Wazo la biashara niliyoiyona kichwani

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
May 3, 2020
2,416
3,911
Wadau mambo Vipi mko poa? Nina wazo ila sina mtaji wa kuanzia nikipata wa kunishika mkono ntashukuru.

Ok. Plan yangu ipo hivi wazo langu ni kuwa nikiwa na kama sh 50,000 hizo zinatosha kabisa naenda kwenye duka la jumla linalouza nguo, za kiume/ kike za jumla mi plan yangu ni kuchukua zile nguo za ndani za kiume (boxer) dozen zipo tatu ndani ambayo kwa moja wao wanauza 3000 na kwa bei ya jumla unachukua kwa 9000

Ntachukua ntakazoona zinazonifaa harafu narudi mtaani kuwauzia wana kwa bei ya 5000 kila boxer moja mtaji ukikuwa naongeza na za kike kidogo ntazoona wadada watapenda.

Kwa mwenye mawazo anaweza akaongezea hapo.
 
Weka kwenye kubeti hyo elfu 50 chagua timu 5 tu za uhakika utakuja6 na mrejesho mzuri.
 
Uzi umekosa wachangiaji?
Wazo zuri mkuu hakuna kupata kudogo. Mi Kuna dada kani-inspire pale morogoro. Ye kaanzisha kijiwe Cha pilau tu, kuanzia saa nne asubuhi Hadi usiku Ni mwendo wa pilau na anauza kwa buku buku tu. Watu wanajaa hatari, yule dada anaweza kua anaangusha faida mpaka 50k kwa siku. Huwezi amini Ana Masters kabisa.
 
jirani yangu anafanya hiyo biashara juzi nilikuta waive kaninunulia kama hizo 3 in1 nikamwambia ulinunua wapi kaniambia jirani kaniuzia kwa mkopo ili uvae,nikamwambia hapana yaani jirani yako hadi ajue mume wako leo kavaa nguo gani ya ndani huko ni kuchorana tu,nikamwambia mrudishie nakupa elf15 nenda dukani kanichagulie.
 
jirani yangu anafanya hiyo biashara juzi nilikuta waive kaninunulia kama hizo 3 in1 nikamwambia ulinunua wapi kaniambia jirani kaniuzia kwa mkopo ili uvae,nikamwambia hapana yaani jirani yako hadi ajue mume wako leo kavaa nguo gani ya ndani huko ni kuchorana tu,nikamwambia mrudishie nakupa elf15 nenda dukani kanichagulie
Dah!
 
Wazo zuri mkuu hakuna kupata kudogo. Mi Kuna dada kani-inspire pale morogoro. Ye kaanzisha kijiwe Cha pilau tu, kuanzia saa nne asubuhi Hadi usiku Ni mwendo wa pilau na anauza kwa buku buku tu. Watu wanajaa hatari, yule dada anaweza kua anaangusha faida mpaka 50k kwa siku. Huwezi amini Ana Masters kabisa.
Mama Asha? Ila ye hana Msc...ni nan huyo? Yuko area ipi
 
Biashara katika kichwa ni simple Sana ila katika utekelezaji ni ngumu sana
Vibaya mno..ni mbingu na ardhi...ila mie katika maisha ya biashara naona biashara za kujilipua pays a lot..sio hizi za makaratasi sijui utafute kipenyo ..yaan namanisha ukiwa na wazo na linakusumbua sana hulali unaliwaza basi usilikawize jilipue zege halilali...utakutana na michangamoto komaa nayo tu mradi una passion na unachokifanya..hizi mambo za kuandika upate ushauri kwangu naonaga nux kishenzi...maana wakosoaji tupo tu
 
Back
Top Bottom