Wazo la leo: CCM bado inapendwa, na inazidi...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,990
2,000
Kukataliwa!

Kukataliwa kuko kwa aina nyingi. Mtu anaweza kutikisa kichwa, anaweza kunyosha mkono kupinga, na anaweza kusema 'hapana'. Lakini pia mtu anaweza kukupigia kura ya kukukataa. Panapokuwa na ushindani na mtu mmoja akapiga kura ya kumkubali mwingine kimsingi amepiga kura ya kukukataa wewe. Na ukiona watu wengi wanazidi kukukataa kila wanapoulizwa swali lazima ujihoji.


Mwanzoni kulikuwa na watu mia wanaulizwa; 99 wakakukubali wewe; walipoulizwa tena, 90 wakakukubali; walipoulizwa tena ikawa 88, mara wakawa 75, mara wakawa 65. Sasa ni "ni kweli" bado unakubaliwa na "wengi" lakini "wengi" wale wamepungua. Kwa maneno mengine, wanaokukataa wameongezeka kutoka mtu mmoja hadi kufikia 35!
Unaweza ukajiambia bado "unapendwa" lakini pia unaweza kujiambia "umezidi kukataliwa". Yote mawili ni kweli. Ila usipoangalia ikifika watu 51 wanakukataa zaidi...


Na unapozidi kukataliwa inamaana wanaokupenda wamezidi kupungua mwisho unaweza kujikuta unaanza kulazimisha kupendwa!!

Tafakari...
 

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,070
1,195
Ni kweli CCM bado wanapendwa sana.
Kuna makundi mawili yanayoipenda CCM.
La kwanza ni la madingi ambao wanaogopa kuipa makalio CCM kwa vile wanaamini TANU imo humo.La pili ni vijana wadogo wenye tamaa ya ngawira,hawa wana mapenzi ya kumaliziana kichakani nipe nikupe. Bila pochi wanaipa kisogo
Uzuri ni kwamba kundi la kwanza namba yao inapungua haingezeki.
Kundi la pili inabidi ufanye hesabu namba au idabi yao inapungua watu wawili na kuongeza nusu mtu kila siku.
kwa hiyo wakati mfupi tu ujao CCM watakuwa wanapendwa sana lakini kwa asilimia nduchu.

Hapo wataonja mauti kama KANU:madgrin:
 

mob

JF-Expert Member
Dec 4, 2009
2,270
2,000
Time will tell

Bado kitambo kidogo tunaanza kuiweka katika vitabu vya historia na watoto wetu waanze kujifunza kulikua na chama hicho
 

AIR MISSILE 2015

JF-Expert Member
Sep 6, 2013
516
500
Mkuu, sisi chama chetu bado kinapendwa, maana ktk uchaguzi huu bado watu 42 (maeneo yaliyofanya uchaguzi) wanatupenda!! Haijalishi wamepungua kias gani kutoka wa mwanzo!!

Hata tukibaki 20 tu watiifu kwa chama bado tutakuwa tunapendwa, kinachotakiwa "TUWE WACHACHE WAPIGA DILI WATIIFU ILI MGAO UPUNGUE"!! Kuliko kuwa na wengi wanaovujisha "MADILI" yetu kwa wananchi!!!
 

jme

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
4,502
2,000
mkuu nape tunamsubili atakuja na drama zake ccm bado inapendwa na inaimarika
 

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,138
2,000
huo ndo ukweli na inahitaji mwenye akili timamu kujua ukisemacho...watakuja watu macho mekundu kupinga.... ni haki yao ya kikatiba....
 

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,227
2,000
Kweli huku kupendwa kukataliwa kuzuri sana. Watakuja hapa povu jingi tunapendwa sana tuna 51% na UKAWA 49%, kwa kweli namba ya kupendwa inaongozeka kwa kasi sana. Kwa sababu 2009 mlikuwa na 99% ya kupendwa msisahau kuja na takwimu za 2014. Hongereni CCM KWA KUPENDWA.
 

Mount Kibo

JF-Expert Member
Apr 7, 2013
1,922
1,250
Ila wao kwa akili zao watakuja na swaga ka zile kufunga tumefungwa lakini chenga twawala.Subiri Nepi na wafuasi amabo hawajatambua kumekucha watakuja na hoja zao nyepesi kama nyusi
 

Bembu

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
243
195
Ukweli haipendwi ila inaogopwa kutokana na ubabe na vitisho na dhulma wanazofanyiwa walalahoi.
 

Gwallo

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
2,729
2,000
Kwa mahesabu ya Mzee Mwanakijiji ni kutafuta Depreciation value of an old asset called ccm by using straight line method.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom