Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amepatwa na nini?

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amepatwa na nini?

Hata Corona ilijaa kila sehemu lakini Tanzania tulikuwa na jibu letu.

Tanzania haiwezi kuwa nchi ya kukopi na kupesti hata mambo ya kijinga kutoka nchi zingine ~~~~JPM
Wewe unaongelea corona ya mwendazake? kopi and [pesti ya Sweden na ikamshinda, kama ulikuwa huelewi.

Sweden corona yote, hawajafunga chochote wala hawajaweka kikwazo aina yoyote ya corona. Unalielewa hilo?
 
NNT uliiona wapi kwengine duniani? Nchi gani duniani zaidi ya Tanzania imetangaza na kuweka mikakati ya kutajirisha vijana wake kwa makusudi kabisa na inafanya hivyo kwa vitendo siyo maneno.

Kwa uchache, vijana kwa malaki kutajirishwa kwa makusudi kabisa na serikali yao na wameshaanza, zaidi ya vijana 500 ndani ya muda mfupi wameshaanza kutajirishwa kwa makusdio kanisa, washindwe wenyewe tu.

Haijawahi kutokea duniani. Mpaka dunia imeyaona hayo ndani ya muda mfupi sana,, nchi zaidi ya 70 duniani zipo Tanzania tayari kujifunza wanawezawezaje Tanzania.

Unayajuwa hayo?
Endeleeni kukejeli namna hii tu lakini mjue kuna siku hata wale wanasiasa waliojilimbikizia mali, matajiri na viongozi wa dini mtaikimbia nchi. Mnafanya kejeli na umaskini siyo...
 
Endeleeni kukejeli namna hii tu lakini mjue kuna siku hata wale wanasiasa waliojilimbikizia mali, matajiri na viongozi wa dini mtaikimbia nchi. Mnafanya kejeli na umaskini siyo...
Kukejeli nini wewe? Unaifahamu BBT?

Kijana unatia huruma sana, kama hata mipango ya kukutajirisha inayofanywa na serikali yako huielewi. Ni wakuhurumiwa tu. Pole sana.

Tumia simu yako kwa faida, siyo kuingia mitandao ya jamii kubishana kijinga.
 
Mama Abdul nchi imemshinda. Viongozi wote wamegeuka wafanyabiashara na kila mmoja ana chimbo lake la kupiga fedha haramu.
 
Pamoja na kuwa na nia njema na kujitahidi kuna mengine yapo nje ya uwezo wake kama Bashe.

Korosho bwana yule aliyepeleka jeshi ndiye aliyeizika.

Pamba tunajua ni miaka yote imekuwa changamoto. Tutumie wingi wetu kuzalisha bidhaa zitokonazo na pamba na tuzitumie wenyewe.

Kuhusu tumbaku, sasa Bashe dollar atazitoa wapi ili wakulima walipwe. Bashe kwa hili anafanya juhudi kubwa sana kuwanasua wakulima.

Pamoja na yeye kuwa mzee wa janja janja, serikali imsaidie kupeleka fedha kadiri ya mpango wa bajeti.
 
Mama kafungua Nchi kwelikweli. Tatizo kafungulia na Majizi sasa.
 
Bashe ni miongoni mwa Mawaziri wanaofanya vizuri sana, isipokuwa kuna ugumu mkubwa kwa kiongozi bora ndani ya CCM kwa maana wengi wa viongozi ngazi za chama hawana ujuzi wa uongozi na elimu ya mambo, akili ndogo inapewa dhamana ya kuongoza akili kubwa, na pale ambapo akili ndogo imeshika Mpini ndo mambo yanaokuwa magumu zaidi, nilishangaa kijani mmoja Mwanza kweupe kabisa tena juu ya mimbali akitetea kijani yake kuhusu DPW akisema wapewe waarabu ili walete wanawake wazuri wawaoe, 'nikajisemea moyoni hajui ataolewa yeye.'
 
Hicho kitu alichokisema ni unafiki mtupu, ukiwa daktari ndio usifungue pharmacy?
Udaktari sio uongozi wa kisiasa hiyo ni proffession ,tofauti na cheo cha kisiasa ambacho mtu yupo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi ya kisheria au sera, na ni rahisi kubadilisha sera ili yeye afaidike
 
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amepatwa na nini? Mbona Bashe wa kabla ya kuteuliwa kuwa waziri alikuwa machachari sana kuliko huyu wa sasa?
Mazao yote makubwa chini yake yameanguka bei ,pamba, korosha hali ni mbaya.
kwenye tumbaku wakulima hawajalipwa hadi leo!!!kila siku ni ahadi na ngonjera zisizo isha kabisa.
Bashe wa leo yuko bize kutetea wafanyabiashara tu ambao ni matajiri tayari na hata asipowatetea hawawezi kufa na njaa, na kuacha wananchi masikini ambao usipowatetea wanatembea bila viatu.

Kitu ambacho hakijui Rais Samia au anakijua lakini ameamua kukaa kimya ni mawaziri wake kugeuka wafanyabiashara wakubwa sana. Ukiona mafuta yameadimika sababu kubwa ni kwamba viongozi wa hiyo wizara ndiyo wamiliki wa vituo vya mafuta kwa hiyo hata yakifichwa ili yapande bei hawaoni shida, pia ukiona mazao ya kilimo hayapandi bei ujue wanunuzi wakubwa wa hayo mazao ni haohao mawaziri wa rais Samia!.
Viongozi sehemu ambazo wao ni wauzaji bei zinapanda balaa eg mafuta, ila sehemu ambazo viongozi ni wanunuzi bei zinashuka kwa kasi au kudumaa palepale, eg korosho na pamba!!
Hakuna jipya chini ya CCM!! CCM ni ileile....
 
Mlikuwa mnaimba hapa kwenye jukwaa kuwa Samia kapandisha bei ya mazao mala mbili zaidi ya Magufuli, Maana Magufuli alikuwa amefunga nchi, Sasahivi Samia kaifungua mambo safi,kuleni matunda ya nchi kufunguliwa Maana miaka 6 nchi ilifungwa 😂😂😂
 
Mlikuwa mnaimba hapa kwenye jukwaa kuwa Samia kapandisha bei ya mazao mala mbili zaidi ya Magufuli, Maana Magufuli alikuwa amefunga nchi, Sasahivi Samia kaifungua mambo safi,kuleni matunda ya nchi kufunguliwa Maana miaka 6 nchi ilifungwa [emoji23][emoji23][emoji23]
Amefungua nchi na bei ndiyo zikafa kabisa
 
Kilimo ni kigumu cha mazao sana maana solo linaamuliwa na mapepari ambayo yanajali kupata supernormal profits.
Nguvu iwekwe kwenye mazoa tunawwza kuyatumia nchini
 
Nimemdharau Bashe kwenye suala la MBOLEA. Wakulima wengi walijiamdikisha kupata MBOLEA ya ruzuku toka mwaka Jana hadi Leo hakuna kitu. Msimu wa kilimo uliopita wengine walilazimika kununua MBOLEA hiyo hivyo ya ruzuku kwa sh 100,000/- kwa mfuko wa kg 50 badala sh 70,000/- toka kwa wakulima wenzao waliofanikiwa kujisajili. Huu ni upuuzi uliosababishwa na Bashe.
 
Back
Top Bottom