Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,086
- 6,568
Inahitajika elimu kubwa na hamasa kwa wananchi kuona umuhimu wake. Kwa serikali hii, usishangae kusikia wasio na bima ya afya wawekwe ndani.Bima ya afya kwa wote ni ndoto. Wanasema... kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
Juu ukilinganisha na nini na wapi? Unadhani gharama zinatoka hewani?Gharama za huduma za afya zipo juu sana
Nadhani suala hapa sio elimu, zaidi ni uwezo wa hao wananchi wataweza kumudu gharama za bima ya Afya na matibabu kwa ujumla? au serikali itaweka mkono wake pale ambapo mwananchi (mgonjwa) nguvu zake zitakapoishia?Inahitajika elimu kubwa na hamasa kwa wananchi kuona umuhimu wake. Kwa serikali hii, usishangae kusikia wasio na bima ya afya wawekwe ndani.
Watanzania tunaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Hiyo basic bima ya afya imeondoa magonjwa sugu. Kama una kisukari, magonjwa ya moyo au saratani inabidi uongeze malipo.Nadhani suala hapa sio elimu, zaidi ni uwezo wa hao wananchi wataweza kumudu gharama za bima ya Afya na matibabu kwa ujumla? au serikali itaweka mkono wake pale ambapo mwananchi (mgonnwa) nguvu zake zitakapoishia?
Kama ni hivyo serikali kuanzia mwaka ujao wa fedha watenge fungu kwenye bajeti ya wizara ya Afya.
Kwani bima ya afya mpaka uwe na ajira?Bima ya Afya itatolewa kwa mtindo upi kwenye taifa ambalo ma jobless ni wengi zaidi ya wenye ajira?
Zaidi wataweka kiwango cha chini mwanachama kulipia kwa mwaka, lakini mwanachama huyo akiugua ugonjwa mkubwa wakuhitaji gharama kubwa hiyo bima haitamsaidia chochote, ataambiwa tena alipie, matokeo yake tutarudi kule kule.
We ni mtanzania wa wapi? Hujui kumuona Dk ni 1000-5000. Bado vipimo na gharama za dawa,unataka alinganishe na wapi?Juu ukilinganisha na nini na wapi? Unadhani gharama zinatoka hewani?
Kwanini kumuona Dr kwenye hospitali za serikali ulipie wakati mshahara wake unalipwa na mlipa kodi, can you justify that cost?We ni mtanzania wa wapi? Hujui kumuona Dk ni 1000-5000. Bado vipimo na gharama za dawa,unataka alinganishe na wapi?
Unaniuliza mimi?Kwanini kumuona Dr kwenye hospitali za serikali ulipie, can you justify that cost?
Mtu mwenye ajira anaweza kulipia kiwango cha juu kitachomuwezesha kutibiwa kwa uhakika magonjwa yote, wewe usie na ajira au machinga unataka ulipie elfu ishirini kwa mwaka halafu utibiwe figo kwa hiyo pesa?Kwani bima ya afya mpaka uwe na ajira?
Leo umedonoa point muhimu.Kile kitambulisho cha machinga kingejumlisha na bima ya afya ingeleta maana.
Kiwango kipi cha juu ambacho sisi wasio na ajira hatuwezi kukimudu? Bima ni suala la kuchangiana,wasiougua wanawachangia wanaougua hivyo hata kama ni 30000 lakini tuwe na uhakika wa tiba. Sio unasubiri kutibiwa kisa huna senti.Mtu mwenye ajira anaweza kulipia kiwango cha juu kitachomuwezesha kutibiwa kwa uhakika magonjwa yote, wewe usie na ajira unataka ulipie elfu ishirini kwa mwaka halafu utibiwe figo kwa hiyo pesa?
Serikali lazima iweke mkono hapo.