Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema uamuzi wa kuzima mtandao wa internet ni chaguo la mwisho kabisa pale ambapo hali ya kiusalama inakwa mbaya ambapo amesema hadi kufikia sasa hali ya Tanzania bado ipo shwari na hakuna tishio la kuwafanya TCRA wazime internet kesho December 09,2025.
Akiongea leo December 08,2025, Simbachawene amesema ““Kuhusu kuzimwa mtandao kwasababu nyenzo kubwa inayotumika na hawa Wanaharakati wa mitandaoni ni kutumia taarifa za taharuki, zikitoka wengine wanapata shida sana wakisikia, wengine wanazifurahia, kwahiyo mpaka sasa hatujaona tishio lolote la kufikia kwamba mtandao umekuwa tatizo”
“Tufahamu mtandao huu ndio unatumika kutoa huduma za kijamii nyingi, mabenki, usafiri na mambo mengine mengi yanatumia mtandao wa internet, kwahiyo kuzima internet ni chaguo la mwisho sana pale ambapo hali ikiwa mbaya ingawa hii inahusika na Sekta nyingine ya wenzetu wanaweza kusema lakini Mimi naona kwakweli mpaka sasa hivi kama ndio tunaoangalia usalama wa nchi na Watu tunaona hali ni shwari hakuna tishio kwamba wenzetu wa TCRA watazima mtandao”
Chanzo: Millard ayo