Na mimi huyo waziri angesaidia kutatua tatizo moja. Nimeona mahali kiwanda cha dawa kilichopo hapa nchini kimenyimwa tender na mamlaka ya dawa na wamepewa kiwanda cha Kenya ilihali dawa wakenya walizonazo hata hicho kiwanda cha tanzania kinazizalisha tena kwa ubora mkubwa. Na sera ya rais JPM ni kuwa ataviwezesha viwanda vya ndani sasa hapa hawa wamekwenda kinyume sijui wanataka mwenye kiwanda afunge apunguze ajira ambazo watanzania zaid ya 150 waliyopata hapo warud mtaani kutuibia?
na nchi haiwez kukuza uchumi wake kama haina viwanda sasa kama serikali tu inashindwa kuvipa support viwanda vyake wanavyotaka watu wenye uwezo wavifungue itakuwaje?
Mfumo wa uzalishaji wa viwanda hapa Tanzania ni wa ajabu sana na hautakaa uendelee kamwe. Magufuli ananga'ngania viwanda lakini hajui tatizo la msingi ni nini.
Ujinga wa kushabikia imported goods kuanzia fukara hadi ikulu ndio chanzo. Hebu fikiria tunaimport wakati tunauwezo wa kuzalisha. Nani ataondoa tatizo hili? Hivi hata bendera za CCM mnaimport toka China si uenda wazimu huo?
- Sukari tunaimport
- Chumvi tunaimport
- Kiberiti
- Toothpicks
- Toothpaste
- wanja za akina mama
- soksi
- Sidiria
- Sabuni za mche za kufulia, za unga
- gloves za hospitalini
- Rubber band za kufungia hela
- viatu
- chupi, boxers
- mchele
- apples
- madaftari
- Kalamu
- pencil
- Sindano
- nyembe
List haiishi. Almost kila kitu tunaimport wakati tunaweza kuzalisha wenyewe. Viongozi wameuwa viwanda vyote kwa sababu ya syndicate hii ya maimpoters amabapo nao wamo. Hata aliye na kiwanda sasa hivi kinamshinda kwa sababu ya kodi nyingi na kubwa kuliko vinavyotoka nje. Umeme haupo na ukiwepo bei juu. Ukitenda serikalini hupati kwa sababu ya syndicate hii ya importers.
Cement ya nje ni bei rahisi kuliko ya Tanzania. Halafu kiongozi anazungumzia nchi ya viwanda. Nani atavunja hii syndicate? Shilingi yetu inaporomoka kila siku sababu ya hii syndicate of importers. Dola zinatafutwa kila kona kwenda kuleta mafanicha mabovu huko China na mnunuzi mkuu ni seriakali. What a shame?
Sipati picha Wachina wanapewa kazi ya ujenzi hapa nchini halafu wanaimport vyuma vyote toka China, wanaimport cement yote toka china, everything everything................ Halafu Magufuli anasema anataka viwanda. Mbaya zaidi hizo importations hazilipiwi hata
sumni. Mbaya zaidi ukikuta kiwanda cha chuma nchini unaambiwa kimepigwa ban kwa kutofikia vigezo au viwango, kumbe ni rushwa kwa watendaji wetu ili za china ziingie. Ni haSIRA HADI BASI. Sio ajabu Waziri akasimama akasema kifua mbele ninyi malofa mnaweza kuuza juice na maji tuu. Poor my country Tz.
Haya huyo Waziri na aje na mbinu za kuvunja hii syndicate , kinyume cha hapo ni bure tuu. Maigizo ya kutosha.