Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,086
- 6,568
Wana JF poleni na pilika pilika za sikukuu.
Kama kichwa cha uzi kinavyojitanabaisha niseme kuwa agizo la waziri wa afya sio zuri kwa mustakabari wa watanzania.
Watanzania wengi tunaishi maisha ya kubahatisha,wengi tunatafuta chakula. Habari ya matibabu huwa ni dharula ndio maana tukiugua au kupata mgonjwa huwa tupata tabu sana.
Kitendo cha waziri mwenye dhamana ya afya zetu kuagiza hospital ziwe zinatukaba tuwe tunalipa gharama ya matibabu kabla ya bahati mbaya ya kufariki haijatokea ni habari mbaya.
Chukulia mkulima wa kijijini ambae amegongwa nyoka na kukimbizwa hospital atapata wapi pesa za kulipia haraka ili atibiwe na asifariki? Mama wa kijijini ambae amepatwa malalaria ghafla ataweza kumudu haya aliyoagiza waziri wa afya?
Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu,hoja ya bima ya afya kwa kila mtanzania iliibuka na kuwa gumzo. Uzuri rais Magufuli kwa kujibu mapigo ya wapinzani alisema suala la bima ya afya lipo kwenye ilani ya Ccm. Na itakuwa bima ya afya kwa watanzania wote.
Waziri wa afya alitakiwa kwa nia njema ya watanzania maskini ambao anajua ndio huwa wanakwama kupata maiti za wapendwa wao ahakikishe bima ya afya kwa kila mtanzania inapatikana haraka ili tusije kupoteza maisha kwa kukosa matibabu maana kiuhalisia ni ngumu kuwa na cash wakati wote.