Nobunaga
JF-Expert Member
- Mar 22, 2019
- 1,169
- 4,986
Kwanza nakushukuru Mh. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwa kulivalia njuga hili jambo la mwanafunzi Lightness Shirima (22) ambaye baba yake Priscus Shirima alifariki Hospitali ya Mloganzila kisha wakakishikilia kitambulisho chake cha NIDA mpaka hapo atakapomaliza deni lake la milioni 9.
Labda kitu ambacho hujui ni kwamba ambao vitambulisho vyetu vimeshikiliwa pale tuko mamia kwa mamia, yani ukienda ile ofisi yao ya uhasibu utajihakikishia mwenyewe. Huu utaratibu unawaumiza wengine ambao wanahitaji kuvitumia vitambulisho vyao kwenye mambo mbalimbali ikiwemo kutafuta ajira, maombi ya kwenda masomoni nk.
Tunashauri uongozi wa Mloganzila utafute utaratibu mwingine ikiwamo wenyeviti wa mitaa na vijiji wahusishwe kwenye kuwatambua wadaiwa na wawe kama wadhamini wao ila sio kushikilia NIDA za watu kisha kupelekea kuwakwamisha kwenye mambo yao mengine ya kimaendeleo.
Hivyo Mh. Waziri tunaomba na wengine ambao vitambulisho vyao vimeshikiliwa pale Mloganzila hospitali warudishiwe vitambulisho vyao kisha utaratibu mwingine mzuri wa wadaiwa kulipa deni uandaliwe.