Waziri wa Utumishi na Katibu Mkuu Kiongozi, niwaombe mwarejeshe kazini waliofukuzwa kimakosa Kwa maamuzi ya kesi za prebagaining

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Naomba nitumie jukwaa la JF kuelezwa Jambo ambalo Watumishi wengi hasa wa Umma awalizungumzi ila Kwa anayefuatilia taratibu za kesi zilizofunguliwa 2015 watakubaliana na Mimi kwamba Watu waliteswa na wengine kupoteza kazi kwa utashi wa WATU wachache walioelekezwa kufanya walivyofanya.

1. Wapo Watumishi wengi wa Umma walikamatwa na kufukuzwa KAZI Kisha kupelekwa mahakamani kwa makosa ya uhujumu uchumi kutokana na tofauti za kisiasa, baadhi wazazi wao kuwa maadui wa Viongozi wa awamu ya Tano, wengine walibambikiwa kesi kwa sababu tu walionekana wanavuruga maslahi flani na wengine walikamatwa kwenye msafara wa wahalifu na kwa kuwa hakuna uchunguzi uliokuwa inafanyika basi walijikuta Wapo mahabusu kwa miezi au miaka.

2. Wapo watu walifunguliwa mashtaka kama njia ya utumbuaji, kwamba hakukuwa na sababu ya kumtumbua ila anayeteua amtaki na hataki aendelee kupokea mshahara baada ya kumtumbua. Hawa walitumbuliwa na kufunguliwa makosa ya uhujumu uchumi.

3. Wengine walituhumiwa kwa makosa yasiyo na uhusiano na uhujumu uchumi wakapigwa uhujumu uchumi wakose dhamana na huku mahakamani kila siku wakisomeka uchunguzi unaendelea.

Baada ya kukaa gerezani muda bila kesi zao kusikilizwa, ofisi ya DPP ikaweka utaratibu wa watu kukiri kosa ili usamehewe na kurejea Uraiani. Watumishi wengi kama walivyowafanyabiashara wakanunua Uhuru wao na kurejea Uraiani. Kitendo cha pre bagaining kikaenda kuandika ukomo wa Utumishi wao pamoja na maslahi yao yote.

Wengine wakati wakiendelea na taratibu na wakisubiri maamuzi ya DPP ndipo ikaingia awamu ya sita na hivyo kuelekeza kesi zisizo na sifa zifutwe. Hapa wakafutiwa kesi watumishi wa umma na wafanyabiashara.

Kiutaratibu watumishi wote waliofutiwa kesi wamerejeshwa kazinj kwa sababu awakupatikana na hatia mahakamani. Lakini wale walioona wanateseka wakakubaliana na DPP bila kesi zao kusikilizwa walifukuzwa KAZI.

Huu utaratibu kwenye macho ya kosheria hakuna tatizo ila kwenye macho ya watu wanaopenda haki kuna tatizo tena kubwa sana.

Kuondoa mkinzano wa kosheria na kikanuni na Katika hali ya kibinadamu Wapo watumishi wamerejeshwa kazini baada ya pre- bagaining lakini Wapo wengine taasisi walizokuwa wanazifanyia kazi zimekataa hata kupokea maombi yao yakuomba wafuatilowe suala la ajira zao.

Maafisa Utumishi waliogoma kusikiliza Watumishi hao siwalaumu maana wanasimamia sheria na wale waliosimama kidete wenzao wakarejeshwa kazini siwalaumu maana waliongozwa Zaidi na utu kuliko kusimamia dhuluma.

Lakini kwa kuwa serikali ni moja na katika kusimamia haki nimwombe mtetezi wa watumishi Mdogo wangu Mchengerwa aunde timu yakupitia majalada Yote watumishi waliokiri makosa kwa dpp na kujiridhisha kama kulikuwepo na kesi ? Ushahidi ulikuwepo? Kwanini walilamika kwenda kwenye prebagaining? Kisha timu hiyo imshauri wangapi walionewa na wangapi hawakuonewa kisha walioonewa warejeshwe kazini.

Hii inaweza kuwa NJ mojawapo yakurejesha Imani ya Watumishi hasa wale walioshuhudia Watumishi wachapakazi na wasio na doa wakiswekwa ndani nakufukizwa kazi Kwa sababu ziszo wazi.

Makati wakuu fanyeni pia kazi hii yakuhusaidia Utumishi wa umma. Nimeandika maana najua Wapo watu wengi waliumizwa. Lakini ninao watu ambao wazazi wao walipishana na awamu iliyopita wakakamatwa watoto na kufukuzwa kazi ila awamu hii wamerudi. Zoezi lakuwasaidia walioteswa liwe la watu wote siyo la vigogo na wafanyabiashara, waangalieni wote na mtende haki. Angalieni pia Mawakili binafsi waliopoteza uwakili na watendaji wengine.
 
Wapambanie chokambaya wenzako watakuombea ata dua sio unajipendekeza kwa mwabwanyenye
 
Naomba nitumie jukwaa la JF kuelezwa Jambo ambalo Watumishi wengi hasa wa Umma awalizungumzi ila Kwa anayefuatilia taratibu za kesi zilizofunguliwa 2015 watakubaliana na Mimi kwamba WATU waliteswa na wengine kupoteza KAZI kwa utashi wa WATU wachache walioelekezwa kufanya walivyofanya...
Wataje majina yao kamabu awajua,
 
Je watumishi waliotengenezewa njama.. Na kuondolewa makusudi.. Kisha wakaamua yaishe na wako vijijini choka mbaya watawapataje?
 
Hapa hoja yangu imejikita Zaid kwa KUNDI kubwa lisilo na wakuwasemea, watoto wa vigogo wengi muda huu watakuwa Wana ajira nyingine au wamerejeshewa kazi za awali bila kujali walikiri kosa au la.

Makabwela wengi hakuna wakuwasemea na may be hata Mhe. Waziri hana taarifa kwamba Wapo watu ambao majalada yao Kwa DPP au TAKUKURU hayana ushahidi wowote ila waliwekwa ndani Kwa amri. Waliwekwa ndani Kwa hisia za wenye nguvu

Tukipaza sauti au kuchokonoa mada Kama hizi tunafungua mjadala wakuponya nafsi za wengi. Wapo watoto watashindwa kuvaa uniform mwakani kisa a baba aliwekwa ndani familia ikauza kila kitu.

Nizidi kutoa wito waajiri wapiganieni waajiriwa, vyama vya wafanyakazi wapiganieni wafanyakazi.

Hoja kama hizi ilipaswa kutwala mei mosi na mabaraza wafanyakazi yalipaswa kuwa na data za wafanyakazi wote na kuomba waruhusiwe kuona tuhuma za Watumishi.

Waajiri na waajiriwa msipojisemea keaho mtaumizwa ninyi na waliobaki watakaa kimya
 
Back
Top Bottom