Kukataliwa!
Kukataliwa kuko kwa aina nyingi. Mtu anaweza kutikisa kichwa, anaweza kunyosha mkono kupinga, na anaweza kusema 'hapana'. Lakini pia mtu anaweza kukupigia kura ya kukukataa. Panapokuwa na ushindani na mtu mmoja akapiga kura ya kumkubali mwingine kimsingi amepiga kura ya kukukataa wewe. Na ukiona watu wengi wanazidi kukukataa kila wanapoulizwa swali lazima ujihoji.
Mwanzoni kulikuwa na watu mia wanaulizwa; 99 wakakukubali wewe; walipoulizwa tena, 90 wakakukubali; walipoulizwa tena ikawa 88, mara wakawa 75, mara wakawa 65. Sasa ni "ni kweli" bado unakubaliwa na "wengi" lakini "wengi" wale wamepungua. Kwa maneno mengine, wanaokukataa wameongezeka kutoka mtu mmoja hadi kufikia 35!
Unaweza ukajiambia bado "unapendwa" lakini pia unaweza kujiambia "umezidi kukataliwa". Yote mawili ni kweli. Ila usipoangalia ikifika watu 51 wanakukataa zaidi...
Na unapozidi kukataliwa inamaana wanaokupenda wamezidi kupungua mwisho unaweza kujikuta unaanza kulazimisha kupendwa!!
Tafakari...