lakini "wengi" wale wamepungua. Kwa maneno mengine, wanaokukataa wameongezeka kutoka mtu mmoja hadi kufikia 35!
Unaweza ukajiambia bado "unapendwa" lakini pia unaweza kujiambia "umezidi kukataliwa". Yote mawili ni kweli. Ila usipoangalia ikifika watu 51 wanakukataa zaidi...


Na unapozidi kukataliwa inamaana wanaokupenda wamezidi kupungua mwisho unaweza kujikuta unaanza kulazimisha kupendwa!!

Tafakari...

CC: Mwana diwani
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom