Wazo la kujiajiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo la kujiajiri

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Stigliz, Oct 27, 2011.

 1. S

  Stigliz Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi ishakuwa kadhia,mwaka ushapita pasi kuwa na ajira japo Degree ninayo,tena ya Uchumi. Nimedhamiria kujiajiri hata kwa kuficha vyeti,Ombi langu, je biashara ipi ya halali na mtaji kiasi gani utafaa?Nipo Dar,Mnijuze tafadhali?
   
 2. N

  NYAGO Member

  #2
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MIE kwa ushauri wangu ungejihusisha na biashara ya kuuza nafaka kama vile mchele wa jumla, maharage, na bizaa zingine za nafaka..au ukiweza fungua ka mini-supermarket kama kamtaji kataruhusu..kila la heri
   
 3. S

  Stigliz Member

  #3
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa wazo lako yakinifu,biashara ya nafaka natazamia cku zjazo ila kwa kuanza kulima then kipindi cha mavuno nifanye manunuzi yakutosha.JE MUDA HUU MCHACHE ULIO MBELE YANGU KIPI NIKIPE KIPAUMBELE?
   
 4. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Kama una mtaji wa kutosha fungua biashara ya M-pesa, Tigopesa na vocha za jumla. Inalipa sana mkuu hii biashara ila angalia kwanza mazingira ya sehemu husika utakayofungulia biashara!
   
 5. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  wazo zuri. Kwa kuongezea mie nitakupatia ushauri wa bure wa jinsi ya kuanziasha biashara ya nafaka, pia nitakuunganisha na wafanyabiashara wakubwa wa nafaka hapa dar.hebu ni pm .
   
 6. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  wazo zuri sana tena sana maana wengi wetu tukishatumbukia kwenye hiz ajira akili zinadumaa kabisa kama umeshafikia maamuzi mazuri na una mtaji pia kama una access na mikoani unaweza fanya biashara ya kuku wa kienyeji hasa hichi kipindi cha sikukuu huku akili yako ikikaa sawa vile unaweza jaribu kilimo chenye maanufaa kwa mwaka mmoja degree yako iko palepale tena na usomi wako unaweza ukafanikisha sana jambo la msingi tembelea jukwa la uchumi(business forum) kuna mambo mengi ya kujifunza na kuna wadau wengi wanaushauri utapata michango mingi sana huko nawasilisha
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Stigliz

  kwanza kabisa nikupongeze kwa uthubutu wako,

  siahidi kukushauri ingawa nikiwa na mawazo mazuri ya biashara nitafanya hivyo

  pia tegemea mwanzo mgumu lakini wenye mwelekeo wenye mafanikio

  wish you all the best
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,603
  Trophy Points: 280
  Stigliz, naanza kwa kukupa pole kwa sababu nawe ni mhanga wa kasumba ya uelimike ili uajiriwe, japo umeshachelewa, lakini 'better late than never'.

  Wewe ulitakiwa tangu unasoma hiyo degree yako una focus ukimaliza ufanye nini, hivyo unakuwa unasoma kwa malengo. Kwa vile ulisoma kwa lengo la kuajiriwa, sasa unataka kujiajirio, sio kwa sababu umepania kujiajiri, bali unataka kujiajiri kwa sababu umekosa ajira ya kuajiriwa, ndio maana hata bussiness idea hauna!.

  Ili ujiajiri kwa mafanikio, kwanza dhamiria, have a 'will do do something', huo ndio mlango wako wa kutokea na sio kutafuta pa kutokea kwa sababu umebanwa!.

  Pili fanya upembuzi yakinifu bussiness line yako ni nini, hii inamaanisha wewe lazima ujijue, interest yako imelala wapi, and if you do that, yu'll do it with passion na mapato ndio yatafuatia. Kwa mfano kama unajijuya wewe ni mtanashati, huwezi kuuza mkaa, kama wewe ni mtulivu biashara za mahangaiko ya kusafiri kufuatilia mazao na kupanda nyumba kwenye malori ya mizigo hutaziweza. Jipime wewe unaweza nini, fanya upembuzi yakinifu mzuri kuhusu mahitaji yako na mtaji.

  Namfahamu mtu pale Mwenge, alianza na bajaji moja miaka miine iliyopita, sasa ana bajaji 20, nyumba mbili na ni tajiri mkubwa hivyo inategemea utafanya biashara gani ambayo inaendana na wewe yaani bussiness line!.
   
 9. S

  Stigliz Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante saaana,Nilishakuwa na ujuzi wa mambo ya mikopo wa miezi saba,kuna wafanyabiashara nataka nianze kukaa nao nipate ujuzi na uzoefu then miezi michache baadae niingie moja kwa moja.UPPER SECOND GPA mtaani ni taabu tupu,nitapambana kwenye biashara najua miaka mitano ijayo nitakuwa m2.
   
 10. S

  Stigliz Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante saaana,Nilishakuwa na ujuzi wa mambo ya mikopo wa miezi saba,kuna wafanyabiashara nataka nianze kukaa nao nipate ujuzi na uzoefu then miezi michache baadae niingie moja kwa moja.UPPER SECOND GPA mtaani ni taabu tupu,nitapambana kwenye biashara najua miaka mitano ijayo nitakuwa m2.
   
 11. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ndugu yangu umeamua vema lakini wakati ukiwa unasubiri au unaendelea na mchakato wako. fuata link hii BetterWebBuilder. then ukiwa na jambo unalohitaji kujua usisite kuuliza.
  nakutakia mafanikio mkubwa
   
 12. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hongera mkuu namimi niko katika line kama
  yako,ila inabidi tuwe wavumilivu
   
 13. S

  Stigliz Member

  #13
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo sawa,tubadili mitazamo,japo mwanzo mgumu naamini mbeleni uamuzi wetu utatunufaisha.
   
 14. S

  Stigliz Member

  #14
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutafika,hii ndio imani yangu kubwa.
   
 15. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  kwa mtu msomi ni jambo la msingi sana kujitofautisha na ambaye hakuipata hiyo elimu yako. sitegemei utakapojiajiri ufanye sawa na wao. Hata kama biashara zinafanana, lazima elimu yako ionekane katika kazi zako. Sitegemei ufanye biashara ya uchuuzi. Kununua na kuuza nafaka kila mtu anaweza. Hata yule asiyejua darasa. Umesoma hadi shahada, unataka kupigana vikumbo na waliokwepa umande? Lazima uwe tofauti. Wewe uliyesoma, hata kama umejiajiri katika huduma ama uzalishaji ni lazima vitu vitatu vionekane; input, process and output. Huu ndio ujasiriamali.
   
 16. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  anzisha banking company ni bonge moja la biashara.....
   
 17. S

  Stigliz Member

  #17
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NI VYEMA UKAWEKA BAYANA NI VP UNATAKA IWE,nitajifunza vyote then mbeleni nitapembua lipi ndo lipi.5 YRS TO COME I NEED TO B SOMEBODY.
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  dont worry. Nikitulia nitafafanua vya kutosha
   
 19. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  mkuu, pole kwa kazi.
  Mkuu ninamashaka makubwa sana na lugha uliyoitumia katika kuwakilisha maoni yako, hasa katika vipengele ambavyo nimeviwekea rangi nyekundu.kwangu naona kana kwamba unawabeza sana watu wasio soma, huamini kwamba wao pia wanaweza kuwa na hiyo "input, process, and output".

  Ndg yangu kusoma ni suala jingine na kufanikiwa katika nyanja ya maisha hususani ktk mambo ya ujasiriamali nalo pia ni suala jingine.

  Sipendi nitoe mifano mingi sana hapa, lakini hebu mchukulie mtu kama bakheresa je amesoma sana mpaka kufikia hicho kiwango unachokiamini wewe?. Je kwa mtazamo wa haraka haraka hana hizo sifa za input, process, na output?.

  Asante ndugu yangu.
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  sitegemei mleta mada ataanza kujiajiri kwa kuanza na kazi ya shoeshine kama alivyoanza bakhresa. Bakhresa katoka mbali sana! Kingine kinachomsaidia ni asili yake pamoja na nguvukazi aliyo nayo. Hivi katika kubuni product mpya mfano azam cola unadhani ni akili ndogo imetumika? Anawatumia waajiriwa wake wasomi anaaowalipa vyema kumuendelezea biashara zake. Hivi unaweza kumlinganisha Mengi na Bakhresa? Kwa nini bakhresa sio public figure? Mengi naye alianzia mbali lakini tofauti. Alianza na product (nadhani ni kalamu za epica). Sasa angalia uendeshaji wa biashara kati ya Mengi na Bakhresa. Nafaka mtu yoyote anaweza cheza nayo ila si media na franchise.

  Pia sioni lugha yoyote kali iliyotumika hapo. Hivi utatoka na shahada yako chuoni halafu uende kufungua duka la nguo, kuna ubunifu hapo? ambaye hajasoma hufanikiwa pia ila in a hard way (kama bakhresa). Naye pia ana input, process na output, lakini sitegemei wewe uliyesoma uzikose hizo.
   
Loading...