Waziri wa Mifugo kubishana hadharani na Rais ni utovu wa nidhamu

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Tumeshuhudia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akipinga hadharani maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyeagiza vitalu vya NARCO vifutwe na kupewa vijana wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo SUA ili kutengeza fursa za ajira kupitia ufugaji

Mambo ambayo Waziri alipaswa kuyafanya ni mawili ama kutekeleza maagizo aliyopewa na Mh. Rais kama yalivyo ama kuandika barua ya kujiuzulu na sio kupingana na Mh Rais hadharani na kusema kabisa kwamba anaunda timu ya wataalamu ili kuishauri Serikali.

Hii ni sehemu ya nukuu ya Waziri Mashimba " jambo hili tumelipima na tukaliona linahitaji umakini mkubwa na kwa hiyo ili kutekeleza jambo hili wizara tumeunda timu ya wataalamu kutoka wizara na taasisi mbalimbali zinazohusika na mambo mbalimbali sasa timu hii tunataka ifanye tathmini ya kina ya utendaji na changamoto zilizoko ndani ya Narco ili tuweze kuishauri sawasawa Serikali"

Huu ni utovu wa nidhamu uliopitiliza lakini tukisema humu mnaanza kuhusisha mambo yenu ya udini na ukabila, sijawahi kuona Waziri anapingana na Rais wake kwa sababu madaraka ya waziri amekasimiwa na Mh Rais sasa unaposema anaundia timu ya wataalamu maagizo ya Mh Rais maana yake nini.
 
acheni kutetea ujinga Mawaziri wangapi wametumbuliwa. ametumbuliwa Kabudi, Lukuvi, Kalemani, Ndugulile, Kitila Mkumbo, Mwambe, Chamuriho, Prof. Manya, Mwita Waitara na wote hao hawajawahi kujibizana na Mh. Rais hadharani kwa lolote
 
Tumeshuhudia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akipinga hadharani maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyeagiza vitalu vya NARCO vifutwe na kupewa vijana wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo SUA ili kutengeza fursa za ajira kupitia ufugaji

Mambo ambayo Waziri alipaswa kuyafanya ni mawili ama kutekeleza maagizo aliyopewa na Mh. Rais kama yalivyo ama kuandika barua ya kujiuzulu na sio kupingana na Mh Rais hadharani na kusema kabisa kwamba anaunda timu ya wataalamu ili kuishauri Sekali.

Hii ni sehemu ya nukuu ya Waziri Mashimba " jambo hili tumelipima na tukaliona linahitaji umakini mkubwa na kwa hiyo ili kutekeleza jambo hili wizara tumeunda timu ya wataalamu kutoka wizara na taasisi mbalimbali zinazohusika na mambo mbalimbali sasa timu hii tunataka ifanye tathmini ya kina ya utendaji na changamoto zilizoko ndani ya Narco ili tuweze kuishauri sawasawa Serikali"

Huu ni utovu wa nidhamu uliopitiliza lakini tukisema humu mnaanza kuhusisha mambo yenu ya udini na ukabila, sijawahi kuona Waziri anapingana na Rais wake kwa sababu madaraka ya waziri amekasimiwa na Mh Rais sasa unaposema anaundia timu ya wataalamu maagizo ya Mh Rais maana yake nini.
Posho unayopata si haba!
 
Back
Top Bottom