Ushauri kwa Rais JPM na Waziri mpya wa Viwanda na Biashara ili kukuza biashara na kupanua tax base

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Hongera Mhe. Rais kufanya mabadiliko ya haraka Wizarani baada ya kuona mchezaji Kakunda kapwaya.

Sifa kubwa sana ya Waziri na makatibu wakuu, lazima wao kuwashawishi Wizara ya Fedha na AG sheria ya kusajili kampuni, jina la biashara au kupata leseni visiwe under dictation ya TRA; TIN mfanyabiashara apate kama facility.

Ila kuna namna ya kuweka controls baada ya muda fulani toka biashara imeanza ndipo kodi zilipwe.

Maafisa wa TRA wasiwe na mandate ya kufunga biashara kama gia ya kumlazimisha mtu alipe kodi. Kama biashara hiafanyiki na kama mzunguko wa fedha haupo hamna kodi.

Wizara ije na mipango mikubwa ya ubunifu na dhamana kwa new business entrants. Mathalani, juzi Rais kapata deal ya kuuza mahindi tani laki 7 zimbabwe na tani zaidi ya laki 3 Namibia. Huu ilikuwa wakati wa Wizara kutoa facility ya government gurantee kwa kushirikiana na Wizara ya fedha Watanzania wapata mikopo wa kununua machinery, wasage unga na kufungasha na wengine wasafirishe mpaka sokoni. Pumba inayobakia inaingia katika kutengeneza chakula cha mifugo. Hii ndiyo dhana ya kuongeza thamani katika mazao.
Tuna-import Tani laki 4 za samaki/annum... hapa ni sehemu ya kuanzia... wizara ya biashara kwa kushirikiana na mifugo,
Tuna-import mafuta metric ton laki 320+; tunakuzaje zao la alizeti, ufuta, karanga, pamba kwa muda mfupi na wa kati ili mafuta haya yazalishwe ndani;
Tunanunua vifaa tiba vya thamani ya mabilioni kwa zaidi ya asilimia 97%; hapa kuna Watanzania wana projects za madawa na vifaa tiba na wana consultants wenye ku-guarantee to make the production happen. Namna gani tuna-wa incorporate on board.
Tuna-import maziwa ya thamani ya bil 50 mpaka 160/annum... Kuna Watanzania wapo wanaweza kuwa sehemu ya kupunguza imports na tukazalisha ndani.
Benki ya kilimo, namna gani inakaa na strategic start-ups
Kuna wakati Namba 1 akatoa ahadi mwenye nia ya kufungua kampuni hata ya Quarry, aje kwake amsaidie ili auze kokoto zake kwenye miradi ya ujenzi. Kuna Watanzania wapo waliandika hizo projects, issue ni red-tape za kumpata Namba moja.Wizara ya fedha na viwanda kuna watu ni either waoga au hawana inquisitive brain za namna gani hayo yakifanyika yanakuza biashara na kupanua tax base.

Mpango kama huo huo wa mahindi ungeweza kufanyika kwenye mazao mengi ya kimkakati kama Korosho, Ufuta... hamna haja kutegemea wahindi kuwa watu kati wa korosho, ufuta hana muhogo kwenda India au China kama raw material. Wizara ikija na mkakati wa kuwawezesha watu wenye business plan kupata equipment/machineries hii itaongeza thamani ya mazao ya kilimo, tutauza kwa bei kubwa, tutatengeneza ajira, TRA atapata tax base kubwa, huduma za UMEME, MAJI, TFDA/TBS wote watapanua wigo wa kupata wateja wapya na kufungua fursa za ajira.

Kwa akili ile ile ya serikali kuwa na bodi ya mikopo kwa elimu ya juu ambapo urejeshaji wake hauna uhakika sana kwa watu wasio na ajira, WIZARA ije na mfuko wa mikopo wa machinery kwa anaenzisha kiwanda kidogo na cha kati chenye lengo la kungeza thamani ya mazao, kupunguza imports za kile kinachoweza kuzalishwa ndani ili kupunguza gharama ya bidhaa na kukuza mzunguko wa ndani.

Kiufupi, biashara kwa sasa inategemea akili sana (intelligence tools) kama strategic economic intelligence tool, competitive intelligence tools ili ku-maximize mzunguko wa ndani kuwa mkubwa, hapo kodi itapatika based on sales of goods and services na spending za watu kununua huduma na bidhaa, hali kadhalika kula bata.

Wizara sio lazima kutegemea watu wenye vyeti vya degree za kwanza na masters pekee, na PhD; strategic economic intelligence tool, competitive intelligence tools zimezaa watu aina ya akina Jack Ma wa Alibaba (huyu ni mwalimu wa kingereza) ila alikuja na mkakati wa kibiashara kujenge network ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa China na ulimwengu. Leo ni mmoja wa mabilinea wakubwa. Wangem-assess based on certificate credentials asingefika kokote.

Kuna mengi ya kufanya na sio mbaya, serikali ikinusanusa kuna brain ndani ya Watanzania sio vibaya kuwapa avenue kwa kuwa-faciliatate wa explode kwenye biashara ili kukuza uchumi. Mifumo ya kuandika barua, ina urasimu, umangi meza... ila kama kuna sort of backdoor channels kuibua miradi ya kimkakati, kuna mengi sana yanaweza kufanyika. Watu wa intelligence wawe na jicho kama la explorers wa madini. Kwa kutambua brain ya Mtanzania huyu ikitumika vyema tunafika mbali, juhudi za kutumia moto, cyanid au mercury hutumika ili hatimae kupata dhahabu za kiakili. Siow watu wote wana akili za kikachero kwenye medani, ila kuna vichwa vina high quality & capacity ya kudevelop buz IQ

Haimhitaji Bashungwa peke yake, inahitaji umoja wa Kitaifa kukuza mambo haya. Wizara ya fedha hasa BOT nao wasisubiri tu watu wenye biashara kubwa za madini ndiyo iwape dhamana; kuna biashara mpya kabisa zaweza kupewa dhamana kama mtu ana business plan nzuri na inatatua tatizo/kukuza uzalishaji kwa haraka.

Wenzetu maslahi ya Taifa inajumuisha serikali kuzipigania private sector yao ikue. Juzi Xi Jing Ping alikuwa Russia kuwatafutia Deal Huwaei kusimika mitambo ya 5G. Huwaie washakuja mpaka Kenya, South Africa kuuza 5G products za telecom. Huwaei ni private sector ila inaongeza ukwasi wa wachina na kupanua tax base ya serikali ya China.

Mungu saidia mabilionea anaotaka JPM watokee tuwe na juhudi za makusudi kuwezesha watokee pasipo kutegemea default setting.

Siku kadhaa kabla ya mabadiliko ya Wazari wa Viwanda na Biashara nilishauri hiviii


Mungu Ibariki Tanzania, Mungu saidia biashara za Tanzania zikue tupate zaidi ya mabilionea wapya wengi
 
Pia ifike mahali watendaji katika taasisi za Serikali waanze kuwajibishwa. Hii ni kwa watendaji wa chini na wa kati. Kwa kweli watendaji wengi wa taasisi za Serikali ni wazembe sana. Ni mabingwa wa kukwamisha michakato mbali mbali ili kutengeneza mazingira ya rushwa.
Hivi inakuaje unafuatilia mfano building permit unaambiwa file halionekani!!?.
If possible kungeanzishwa kitengo maalumu cha kudeal na malalamiko ya watu ambao wanataka kuwekeza ila wanapata vikwazo toka taasisi mbali mbali. Kitengo chenyewe kiwe chini ya ofisi ya Rais. La sivyo itakuwa business as usually.
 
Back
Top Bottom