#COVID19 Waziri Ummy Mwalimu: Watu 3,147 walazwa kwa UVIKO-19 huku 76 wakifariki

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
1643211830772.png

Serikali imesema watu 3,147 walilazwa hospitalini kutokana na Uviko-19 kati ya Septemba 2021 mpaka Januari 23, 2022 ambapo kati yao 2990 sawa na asilimia 95 walikuwa hawajachanja.

Pia, imesema kuwa mpaka sasa ni watu 1,922,019 waliochanja sawa na asilimia 3.3 ya Watanzania waliolengwa.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Januari 26, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu baada ya kupokea shehena ya chanjo 800,000 za Sinopharm ambazo ni sawa na dozi 400,000 kutoka Serikali ya watu wa China.

“Wagonjwa waliokuwa mahututi katika vyumba vya uangalizi maalumu kwa siku ya Januari 23 mwaka huu ICU walikuwa 31 kati yao 30 walikuwa hawajachanjwa.

Vifo vilivyotokea vilikua 76 kati ya hivyo vifo 73 viliwahusisha wagonjwa ambao hawakuchanja,” amesema Waziri Ummy.

Amewataka Watanzania kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya kupima kwa kuwa si kila homa au mafua ni Uviko-19.

“Una homa kapime watu sasa hivi wanakunywa Azuma na dawa zingine za antibaotiki, si kila homa ni corona tuache kujitibu kapime upate matibabu sahihi, tunatengeneza usugu wa dawa baadaye tutakua tunatibu watu hawaponi,” amesema.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dk Beatrice Mutayoba amesema chanjo hizo zina uwezo wa kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.

“JJ inakaa miezi mitano tunafanya utaratibu wa kuzigawa ndani ya muda mfupi tunakuwa tumezimaliza, chanjo za Sinopharm ni miaka miwili na Pfizer zinakaa miezi 8,” amesema Dk Mutayoba.

Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian amesema mpaka sasa zaidi ya asilimia 80 ya watu wa China wamechanja.

Mwananchi
 
Wakati wa kuongea walikuwa Kimya kwamba hili jambo halipo sasa hivi linavumilika na tunaswampa nalo ndio wanaleta habari ya kutujuza...

Kweli wanakwenda Vice Versa...
 
apa yabidi tuombe fungu jingine tulitumie kujenga kituo cha afya kila kataa
 
Serikali imesema watu 3,147 walilazwa hospitalini kutokana na Uviko-19 kati ya Septemba 2021 mpaka Januari 23, 2022 ambapo kati yao 2990 sawa na asilimia 95 walikuwa hawajachanja.

Pia, imesema kuwa mpaka sasa ni watu 1,922,019 waliochanja sawa na asilimia 3.3 ya Watanzania waliolengwa.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Januari 26, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu baada ya kupokea shehena ya chanjo 800,000 za Sinopharm ambazo ni sawa na dozi 400,000 kutoka Serikali ya watu wa China.

“Wagonjwa waliokuwa mahututi katika vyumba vya uangalizi maalumu kwa siku ya Januari 23 mwaka huu ICU walikuwa 31 kati yao 30 walikuwa hawajachanjwa.

Vifo vilivyotokea vilikua 76 kati ya hivyo vifo 73 viliwahusisha wagonjwa ambao hawakuchanja,” amesema Waziri Ummy.

Amewataka Watanzania kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya kupima kwa kuwa si kila homa au mafua ni Uviko-19.

“Una homa kapime watu sasa hivi wanakunywa Azuma na dawa zingine za antibaotiki, si kila homa ni corona tuache kujitibu kapime upate matibabu sahihi, tunatengeneza usugu wa dawa baadaye tutakua tunatibu watu hawaponi,” amesema.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dk Beatrice Mutayoba amesema chanjo hizo zina uwezo wa kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.

“JJ inakaa miezi mitano tunafanya utaratibu wa kuzigawa ndani ya muda mfupi tunakuwa tumezimaliza, chanjo za Sinopharm ni miaka miwili na Pfizer zinakaa miezi 8,” amesema Dk Mutayoba.

Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian amesema mpaka sasa zaidi ya asilimia 80 ya watu wa China wamechanja.

Mwananchi
Machanjo hayo nahofia yalishapitwa na wakati expired mimi siwezi kusogelea kabisa! Chanjo tokea September zipo mpaka leo! Ndo muamze kutishia watu wakachanje! Mlishafeli pakubwa sana!
 
Serikali imesema watu 3,147 walilazwa hospitalini kutokana na Uviko-19 kati ya Septemba 2021 mpaka Januari 23, 2022 ambapo kati yao 2990 sawa na asilimia 95 walikuwa hawajachanja.

Pia, imesema kuwa mpaka sasa ni watu 1,922,019 waliochanja sawa na asilimia 3.3 ya Watanzania waliolengwa.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Januari 26, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu baada ya kupokea shehena ya chanjo 800,000 za Sinopharm ambazo ni sawa na dozi 400,000 kutoka Serikali ya watu wa China.

“Wagonjwa waliokuwa mahututi katika vyumba vya uangalizi maalumu kwa siku ya Januari 23 mwaka huu ICU walikuwa 31 kati yao 30 walikuwa hawajachanjwa.

Vifo vilivyotokea vilikua 76 kati ya hivyo vifo 73 viliwahusisha wagonjwa ambao hawakuchanja,” amesema Waziri Ummy.

Amewataka Watanzania kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya kupima kwa kuwa si kila homa au mafua ni Uviko-19.

“Una homa kapime watu sasa hivi wanakunywa Azuma na dawa zingine za antibaotiki, si kila homa ni corona tuache kujitibu kapime upate matibabu sahihi, tunatengeneza usugu wa dawa baadaye tutakua tunatibu watu hawaponi,” amesema.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dk Beatrice Mutayoba amesema chanjo hizo zina uwezo wa kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.

“JJ inakaa miezi mitano tunafanya utaratibu wa kuzigawa ndani ya muda mfupi tunakuwa tumezimaliza, chanjo za Sinopharm ni miaka miwili na Pfizer zinakaa miezi 8,” amesema Dk Mutayoba.

Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian amesema mpaka sasa zaidi ya asilimia 80 ya watu wa China wamechanja.

Mwananchi
Hii ni kutaka watu waone wasiochanjwa ndo walioathirika zaidi mpk Vifo!

Ila huku mtaani naona hali ni tofauti....
 
Hawa wanataka kuomba mkopo mwingine kwa wazungu tu,tangia waseme Covid hipo Nchini sijawai kutana na hata mgonjwa wa hiyo kitu,sijui wanatokea Wapi, maana huko mtaani covid tunaisikia kwenye tv na redioni 🤣🤣🤣
 
Mimi na sema ukweli wangu akuna covid duniani hizi ni propaganda tu na kuogopesha watu akuna ukweli wowote wanatafuta njia ya kuweka chanjo iwe lazima

Kama ni kweli waonyeshe watu izo hospitali za watu wa covid tukawasalimie

Na uyu mwalimu ommy Huyu ndo mjinga kabisa Huyu amesha pewa pesa tayari
 
Ndugu zangu naomba tuwe makini
Na vitu tunavyo ambiwa lakini havionekani, tumedanganywa muda mrefu sana
.Pia naomba tusitiane hofu na stress bure
 
Very awkward!

Katika nchi ambayo almost everyone hajachanja unawezaje kuweka msisitizo eti "Vifo vilivyotokea vilikua 76 kati ya hivyo vifo 73 viliwahusisha wagonjwa ambao hawakuchanja"?

If anything huo msisitizo unaonyesha jinsi hizo chanjo za corona zilivyo useless: kumbe kati ya watu 76 waliokufa kuna watu watatu waliochanjwa still wakaambukizwa na kufa?
 
Back
Top Bottom