Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari: Bei elekezi ya Data itaanzia Shs 2-9 kwa MB 1 kuanzia Aprili 02, 2021

Mtoa mada kachanganya,hajui kuwa kabla ya mabadiliko hayo mb moja ilikuwa na wastani wa TSH 124
Pia hapo kwenye sh 2_9 Ni kwa mtu ambaye anatumia salio la kawaida ambalo ni non bundle
Waziri amesema ni bando,angalia video iliyopo kwenye uzi
 
Wametuona mazuzu😀 1024*2= 2048 in maana ukiuziwa kwa bei ndogo kabisa Gb 1 itakua Tsh 2048, hapa watakua wamepunguza Nini?😀
Na ukiuziwa kwa bei kubwa zaidi Ni TZS 9,000/-. Hajasema hata ni wakati gani watoze TZS 9/Mb na wakati gani watoze TZS 2/Mb. Ina maana wengi watakimbilia kutoza TZS 9.

Hapo kabla Airtel walikua wakitoza TZS1/Mb Uni-Offer, lakini Sasa wanatoza TZS2/Mb. Perhaps walijua hili linakuja. Serikali inajifanya inatusaidia lakini kwa hili ndio inatukaanga zaidi.

Wangeweka uko wa juu (maximum) kisha wawaachie makampuni wapambane wenyewe kwenye kushusha bei, lakini kuwawekea na minimum ni kutubana sisi wananchi
 
Hiyo shilingi 2 ndiyo bei kwa iliyopo kwa airtelView attachment 1720184
Acha uongo
IMG_20210309_062752.jpeg
 
Kama umenitumia ile mimeseji ya mjukuu wangu mbona kimya toka nimekutumia ile ndangu ya kupata utajiri?? Sasa nai forward hiyo msg yako kwenda TCRA na pia naweka namba yako iliyokuja kwangu. Wakifuatilia huko wataona kweli ulinutumia hiyo msg so wanakudaka bila kuonewa hapo.
Hujanielewa mimi nina kisa tu na wewe, ninatuma namba yako kwenye 15040.

Je, ikigundulika wewe siyo tapeli, kuna hatua zozote watakazonichukulia mimi??
Maana hizi huduma wapo wanaozitumia vibaya.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Bando yako ya intaneti imekwisha. Peruzi intaneti kwa Tsh 5/MB tu kwa kutumia mda wako wa maongezi Piga *149*99#, chagua 5, chagua 11. Au Nunua bando mpya
 
Hili swala bado ni kizunguzungu kwa kweli sioni kama serikali imesaidia zaidi ya kutu umiza zaidi. Mimi maswali nayo jiuliza ni rahisi tu, Hivi ule mkonga mkubwa wa internet ulilazwa baharini kusaidia nchi za dunia ya tatu kusaidia mawasiliano uliishia wapi? Je kama upo nini kazi ya huo mkonga? Je nani ana nufaika na huo mkonga? Je ni lini tutanufaika na huo mkonga?
Nadhani haya maswali ndio maziri angeanza kujibu alafu tuje sasa kwenye garama za mawasiliano.
 
Hii inamaanisha nini? Maana yake ni kwamba:
9TSH=1MB
XTSH=1000MB
Hii bei itakuwa ghali mara kumi zaidi ya bei za vifurushi ambazo zipo kwenye soko sasa hivi. Kama kweli Mh Waziri alimaanisha kupunguza bei ya vifurushi, basi alitakiwa aseme bei kuanzia senti 10 (0.10 Tshs) mpaka shillingi moja (1.0 Tshs) kwa MB moja.

Nadhani pengine hiki ndicho alichokuwa anataka kusema ila akawa amepitiwa. Kwa bei hiyo bora waache bei ya soko iliyopo sasa hivi iendelee
 
Hawezi sema hivyooo serikali imekaa kipigajii tu nayooo.. Lengo ni kuongeza mapato yani kama tutaumia ni sisi na maisha yetu...!! Waziri anaongea ujinga kama huu si afadhali asiongeongea...

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Huu ujumbe niliwahi kuupata kwenye simu yangu halafu nilipofanya mahesabu hofu niliyoipata baada ya hapo ilibidi nianze kutetemeka mithili ya mtu aliyeona simba mbele yake. Unajua nini, kuna watu ambao hawajui kabisa namna data za internet zinavyosomwa. Yaani unakuta mtu anatumia data tu na hajui uhisano uliopo kati ya B, KB, MB, GB (au TB, sometimes in the future). Kwa hiyo akiambiwa sh 5/MB yeye anaona ni pesa ndogo, kumbe ukweli ni kuwa akifanya hivyo anaweza akapoteza ndani ya saa moja tu, hela ambayo angeweza kununua hata bundle ya kutumia wiki nzima,
 
Ndugulile tokea Makonda atake kumnyang'anya Jimbo amekuwa mtu wa jabu sana.Nlitaraji wasema 1GB isizidi 1000 sasa 1 gb wanauza 2000.Kwa lugha nyingine ni kwamba gharama zitakuwa kubwa sana kiasi kwamba hakuna atakayeweza kumuda tena kutumia mtandao.Useless nation.
 
Yale majambazi tu mtandaoni yameyashinda yamesajili namba na yanadunda tu mtaani

Hapa ni vita ya vilaza VS akili kubwa
Tunaendelea kupata matokeo
 
Hii bei itakuwa ghali mara kumi zaidi ya bei za vifurushi ambazo zipo kwenye soko sasa hivi. Kama kweli Mh Waziri alimaanisha kupunguza bei ya vifurushi, basi alitakiwa aseme bei kuanzia senti 10 (0.10 Tshs) mpaka shillingi moja (1.0 Tshs) kwa MB moja.

Nadhani pengine hiki ndicho alichokuwa anataka kusema ila akawa amepitiwa. Kwa bei hiyo bora waache bei ya soko iliyopo sasa hivi iendelee
Ni ishu za tamaa ya serekali iliyokosa weledi kuua makampuni kupitia kodi kubwa.Gharama ndiyo hizo mkuu,ni mambo ya kodi.
 
Back
Top Bottom