Waziri wa Afya ni bora ungeanza na mchakato wa Bima ya Afya kwa kila Mtanzania kuliko kutoa agizo kama hili

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,067
2,000
Wana JF poleni na pilika pilika za sikukuu.

Kama kichwa cha uzi kinavyojitanabaisha niseme kuwa agizo la waziri wa afya sio zuri kwa mustakabari wa watanzania.

Watanzania wengi tunaishi maisha ya kubahatisha,wengi tunatafuta chakula. Habari ya matibabu huwa ni dharula ndio maana tukiugua au kupata mgonjwa huwa tupata tabu sana.

Kitendo cha waziri mwenye dhamana ya afya zetu kuagiza hospital ziwe zinatukaba tuwe tunalipa gharama ya matibabu kabla ya bahati mbaya ya kufariki haijatokea ni habari mbaya.

Chukulia mkulima wa kijijini ambae amegongwa nyoka na kukimbizwa hospital atapata wapi pesa za kulipia haraka ili atibiwe na asifariki? Mama wa kijijini ambae amepatwa malalaria ghafla ataweza kumudu haya aliyoagiza waziri wa afya?

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu,hoja ya bima ya afya kwa kila mtanzania iliibuka na kuwa gumzo. Uzuri rais Magufuli kwa kujibu mapigo ya wapinzani alisema suala la bima ya afya lipo kwenye ilani ya Ccm. Na itakuwa bima ya afya kwa watanzania wote.

Waziri wa afya alitakiwa kwa nia njema ya watanzania maskini ambao anajua ndio huwa wanakwama kupata maiti za wapendwa wao ahakikishe bima ya afya kwa kila mtanzania inapatikana haraka ili tusije kupoteza maisha kwa kukosa matibabu maana kiuhalisia ni ngumu kuwa na cash wakati wote.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,866
2,000
Bima ya Afya itatolewa kwa mtindo upi kwenye taifa ambalo ma jobless ni wengi zaidi ya wenye ajira?

Zaidi wataweka kiwango cha chini mwanachama kulipia kwa mwaka, lakini mwanachama huyo akiugua ugonjwa mkubwa wakuhitaji gharama kubwa hiyo bima haitamsaidia chochote, ataambiwa tena alipie, matokeo yake tutarudi kule kule.

Hapa serikali ni vyema ikatenga fungu kwa ajili ya kuwasaidia wale wataokwama kulipia gharama zote za matibabu yao.
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,442
2,000
The whole health system needs overhauling you can’t have services which by law are supposed to be non profitable and yet the current modus operandi is partly universal and partly private funded; resulting discrimination in access.

Gwajima needs to sort that mess, ili wananchi wachangie appropriately based on the government health objectives kwa watanzania kama ni health insurance or paying for services at point of entry whichever contribution approach is pursued; profit making is not the motive nor depriviation of access to health services for low income Tanzanians that is according to Tanzania’s constitution.

Lengo la tozo ni ku cover costs deficit ilhali lifanyike kila linalowezekana kila mtu apate huduma sawa.

Sorting out that mess requires kwanza kumuelewesha raisi ‘cost benefit analysis’ ya malengo ya afya ili apate backup na kuchukua hatua sahihi, vinginevyo atapata resistance kubwa na majungu kutoka huko wizarani not because she is wrong ila kuna wapuuzi wengi waliokuwa wakifanya haya maamuzi who were not qualified to make those decision na culture yetu ya wasomi kutopenda kupingwa ita mletea matatizo.

The woman got to understand the risks which comes with her decisions she might be right, but also there is the need to weigh-in Tanzania culture context on government working (as a management expert she should know that) and learn how to mitigate those aspects of change management.

Haya mambo ya taasisi za serikali kujiamulia JK aliyachekea sana na taasisi nyingi zilipoteza operation model zake in-line na matakwa ya katiba, it’s time to revert that nonsense.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,866
2,000
Inahitajika elimu kubwa na hamasa kwa wananchi kuona umuhimu wake. Kwa serikali hii, usishangae kusikia wasio na bima ya afya wawekwe ndani.
Nadhani suala hapa sio elimu, zaidi ni uwezo wa hao wananchi wataweza kumudu gharama za bima ya Afya na matibabu kwa ujumla? au serikali itaweka mkono wake pale ambapo mwananchi (mgonjwa) nguvu zake zitakapoishia?

Kama ni hivyo, serikali kuanzia mwaka ujao wa fedha watenge fungu kwenye bajeti ya wizara ya Afya, wajaribu kama walivyofanya kwenye elimu bure, japo nayo inayumba lakini atleast.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
48,987
2,000
Nadhani suala hapa sio elimu, zaidi ni uwezo wa hao wananchi wataweza kumudu gharama za bima ya Afya na matibabu kwa ujumla? au serikali itaweka mkono wake pale ambapo mwananchi (mgonnwa) nguvu zake zitakapoishia?

Kama ni hivyo serikali kuanzia mwaka ujao wa fedha watenge fungu kwenye bajeti ya wizara ya Afya.
Watanzania tunaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Hiyo basic bima ya afya imeondoa magonjwa sugu. Kama una kisukari, magonjwa ya moyo au saratani inabidi uongeze malipo.
 

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,067
2,000
Bima ya Afya itatolewa kwa mtindo upi kwenye taifa ambalo ma jobless ni wengi zaidi ya wenye ajira?

Zaidi wataweka kiwango cha chini mwanachama kulipia kwa mwaka, lakini mwanachama huyo akiugua ugonjwa mkubwa wakuhitaji gharama kubwa hiyo bima haitamsaidia chochote, ataambiwa tena alipie, matokeo yake tutarudi kule kule.
Kwani bima ya afya mpaka uwe na ajira?
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,442
2,000
We ni mtanzania wa wapi? Hujui kumuona Dk ni 1000-5000. Bado vipimo na gharama za dawa,unataka alinganishe na wapi?
Kwanini kumuona Dr kwenye hospitali za serikali ulipie wakati mshahara wake unalipwa na mlipa kodi, can you justify that cost?

Hiyo wizara inahitaji sorting out mambo yalikuwa yanafanyika ovyo mno. Taasisi za afya za serikali sio profit seeking organisation na wala mapato yao sio sehemu ya government revenue they are meant to provide inclusive services to all Tanzanians by law.

Magufuli amuandae Makamba ili kumjengea discipline za kuacha mambo ya urafiki na kuwa firm kwenye kazi vinginevyo nchi aitoenda.

Why him pamoja na upuuzi wake Makamba ni kijana pekee anae pokea criticism na kuzifanyia kazi pale anapoona merit za hoja na kukubali approach zake zina matatizo (you can see anakubali hajui kila kitu).

However ata pale anapokubali kubadili mbinu za kufanya mambo lengo halisi la kuchukua hatua zake lazima lifikiwe it shows he is stern on his decision making kama Magu anahitaji kupikwa zaidi tu, aelewe some decision are wrong all together kwa maslahi ya nchi you got to learn to compromise or speed up the process kama alivyokuwa anaachia upuuzi wa NEMC ukwamishe pace za maendeleo.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,866
2,000
Kwani bima ya afya mpaka uwe na ajira?
Mtu mwenye ajira anaweza kulipia kiwango cha juu kitachomuwezesha kutibiwa kwa uhakika magonjwa yote, wewe usie na ajira au machinga unataka ulipie elfu ishirini kwa mwaka halafu utibiwe figo kwa hiyo pesa?

Serikali lazima iweke mkono hapo.
 

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,067
2,000
Mtu mwenye ajira anaweza kulipia kiwango cha juu kitachomuwezesha kutibiwa kwa uhakika magonjwa yote, wewe usie na ajira unataka ulipie elfu ishirini kwa mwaka halafu utibiwe figo kwa hiyo pesa?

Serikali lazima iweke mkono hapo.
Kiwango kipi cha juu ambacho sisi wasio na ajira hatuwezi kukimudu? Bima ni suala la kuchangiana,wasiougua wanawachangia wanaougua hivyo hata kama ni 30000 lakini tuwe na uhakika wa tiba. Sio unasubiri kutibiwa kisa huna senti.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom