Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba si mbunifu

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Nakiri kama nchi hii msomi wa ngazi ya PhD anaweza kufikiri kama darasa la saba, ni jambo la kusikitisha sana.

Mimi nisingeshindwa kusema naogeza tozo kwenye miamala, natoza kodi ya Nyumba kwenye luku, naongeza bei ya mafuta. Je, ijahitaji PhD kufikiri vitu hivyo?

Je, nini kinafanyika kwa wenzetu mfano Uganda hadi inatokea wafanyabiashara wote wa kanda ya ziwa wanaenda kuhemea Bidhaa Uganda? Wakiingia uganda ni uchumi kiasi gani wanaacha huko? Mimi nikiona hayo ndipo ninaweka heshima kwa wasomi waliodababisha hiyo halo ikatokea na si tozo sijui ya baiskeli, pikipiki na bajaji kwa vile unaziona ni nyingi.

Tunahitaji waziri wa fedha mbunifu sana ili kuwapunguzia wananchi maumivu na kuwadidimiza kwenye umaskini.
 
Kumsikiliza mwigulu akiongea chochote nchi Hii imekua Ni KERO sana.
Huyu jamaa
Ana kauli za kikatili Sana
Ana kauli za kebehi, majivuno na kujiskia Sana.
Huyu jamaa anachochea sana chuki ya wananchi dhidi ya serikali yao
 
Waziri hapangi masuala ya kodi, Bunge linakaa na kujadili na kupitisha, kama mnachuki binafsi na Mwigulu muwe wazi, wakulaumiwa ni wabunge
 
Mwigulu yupo busy kutudadavulia kuhusu hii Tozo mbona kwenye mitandao kuna 18% ya VAT miaka nenda miaka rudi wanachukua wamepata shilingi ngapi na wamejenga nini anataka kuja na hoja ya zahanati na shule wakati kodi zingine tunalipa hizo hela zinafanya nini.
 
Hahaha, mna waziri kuanzia shahada ya kwanza mpaka shahada ya uzamivu kapata hapa hapa nyumbani, tena hiyo ya ya uzamivu kapata akiwa mwanasiasa mwenye ushawishi wakati huo. Hapo hamna exposure yoyote zaidi kujidai kuwatetea walalahoi huku wakiwang'ong'a kisogoni.
 
Kumsikiliza mwigulu akiongea chochote nchi Hii imekua Ni KERO sana.
Huyu jamaa
Ana kauli za kikatili Sana,
Ana kauli za kebehi, majivuno na kujiskia Sana.
Huyu jamaa anachochea sana chuki ya wananchi dhidi ya serikali yao

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
Yaani kiufupi jamaa ana tabia za kichawi. Inashangaza kuona mtu kama huyu eti anapewa Wizara nyeti! Ubunifu hana!! Zaidi tu ya kudesa mawazo ya Zungu na ya humu JF, na kuyachukua kama yalivyo! Pasipo hata kuyafanyia utafiti.

Mimi daima nitaendelea tu kumshangaa Bosi wake aliyemteua.
 
Naenda kusema kwa maa ma kuseema ,Naenda kusema kwa maa ma kuseema !!

wazir wake anatuteesa ,kutwaa kuucha ana-tuliimaaa
Kila kitu kwake peeesaaa,anakama kila konaa
katufuata wasaapuu ,wa Insta hawajapoona.
Naenda kusema kwa maa ma kuseema

Katuwinda tumo ndaanii, waziri wako nishi daa
Ubaya mwake rohonii ,katuona tunang'aa
karuka kazima taa,tukawasha vibatalii
kafukuwa upenunii ,balaa kwenye mafuutaa.
Naenda kusema kwa maa ma kuseema.

kama ni kooodi ulaayaaa waziri aljifahamu.
walipwa waimba kwaya,na wale wa vibaraza.
raia wasio kaazi nao hutiliwa chajii,wakasifu serikali.

Sasa avuka mipaka waziri wako jamaanii.
mtulize shetaniwe apate kuona mbaalii.
asingoje alaniwe akapata idhilali.
Raia tumasikini vipi tutoe shilingii

Naenda kusema kwa maa ma kuseema
 
Back
Top Bottom