Wazo la leo: CCM bado inapendwa, na inazidi...

MM Kwa muono wetu wa Kichama chetu cha Mafisadi ,hata wapiga kura wakiwa 35% bado tunajiona tunapendwa sana tu,na tunauhakika wa kuongoza miaka mingine 100.Lakini ukumbuke piahata hawa 75% au 65% ujue tumelazimishwa,tumewekewa mizengwe mingi,vitisho nk nk.

Hapo ukiondoa siye wenye uwoga kwa kweli Chama chetu hiki pendwa nina uhakika kwa sasa trend imeshuka kufikia 50% kama siyo 35%
 
Kukataliwa!

Kukataliwa kuko kwa aina nyingi. Mtu anaweza kutikisa kichwa, anaweza kunyosha mkono kupinga, na anaweza kusema 'hapana'. Lakini pia mtu anaweza kukupigia kura ya kukukataa. Panapokuwa na ushindani na mtu mmoja akapiga kura ya kumkubali mwingine kimsingi amepiga kura ya kukukataa wewe. Na ukiona watu wengi wanazidi kukukataa kila wanapoulizwa swali lazima ujihoji.

Mwanzoni kulikuwa na watu mia wanaulizwa; 99 wakakukubali wewe; walipoulizwa tena, 90 wakakukubali; walipoulizwa tena ikawa 88, mara wakawa 75, mara wakawa 65. Sasa ni "ni kweli" bado unakubaliwa na "wengi" lakini "wengi" wale wamepungua. Kwa maneno mengine, wanaokukataa wameongezeka kutoka mtu mmoja hadi kufikia 35!
Unaweza ukajiambia bado "unapendwa" lakini pia unaweza kujiambia "umezidi kukataliwa". Yote mawili ni kweli. Ila usipoangalia ikifika watu 51 wanakukataa zaidi...

Na unapozidi kukataliwa inamaana wanaokupenda wamezidi kupungua mwisho unaweza kujikuta unaanza kulazimisha kupendwa!!

Tafakari...

Kwahiyo unaililia CCM au?
 
nimependa hiyo"wanaokupenda wanazidi kukukataa"
Najivunia kuwa Mtanzania

Mtu mmoja alifariki na kwenda kuzimu. Akiwa huko aligundua kwamba kuna kuzimu tofauti kwa nchi tofauti na akaamua kuchagua mojawapo yenye maumivu kidogo kwa ajili kufaidi ufalme wa kuzimu. Akaenda kuzimu ya Ujerumani na kuuliza “hapa wanafanya je?”

Akajibiwa "kwanza unakalishwa kwenye kiti cha umeme kwa muda wa saa moja.Halafu unalazwa kwenye kitanda chenye misumali kwa muda saa moja nyingine.Halafu anakuja shetani wa Kijerumani na kukucharaza bakora kutwa nzima”.Hakukubaliana na hali hiyo akaondoka.

Akaenda kuzimu ya Marekani,Urusi na nyingine nyingi.Akagundua kwamba zote zinafanana na kuzimu ya Ujerumani. Baada ya hapo akaenda kuzimu ya Tanzania, huko alikuta kuna misururu mirefu ya watu wanaosubiri kuingia ndani,akashangaa,akauliza wanafanya nini humo?.

Akajibiwa, "kwanza unakalishwa kwenye kiti cha umeme kwa muda wa saa moja.Halafu unalazwa kwenye kitanda chenye misumali kwa muda saa moja nyingine.Halafu anakuja shetani wa Kitanzania na kukucharaza bakora kutwa nzima. " Akauliza,Lakini hii inafanana kweli na kuzimu za nchi nyingine mbona kuna misururu mirefu ya watu namna hii?

"Akajibiwa ,kwa sababu hakuna umeme hivyo kiti cha umeme hakifanyi kazi na misumali iliyonunuliwa haijaletwa, kwa hiyo kitanda ni kizuri kulalia.Na shetani wa kitanzania ni mtumishi wa umma,ambaye anakuja asubuhi,anasaini kwenye kitabu cha mahudhurio kazini na kurudi nyumbani kuendelea na shughuli zake binafsi.

Ni Yule anayewaibia Watanzania hela kwa ufisadi na kugoma kujiuzulu, kwa kulindwa na wakubwa na kuwaacha watanzania walio wengi wakikosa huduma muhimu za Jamii na huku walioko madarakani wanateteana kwenye ”madeal” kibao ya kupiga fedha za walalahoi na wezi wadogo wanaoiba chakula kwa sababu ya njaa ya chakula cha siku na mazao waliyolima na wazazi wao hayana soko na yaliyonunuliwa wakulima wamekopwa na bado wanaibiwa kura zao wanapofanya maamuzi ya kubadilisha viongozi wasiofaa na wezi wa mali ya umma.Pia viongozi wanaopuuza maamuzi ya wananchi ya kubadili katiba wanayoitaka na kuweka matakwa yao ili kujilinda wao na mafisadi wenzao.”Eee mungu tusaidie tuepuke kikombe hiki”

Siku njema!!
 
Subirini tu nyie fisiwatu ipo siku isiyo na jina ccm itadondosha mkono wake mpate kitoweo
 
Na unapozidi kukataliwa inamaana wanaokupenda wamezidi kupungua mwisho unaweza kujikuta unaanza kulazimisha kupendwa!! Tafakari...
Na ukilazimisha kupendwa ndiyo unafanya watu wakukatae zaidi. Pia ukilazimisha kupendwa utasababisha watu wakulazimishe kukubali kuwa wamekukataa. Inapofikia hatua ya wewe kulazimisha kupendwa na watu wakakulazimisha kukukataa, basi jua mwisho wako ni mbaya zaidi. Kwa maana Chuki itazaliwa na watu siyo tu watakukataa bali watakuchukia na Chuki hiyo itadumu hata kwa vizazi vyako vya baadaye. Nimetafakari......
 
Nimeipenda hii "Na unapozidi kukataliwa inamaana wanaokupenda wamezidi kupungua mwisho unaweza kujikuta unaanza kulazimisha kupendwa!!" Halafu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ccm ilipigwa na butwaa kwa jinsi ilivyopata ushindi kiduchu. Kamati kuu yake ikakaa kuangalia nini tatizo. Kutokana na ile hali ya kuchanganyikiwa wakaona vijana ndio wanawapiga chini. Ikabidi vijana kama akina Mwigulu, Nape, January, Nchimbi nk waliulizwe nini cha kufanya ili kukiokoa chama dhidi ya hii hali. Kwa bahati mbaya sana vijana hawa sio wabunifu bali watu wakucheza na nafasi, ikabidi wajitutumue kukisaidia chama. Hapa ndipo tulipoona mawazo ya kizee lakini toka kwa vijana. Nadhani unakumbuka kubambikizia kesi kwa wapinzani. Sisemi chochote kwani mtoa wazo anafahamika japo siku hizi kama ametubu kwa nabii Joshua. Likaja wazo la kuweka watu kupambana mitandaoni ili kujibu mapigo, wazo toka kwa Nape akapita mpaka kwenye vyombo vya habari eti kujenga urafiki na kuitangaza ccm yenye miaka karibia 40 sasa!! Hapa ndio tukaona wajenga hoja za kitoto na kipuuzi kama akina Lizaboni, Ifweero, Msalani nk. Hawakuishia hapo akina January wakajifanya wanajua sana mitandao ndio hao wamekaa na mbinu za ulaya mashariki kufuatilia IP adress zinazowapa ukweli.

Ukijaribu kuangalia vijana wote hawa walioko ccm sio wabunifu bali wanajivunia kuwa na dola, mambo yakazidi kuwa mabaya na wazee sasa wakaanza kupanic kwani mbinu za vijana hazileti matunda. Ikabidi sasa ni kuzuia mikutano ya wapinzani kwa njia yoyote. Nadhani unakumbuka mauaji ya kwenye mikutano ya wapinzani iliyotoa roho za watz wenzetu nayo ni mingi, mauaji ya Ali Zona morogoro, Daud Mwangozi japo si mwanachadema lakini sababu ilikuwa ni cdm, bomu mkutano wa kampeni arusha, bila kusahau mauaji wakati wa uchaguzi Igunga na arumeru mashariki. Hivi katika mazingira haya unategemea kwamba unachaguliwa kwenye uongozi kwakuwa unapendwa ama hila? Hapo ndipo ccm ilipofikia.
 
Mkuu Mwanakijiji

Tathmini matata sana hii.

Wenyewe CCM watakuja kusema wamepata ushindi wa kishindo. Watachagiza zaidi kwa kunadi kuwa kuna maeneo wamepita bila kupingwa.

Laiti wangeelewa maana ya andiko hili....
 
..... Jipe Moyo.!

Huu Ushauri unanikumbusha ule wimbo wa Flora Mbasha wa "Jipe moyo...... Yana mwisho", juzi niliposikia anadai talaka nikacheka sana!!! Kumbe ule wimbo alikuwa au anatuimbia sie wengine yeye yale maneno hayamuhusu au alikuwa hajui anachoimba. Mbona hangoji ayashinde? Naona yamemshinda.
CCM Jipe moyo, Mtayashinda.
Hahahahaaaa!!!
 
mkuu CCM haijakataliwa ila tu fahamu kwamba,,, kuna kizazi kilichokuwa hakipigi kura nikiwemo mimi....... hiki kizazi kwa asilimia kubwa kimeamua kupiga kura sasa,,, na matokeo yake yatakuwa mabaya sana kwa CCM 2015,,, Kiumjumla sasa watu wamechoshwa na wameamua kuingilia hili suala kwa kupiga kura, ufahamu tu mkuu miaka yote wanaojiandikisha kupiga kura na wanaoipiga kura tofauti huwa ni kubwa sana,,, sasa hii tofauti ndio inawaletea CCM matatizo sasa....hiki kizazi kisichopiga kura ni kile kizazi korofi na ndio shida ya CCM hiyoo sasa.

fanya uchunguzi kwa mtu mmojammoja mtaani hasa vijana ambao ni wengi uone tofauti ya watu,,, watu hawaipendi CCM siku nyingi ila tu kizazi hiki huwa kinapuuzia suala zima la upigaji kura, na siku hizi kizazi kikiamua mambo yatakuwa mabaya sana kwa CCM....

CCM kama chama tawala kimefanya mambo mabaya sana kwa wananchi wake,,, yote ambayo CCM hujisifia nayo huwa yako ndani ya majukumu yao na sio maajabu ambayo wanataka tuwasifie... kujenga barabara, miundo mbinu kwa ujumla, huduma za jamii, elimu nk haya ni majukumu ya mtawala... kwenda mwezini, kuchimba mafuta wenyewe, kuwa na migodi yetu inayoperfom, kuwa na shirika bora la ndege na bandari inayofanya kazi kwa ufanisi, kuwa na reli ya kisasa inayooperate mizigo na abiria.... haya ndio maajabu tunayoyataka.
 
Kukataliwa!

Kukataliwa kuko kwa aina nyingi. Mtu anaweza kutikisa kichwa, anaweza kunyosha mkono kupinga, na anaweza kusema 'hapana'. Lakini pia mtu anaweza kukupigia kura ya kukukataa. Panapokuwa na ushindani na mtu mmoja akapiga kura ya kumkubali mwingine kimsingi amepiga kura ya kukukataa wewe. Na ukiona watu wengi wanazidi kukukataa kila wanapoulizwa swali lazima ujihoji.

Mwanzoni kulikuwa na watu mia wanaulizwa; 99 wakakukubali wewe; walipoulizwa tena, 90 wakakukubali; walipoulizwa tena ikawa 88, mara wakawa 75, mara wakawa 65. Sasa ni "ni kweli" bado unakubaliwa na "wengi" lakini "wengi" wale wamepungua. Kwa maneno mengine, wanaokukataa wameongezeka kutoka mtu mmoja hadi kufikia 35!
Unaweza ukajiambia bado "unapendwa" lakini pia unaweza kujiambia "umezidi kukataliwa". Yote mawili ni kweli. Ila usipoangalia ikifika watu 51 wanakukataa zaidi...

Na unapozidi kukataliwa inamaana wanaokupenda wamezidi kupungua mwisho unaweza kujikuta unaanza kulazimisha kupendwa!!

Tafakari...

baada ya rongorongo nyingi matusi mengi kebehi nyingi dharau nyingi unakuja kutambua kuwa ccm ni nambari one ahsante mkuu endelea na ndoto hizo mungu atakubariki kumbuka ccm ikiondoka madarakani si upinzani watakaotawala bali diaspora ambao watakuwa vibaraka wa mabeberu mifano ipo amba arabspring walivyobadilisha tawala zilizowaletea uhuru na kiwasomesha
 
Kukataliwa!

Kukataliwa kuko kwa aina nyingi. Mtu anaweza kutikisa kichwa, anaweza kunyosha mkono kupinga, na anaweza kusema 'hapana'. Lakini pia mtu anaweza kukupigia kura ya kukukataa. Panapokuwa na ushindani na mtu mmoja akapiga kura ya kumkubali mwingine kimsingi amepiga kura ya kukukataa wewe. Na ukiona watu wengi wanazidi kukukataa kila wanapoulizwa swali lazima ujihoji.

Mwanzoni kulikuwa na watu mia wanaulizwa; 99 wakakukubali wewe; walipoulizwa tena, 90 wakakukubali; walipoulizwa tena ikawa 88, mara wakawa 75, mara wakawa 65. Sasa ni "ni kweli" bado unakubaliwa na "wengi" lakini "wengi" wale wamepungua. Kwa maneno mengine, wanaokukataa wameongezeka kutoka mtu mmoja hadi kufikia 35!
Unaweza ukajiambia bado "unapendwa" lakini pia unaweza kujiambia "umezidi kukataliwa". Yote mawili ni kweli. Ila usipoangalia ikifika watu 51 wanakukataa zaidi...

Na unapozidi kukataliwa inamaana wanaokupenda wamezidi kupungua mwisho unaweza kujikuta unaanza kulazimisha kupendwa!!

Tafakari...
Vyama vyetu vingi tawala Afrika vilianza 'kulazimishwa kupendwa' mara tu nchi zilishaingia kwenye mfumo wa vyama vingi.
 
42 Reactions
Reply
Back
Top Bottom