Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, Aprili 7, 2025 ambapo ameongeza kuwa hafla hiyo inalenga kutambua na kuenzi mchango wa Waandishi Bunifu katika kukuza lugha, utamaduni, na fikra za maendeleo nchini.
Tuzo hiyo, iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ni ishara ya kumuenzi kutokana na mchango wake mkubwa katika Uandishi Bunifu.
Prof. Mkenda amesema kuwa maandalizi ya hafla hiyo yamekamilika na kwamba ni heshima kubwa kwa Sekta ya Elimu kuwa na ugeni huo wa juu unaoonyesha namna ambavyo serikali inatambua mchango wa uandishi bunifu katika kukuza lugha ya Kiswahili, maarifa, na utamaduni wa taifa.
“Tuzo hii ni heshima kwa Mwalimu Nyerere lakini pia ni jukwaa mahsusi kwa waandishi chipukizi na wakongwe kuonyesha umahiri wao katika nyanja mbalimbali za uandishi kama vile riwaya, ushairi, hadithi za watoto na tamthiliya,” amesema Prof. Mkenda.
Profesa Mlama alitangaza majina na kazi zilizokidhi vigezo, mbele ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda jijini Dar es Salaam leo Aprili 7, 2025 wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Ameeleza tuzo hizo zimegawanyika kwenye nyanja nne ambazo ni ushairi, riwaya, hadithi za watoto na tamthiliya.
“Kama tunavyofahamu, tuzo hii ilianzishwa na serikali chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na inaratibiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania… huu ni mwaka wa tatu wa utoaji wa Tuzo hii.
Pia soma ~ Hafla ya Utoaji Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Aprili 13, 2025