Waziri wa Ujenzi atoa maelekezo mawasiliano Barabara ya Dar - Lindi yarejee ndani ya Saa 72

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,896
12,146
WhatsApp Image 2024-05-05 at 19.39.02_be92bd20.jpg
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameeleza kuwa timu ya watalaamu wa Wakala ya Barabara (TANROADS) na Makandarasi itatumia saa 72 (siku 3) kukamilisha zoezi la kurejesha miundombinu ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam, ambayo imeharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zilizombatana na kimbunga Hidaya.

Amesema hayo Mkoani Lindi Mei 05, 2024, mara baada ya kuwasili na kukagua uharibifu wa miundombinu ya barabara ya Lindi - Dar es Salaam na kuzungumza na wananchi na wasafiri wa Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, na Dar es Salaam wanaotumia barabara hiyo na kutoa pole na kuwataka kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kujereshwa miundombinu.
WhatsApp Image 2024-05-05 at 19.39.01_62eb3f56.jpg

WhatsApp Image 2024-05-05 at 19.39.00_106b2afe.jpg

WhatsApp Image 2024-05-05 at 19.39.01_9ce9ee2d.jpg

“Mitambo ipo inaletwa hapa, kazi ya kurudisha mawasiliano ya barabara hii itaanza wakati wowote kuanzia sasa, ni lazima tuanze na kipande kimoja ili tuweze kufika katika maeneo mengine yaliyoathiriwa. Namna miundombinu imeharibika na tathmini iliyofanyika tunahitaji masaa yasiyopungua 72 ili kuweza kurudisha mawasiliano,” amefafanua Bashungwa.

Bashungwa ameeleza kuwa mawasiliano ya barabara hiyo yamekatika katika maeneo matano ambayo ni pamoja na eneo la barabara ya Somanga – Mtama, eneo la Mikereng’ende kutokea Somanga na eneo la Lingaula kutokea Lindi.

Aidha, Bashungwa amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itafanya kila jitihada ili ifikapo Jumatano jioni mawasiliano ya barabara hiyo yarejee katika hali yake.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo ameeleza kuwa maji yaliyokuwa yakipita juu ya barabara yalizidi kiwango na kusababisha madaraja kushindwa kuhimili wingi na kasi ya maji na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa katika maeneo matano ikiwemo Somanga, Mikereng’ende, na Lingaula.

Nyundo amemueleza Waziri Bashungwa kuwa kazi ya awali iliyofanyika ni kuwasiliana na taasisi zinazohusika kwa Mkoa wa Ruvuma, Mtwara na Lindi ili kutoa taarifa kwa wasafirishaji na watumiaji wa barabara hiyo kusimamia safari zao mpaka pale miundombinu itakaporejeshwa katika hali yake.

Pia soma - Barabara Kuu ya Dar- Lindi imekatika sehemu 2 na kukata mawasilino
 
BABA MUNGU AKAWATIE NGUVU KATIKA UJENZI HUU MPYA WA BARABARA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.

AMINA.
 
Me Bashungwa namuonaga kama Hana Haiba na uwaziri

Sijui wengine mnamuonaje?
 
Siku 3 nyingi sana.
Kwa ule uharibu ni siku chache sana hizo. Jamaa namuonea huruma huu mwaka wote tokea umeanza anazunguka kwenye mafuriko huko kusini.

Tutamjengea ofisi ndogo kabisa awe anakaa huko kipindi cha mvua.
 
Nchi kwa Maigizo haijambo hii, ujenzi wa barabara siku 3? Ikifika mvua inabomoa tena, pesa za kuchezea zipoo.
 
Back
Top Bottom