TANZIA Waziri William Lukuvi (na Mbunge wa Isimani) afariki Dunia

TANZIA Waziri William Lukuvi (na Mbunge wa Isimani) afariki Dunia

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
72,934
Reaction score
102,687
1774423214803.jpeg


Rais Samia, amesikitika kutangaza kifo cha William Vangimembe Lukuvi (Mb.), aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Isimani.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Lukuvi amefariki dunia leo tarehe 25 Machi, 2026, majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma, alipokuwa akipatiwa matibabu kufuatia ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Rais Samia ametoa salamu za pole kwa Spika wa Bunge, familia ya marehemu, wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa na marafiki, pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kufuatia msiba huo.
Screenshot 2026-03-25 at 10.03.51.png



Historia ya William Lukuvi

William Vangimembe Lukuvi ni mmoja wa wanasiasa mashuhuri wa Tanzania ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika masuala ya ardhi, maendeleo ya makazi, na siasa za kitaifa. Akiwa Mbunge wa Jimbo la Ismani kwa zaidi ya miaka 30 tangu mwaka 1995 mpaka kufariki mwaka 2026, Lukuvi ameshikilia nyadhifa mbalimbali za uwaziri.

Maisha ya Awali na Elimu
William Lukuvi alizaliwa tarehe 15 Agosti 1955 katika kijiji cha Mapogoro, Wilaya ya Iringa Vijijini, Tanganyika. Alipata mafunzo yake ya awali katika Tabora Teachers College (TTC) na baadaye kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Huria cha Tanzania.

Safari ya Kisiasa
Lukuvi alianza safari yake ya kisiasa kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ismani mnamo mwaka 1995 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), nafasi ambayo ameendelea kushikilia hadi amefariki Dunia March 25, 2026.

Aidha, amehudumu kama Waziri katika nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge.

Mnamo Juni 2023, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Mshauri wa Rais kuhusu Mahusiano ya Kisiasa na Kijamii na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 Rais Samia alimteua William Lukuvi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) nafasi ambayo ameishikilia mpaka kufariki kwakwe.

Zaidi, Soma=> CV ya William Lukuvi
 
WhatsApp Image 2026-03-25 at 09.55.07.jpeg
TAARIFA YA KIFO CHA MHE. WILLIAM VANGIMEMBE LUKUVI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anasikitika kutangaza kifo cha Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi (Mb.), aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, kilichotokea leo tarehe 25 Machi, 2026, majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Mheshimiwa Rais anatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, familia, wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huo.

Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka
KATIBU MKUU KIONGOZI 25 Machi, 2026​
 
Back
Top Bottom