Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,921
- 15,613
Waziri wa mambo ya nje wa South Afrika kamchana Blinken kuwa South Afrika na Afrika kwa ujumla hawataki siasa za kipumb2vu za Marekani za kulazimisha kuchaguliana maadui au marafiki.
Maneno hayo yamejiri baada ya Biden wa Marekani kumtuma waziri wake wa mambo ya nje Bwana Blinken aende South Afrika, DR Congo na Rwanda akazipigie magoti nchi hizo za Afrika na kuziomba ziiunge mkono Marekani na kuwa upande wa Marekani ktk suala la vita vya Ukraine. Sanjari na hilo ni pamoja na kuziomba nchi hizo za Afrika zijiweke mbali na Urusi na China.
Waziri wa mambo ya nje wa South Afrika Bi Naledi Pandor anasema pamoja na kuwa Blinken alijifanya kudai kuwa Marekani haiilazimishi Afrika kuchagua upande ktk mizozo inayoihusisha Marekani, Blinken alishindwa kuficha ukweli juu ya mswaada uliopitishwa Marekani wa kuitaka serikali ya Marekani kuziwajibisha nchi za Afrika zilizokataa kupiga kura Umoja wa Mataifa ya kuilaani Urusi. Bi Naledi akampa maneno ya shombo Biden kupitia waziri wake (Blinken) kuwa South Afrika yaamini ktk UHURU, na uhuru wenyewe ni uhuru wa kila mtu kila nchi. Huwezi kusema kwa kuwa Afrika imeamua kufanya hivi (haiiungi mkono Marekani) basi lazima Afrika iadhibiwe na Marekani!
Mwana mama huyo machachari akamuonya Blinken kwa kumweleza kuwa Afrika haitaki siasa za kishamba za Marekani za kuitaka Afrika kuzitenga Urusi na China.
=======