Kwani Ajira ni nini.
Ukikimbilia mjini kichwa kichwa lazima usomeshwe Number tu.
Hakuna Nchi yoyote Duniani ambayo wananchi wake wote wana Ajira.
USA kwenyewe njaa kali vile vile,watu hawana Ajira,itakuwa hapa.
Uwezo wa kufikiri na kujituma,ndio mtaji wako.
Vijana wa Kiume wamekuwa hovyo sana,hatimae madada ndio wajasiriamali wenye mafanikio makubwa na kwa kasi kuliko vijana wa kiume wenye kutaka maisha ya mkato na muda mfupi.Ujanja ujanja,utapeli,dili za ajabu.Huku matumizi yakiwa makubwaa
Akili kumkichwa,maisha mepesi ukiwa na akili,ukishindwa rudi kijijini,watu wa mjini wanawekeza kwenye mashamba vijijini kwa sasa na vijana mmekimbia huko mnapishana na Maisha.
Mtu akifanikiwa mnasema Freemason,sasa watu tutulieee tuendelee kusema Mkulima Masanja na Diamond ni freemason wakati vijana hao wanatumia fursa huku tukiwapiga majungu.
Blessed vijana wote wenye kujituma