Waziri wa Ulinzi na JKT amkabidhi Mkuu wa Majeshi wa Kwanza Mstaafu (Jenerali Sarakikya) gari jipya la kisasa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 06 Juni, 2025 amemkabidhi Mkuu wa Majeshi wa kwanza mstaafu Jenerali Mirisho Sam Hagai Sarakikya gari jipya la kisasa aina ya Toyota VXR nyumbani kwake Arumeru nje kidogo ya Jiji la Arusha.
WhatsApp Image 2025-06-06 at 20.42.59_2bd95142.jpg

WhatsApp Image 2025-06-06 at 20.42.59_9d6f7397.jpg
Akiongea muda mfupi kabla ya kumkabidhi gari hilo aina ya Toyota VXR toleo jipya la mwaka 2025 Mhe. Waziri Tax amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya na Majenerali wengine waliostaafu, ambapo amesema pamoja na kwamba hii ni stahiki yake, lakini stahiki hiyo inatokana na kutambua mchango wa Wakuu wa Majeshi wastaafu katika Ulinzi wa Taifa letu, lakini kipekee mchango wa Jenerali Sarakikya kama Muasisi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambalo Jenerali Sarakikya alianza nalo hadi lilipobadilishwa, na Jenerali Sarakikya aliyekuwepo na kuweka misingi yote iliyo bora na kuwafanya Wakuu wa Majeshi waliofuata kukuta misingi mazuri ambayo imewezesha Taifa la Tanzania kuwa imara.

Waziri Tax akaongeza kwa kusema “Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan analithamini sana Jeshi lake, anawathamini sana nyinyi waanzilishi, anawathamini sana wote waliochangia katika kuimarisha Ulinzi wa Taifa letu kuhakikisha mipaka ipo salama, uhuru wetu hauteteleki, mapinduzi yetu hayateteleki na Katiba yetu inabaki salama. Kwahiyo kwa kulitambua hilo amewezesha Majenerali wale wote waliokuwa wamefikia muda wa kubadilishiwa magari wabadilishiwe, hivyo naomba nikukabidhi gari hili ili liendelee kukusaidia na kukupa faraja katika maisha yako pamoja na kwamba umestaafu bado ni hazina na uendelee kutusaidia” alisema Mhe. Waziri wa Ulinzi na JKT, Tax.
WhatsApp Image 2025-06-06 at 20.43.02_6f106096.jpg

WhatsApp Image 2025-06-06 at 20.43.00_4c112a83.jpg

WhatsApp Image 2025-06-06 at 20.43.03_078d7c0c.jpg
Awali akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na JKT ili akabidhi gari hilo kwa Mkuu wa Majeshi wa Kwanza Mstaafu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe alisema kuwa tukio la kukabidhi gari lililonunuliwa na Serikali, toleo la mwaka 2025 ni stahiki ya Wakuu wa Majeshi Wastaafu kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Ulinzi wa Taifa ya mwaka 1966 pamoja na kanuni zake za mwaka 2015 ambazo zinasema Jenerali wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania baada ya kustaafu atakabidhiwa Gari Jipya la wakati husika.

Naye Mkuu wa Majeshi wa Kwanza, Mstaafu na Mkuu wa Majeshi Muasisi wa JWTZ, Jenerali Sarakikya amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kuendelea kuwakumbuka wastaafu, na pia amemshukuru Waziri wa Ulinzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi kwa kuwa nguzo imara kwao Wastaafu.
WhatsApp Image 2025-06-06 at 20.43.03_a650bae9.jpg
Hafla ya kumkabidhi gari kwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu wa kwanza, Jenerali Sarakikya imehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda , Maafisa Wakuu, Maafisa wadogo na Wapiganaji.
 
Sawa wenye nacho wanaongezeana tu mpk wanapofikishana kaburini ..hapo Bado ajafa aje azikwe kishujaa Tena Kwa gharama kubwa kubwa za serikali uku mambo Bado n bila bila Kwa wananchi...
 
hivi yule aliyefariki majuzi ma miaka 100+ anaitwa nani?

Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ​

Mwaka 1964 hadi 1974 liliongozwa na Jenerali Mirisho Sarakikya

Mwaka 1974 hadi 1980 liliongozwa na Jenerali Abdalah Twalipo.

Mwaka 1980 hadi 1988 liliongozwa na Jenerali David Musuguri.

Mwaka 1988 hadi 1994 liliongozwa na Jenerali Mwita Kiaro.

Mwaka 1994 hadi 2001 liliongozwa na Jenerali Robert Mboma.

Mwaka 2001 hadi 2007 liliongozwa na Jenerali George Waitara.

Mwaka 2007 hadi 2017 liliongozwa na Jenerali Davis Mwamunyange

Mwaka 2017 hadi 2022 liliongozwa na Jenerali Venance Mabeyo

Mwaka 2022 hadi sasa linaongozwa na Jenerali Jacob Mkunda
 
Hakuna shida hawa watunzwe vizuri ni mashujaa wa nchi yetu ni haki yao ila msiwasahau wastaafu wengine wa zamani wa jeshi hasa wa kipindi cha mkapa kushuka chini wanamaisha magumu sana isee pension zao ni kituko..
 
Sawa wenye nacho wanaongezeana tu mpk wanapofikishana kaburini ..hapo Bado ajafa aje azikwe kishujaa Tena Kwa gharama kubwa kubwa za serikali uku mambo Bado n bila bila Kwa wananchi...
Huyu Mchango wake katika Ulinzi wa Taifa hili auna mfano! Nimewai kufanya nae some projects miaka ya 20xx.Alafu tofautisha wanasiasa na Jeshi.Akuna mwanajeshi anaengangania Madaraka.na Mwanajeshi astaafu.anastaafu just as formality.ila akiitajika.24/7 yupo. Na pia yupo fiti mpaka leo japo ana miaka zaidi ya 80+ na ana hobby ya kupanda mliman kilimanjaro kila mwaka (japo toka mwaka juzi ajapanda) na hizo ishu za kutunzwa na kuzikwa na Serikali etc.... Ni sheria zilizopitishwa na Bunge halali!acha Makasiliko-somesha watoto wako walau atoke Diwani
😃😃
Karibu USA River Arusha.Uje akupe nondo.Nyerere alikuwa afanyi kazi na VIMEO! Huyu kama Nyerere alimkubali basi ni Kichwa,Mzalendo na Kiongozi alietukuka....Ukipata Wasaa mtafute Jakaya Kikwete akupe story za huyu mwamba
 
Attachments

  • images - 2025-06-06T213344.002.jpeg
    images - 2025-06-06T213344.002.jpeg
    7.8 KB · Views: 16
  • images - 2025-06-06T213337.473.jpeg
    images - 2025-06-06T213337.473.jpeg
    15.3 KB · Views: 23
  • images - 2025-06-06T213333.990.jpeg
    images - 2025-06-06T213333.990.jpeg
    11.8 KB · Views: 22
  • download - 2025-06-06T213321.397.jpeg
    download - 2025-06-06T213321.397.jpeg
    9.1 KB · Views: 16
Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe alisema kuwa tukio la kukabidhi gari lililonunuliwa na Serikali, toleo la mwaka 2025 ni stahiki ya Wakuu wa Majeshi Wastaafu kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Ulinzi wa Taifa ya mwaka 1966

jenerali wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania baada ya kustaafu atakabidhiwa Gari Jipya la wakati husika.
hiyo siyo zawadi ni stahiki yake
 
Alafu tofautisha wanasiasa na Jeshi.
Kuna tofauti gan mkuu wangu hapo,maana nachojua huyo mwanajeshi Kila kitu anachotumia na anacholipwa kinapangwa na mwanasiasa 🤔🤔🤔
 
unajua kwa nini Bendera ushushwa kila jioni??na kupandishwa kila asbuhi??
 
Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ​

Mwaka 1964 hadi 1974 liliongozwa na Jenerali Mirisho Sarakikya

Mwaka 1974 hadi 1980 liliongozwa na Jenerali Abdalah Twalipo.

Mwaka 1980 hadi 1988 liliongozwa na Jenerali David Musuguri.

Mwaka 1988 hadi 1994 liliongozwa na Jenerali Mwita Kiaro.

Mwaka 1994 hadi 2001 liliongozwa na Jenerali Robert Mboma.

Mwaka 2001 hadi 2007 liliongozwa na Jenerali George Waitara.

Mwaka 2007 hadi 2017 liliongozwa na Jenerali Davis Mwamunyange

Mwaka 2017 hadi 2022 liliongozwa na Jenerali Venance Mabeyo

Mwaka 2022 hadi sasa linaongozwa na Jenerali Jacob Mkunda
Mabeyo hovyo sana. Huyu kizazi cha mbele kitamlaani sana.
 
Hakuna shida hawa watunzwe vizuri ni mashujaa wa nchi yetu ni haki yao ila msiwasahau wastaafu wengine wa zamani wa jeshi hasa wa kipindi cha mkapa kushuka chini wanamaisha magumu sana isee pension zao ni kituko..
Ni aibu wastaafu hapa kitaa wa miaka 2010 kurudi nyuma ,wengi wamekuwa walinzi ,wamwchoka balaa mpaka nashangaa.
 
Back
Top Bottom