Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari: Bei elekezi ya Data itaanzia Shs 2-9 kwa MB 1 kuanzia Aprili 02, 2021

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ndugu Ndungulile akizungumza katika kipindi cha Clouds 360 amesema, nanukuu:"Bei elekezi ya Data itaanzia Shs 2-9 kwa MB 1 kuanzia April 2"

"Hakuna upandishaji holela wa bando mpaka baada ya miezi mitatu ipite, kampuni hazitaruhusiwa kupunguza spidi ya bando" Mwisho wa kunukuu.

Hii inamaanisha nini? Maana yake ni kwamba:
9TSH=1MB
XTSH=1000MB

Ukitafuta thamani ya X hapo juu utagundua kuwa kampuni za simu zimeruhusiwa kucharge hadi TSH 9000 kwa 1GB! Hili ni pigo kubwa sana kwa watumiaji wa internet pamoja na uchumi kwa ujumla kwa sababu katika karne ya 21 uchumi endelevu na thabiti unategemea sana matumizi ya internet. Watumiaji wa internet wakae mkao wa kuumia zaidi kwa sababu gharama za internet zilizo juu sasa hivi ni manyunyu tu, the worst is yet to come.

Waziri aliahidi kushughulikia suala la vifurushi vya internet kuwa juu lakini ambacho wengi walikuwa hawajui ni kwamba waziri alikuwa anaenda kupandisha zaidi gharama za vifurushi.

Source: Cloudsmedia twitter page

=======

WAZIRI NDUGULILE: Nimeingia ndani ya wizara hii tulikuwa hatuna bei elekezi ya mabando, hayakuwepo kama ilivyo kwenye mafuta, umeme wala katika maji, hayakuwepo. Kwahiyo katika utaratibu huu sasa tumetoa bei elekezi ya data kwahiyo itaanzia shilingi 2 mpaka shilingi 9, makampuni ya simu hayapaswi kwenda zaidi ya hapo kwa MB moja, kwahiyo hiyo bei elekezi tumeitoa na sasa hivi makampuni yote ya simu itabidi yazingatie bei hiyo.

Pili ambalo tumelifanya ni kuhakikisha sasa hamna upandishaji holela wa holela, tumeweka taratibu ambazo bando likitolewa leo, limezinduliwa leo na TCRA wakalipitisha hautaruhusiwa uje ufanye mabadiliko yoyote mpaka baada ya miezi mitatu ipite, nayo itakuwa inaleta stability katika soko.

Tatu ambalo tumelifanyia kazi ni wananchi kusema mabando yao kuisha kabla ya muda. Sasa hivi kutakuwa na mabando ambayo hayana ukomo, wewe ukinunua iwe mwezi mmoja, miwili, mitatu mpaka liishe ndiyo unanunua tena lakini kuna wenzangu na mimi ambao kununua bando ambalo halina ukomo hawana, wana bando lao la siku, wiki na mwezi, hata wao tumewatengenezea mazingira vilevile. Kwa mfano umenunua GB 10 wiki hii, umetumia umeona umebakiza siku tatu, umebakiza GB 5. Kuna mambo mawili unaweza ukayafanya, moja sasa hivi kutakuwa na uwezo wa kugawa GB 5 iliyobaki kwa mwenzako katika mtandao uleule, hilo nalo tumeweza kulifanya, tumeshatoa maelekezo au unaweza ukanunua bando lilelile la GB 10, ile 5 inahamia huku unakuwa na 15.

=====

Nitumie fursa hii kuongea na watanzania, moja kuna namba *106# na niwaombe sana kila mtanzania, ingia pale, ingiza kitambulisho ambacho umekisajilia, utaona namba ambazo zimesajiliwa kwa jina lako, kama huitambui namba yoyote pale, nenda kaifute.

Pili tunafanya sasahivi uhakiki wa namba tena kwa kushirikiana na makampuni ya simu na TCRA, kuna uhakiki ambao utakuwa unaendelea wa namba za simu.

Tatu, tumetoa namba 15040, namba yoyote inayokwambia tuma hela kwenye namba hii au sijui umeshinda bahati nasibu au mimi ndie mganga fanya hivi sijui na nini au wale ambao wanasema mimi ni Sam Sasali wakati sio Sam Sasali, bwana siwezi kuongea nitumie hela kwenye namba hii. Zile namba unapeleka 15040, tunataka sasa tuweke mfumo wa kuwa tunashughulikia yale malalamiko.

Jingine ambalo niwaombe sana na ambalo watanzania wanapigwa na huu usajili wa laini mitaani, usajili wa laini mitaani, unaenda kusajili mtu anakwambia weka kidole hiki, anakuambia hakijasoma, weka kidole hiki. Kila moja ile ni laini imesajiliwa, kwahiyo zile sasa wanaziuza kwa wahalifu.

Linatokea tukio la uhalifu, unakuja unamtafuta unakuta ni PJ, PJ kafanya tukio Manyara. Nalo hili tunaenda kuimarisha mifumo ya mawakala na mimi nimesema ni lazma makampuni ya simu yaimarishe mifumo ya mawakala wao, sisi ikitokea uhalifu katika mitandao tutaziwajibisha kampuni za simu.

Pigo kubwa sana hili, tatizo wazee wetu wanazungumza Bila kutafakari,
Assume mtu una internet cafe,
Vipi kwa sisi tunaotegemea data katika kujisomea hasa wanafunzi wa vyuo vikuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao ni Vodacom wanakula 29tshs per 1mb, vipi kuhusu mitandao mingine kwa sasa
 

Attachments

  • D6047555-8748-49D3-9373-45350B59CC9F.png
    D6047555-8748-49D3-9373-45350B59CC9F.png
    55.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom