Waziri Simbachawene acha maigizo, mpe IGP muongozo wa COVID-19 na dhana ya Mikusanyiko

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
PICHA: Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, akisonga ugali wa wafungwa katika Gereza la Isupilo, Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa, alipolitembelea gereza hilo katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa taasisi zake mkoani humo.

Mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani aache hizi Comedy, Ni wakati sasa wa kutoa Muongozo wa Wizara ya Mambo ya ndani kuhusu Covid 19. Amemsikia waziri wa afya akilalamika kuwa hapewi ushirikiano. Kiuhalisia inaoneka Polisi ndo wana Mamlaka makubwa ya kuzuia na kuruhusu mikusanyiko. Kisheria si hivyo bali ndo mazoea yaliyopo.

Ni wakati sasa wa Simbachawene kuwakaripia watendaji wakuu wa jeshi hili na kuwapa Muongozo wa pamoja kitaifa si kila mmoja kusema lake.

Huu si wakati wa kupiga picha na kusonga Ugali wakati unaona Mikanganyiko nchi Nzima kuhusu Mikusanyiko ya Lazima VS Isiyo ya Lazima

E6z2C3NXMAI8HGn.jpg
 
Back
Top Bottom