Waziri wa Ardhi aagiza kuondolewa kwa Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,612
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ameagiza kuondolewa kwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa wizara hiyo, Venance Mwolo akisema hatoshi katika majukumu hayo.

Waziri Mabula ametoa maelekezo hayo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Allan Kijazi leo Jumanne, Septemba 6, 2022 mbele ya waandishi wa habari.

"Mkurugenzi wa Tehama simtaki katika wizara ya ardhi, ameshindwa kutekeleza majukumu yake. Katibu Mkuu (Dk Allan Kijazi), wasiliana na utumishi wafanye utaratibu wa kuleta mtu mwingine," amesema.

Ametaka mkurugenzi atakeyeletwa kuifanya kazi hiyo ahakikishe anaendana na kasi ya Serikali katika matumizi ya Tehama.

Chanzo: Mwananchi
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ameagiza kuondolewa kwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa wizara hiyo, Venance Mwolo akisema hatoshi katika majukumu hayo...
Habari nusu, ameshindwa nini?
 
Waziri angetuuma sikio kidogo tujue walau kwa uchache kwa nini hatoshi?

Hapa ndio ninapoona pengo la Hayati lisilozibika. Hayati alikuwa akitaka kukutumbua alikuwa anakufanyia physiological torture mbele ya Umma alikuwa hataki maneno yasemwe pembeni Rais kaonea mtu.

Mbele ya Umma unaitwa ujieleze unapigwa maswali heavy ukiteteleka umma wote wanaona kweli unastahili kufukuzwa na huonewi hata huruma ,ogopa Sana kuhukumiwa na Umma
 
Back
Top Bottom