Waziri Simbachawene apendekeza Watumishi wa Umma wasiingie ofisini na simu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,840
Hili pendekezo ni kiki, kwasababu binafsi sijawahi enda ofisi ya umma nikaacha kuhudumiwa eti mtu anachati.

===

1680680798419.png


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameeleza dhamira yake ya kushirikiana na watumishi wa ofisi yake katika kutekeleza jukumu la kuwasimamia watumishi wa umma nchini kutumia vizuri saa za kazi kuwahudumia wananchi badala ya kufanya mambo ambayo yanakwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Mhe. Simbachawene ameweka wazi dhamira hiyo ya kuwasimamia watumishi wa umma kutekeleza wajibu wao kikamilifu pindi alipowasili ofisini kwake na kuzungumza na watumishi wa ofisi yake waliompokea mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Aprili, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini.

Mhe. Simbachawene amesema, rasilimaliwatu ni muhimu sana katika maendeleo ya taifa lolote, hivyo ni lazima ofisi yake ihakikishe watumishi wa umma wanafanya kazi kwa mujibu wa Kanuni, Sheria, Taratibu, Miongozo na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo sheria mama ya nchi.

Mhe. Simbachawene ameeleza kuwa, wateja wanaofuata huduma katika taasisi za umma wamekuwa wakilalamika kutopatiwa huduma nzuri na kwa wakati, na kuongeza kuwa, baadhi ya watumishi wa umma wamekuwa wakifanya shughuli zao binafsi mahala pa kazi wakati wananchi wakisubiria kupatiwa huduma.

“Muda ambao mtumishi wa umma anatakiwa kufanya kazi ni saa nane, lakini utakuta mtumishi akiingia kazini anakuwa na pilika nyingine ambazo si za kazi anayopaswa kuifanya, akitoa mfano wa Muuguzi au Mwalimu anaposhindwa kuwajibika, madhara yake ni makubwa na taifa linapata hasara kubwa kwasababu rasilimaliwatu haitumiki ipasavyo,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.

Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, mtumishi anaingia kazini na simu ambayo ina makundi mengi, akianza kuwasiliana na makundi matatu tu saa moja ya kazi imeondoka na kwa kuwa ana makundi ya majirani, vikoba na mengineyo hivyo akiendelea kushiriki kinachojadiliwa unakuta matumizi ya simu yanachukua muda mwingi wa kazi

Utumishi
 
Hili pendekezo ni kiki Kwa sababu binafsi sijawahi enda ofisi ya umma nikaacha kuhudumiwa eti mtu anachati.

Matumia muda mwingi wa utumishi kwa mambo yenu binafsi ilhali mnalipwa mishahara kwa kodi zetu!
Mmekopa na kujenga majumba yenu kwa kodi zetu!

Mmekopa na kununua magari kwa kigezo cha kuwahi makazini kumbe ni uongo,ni usafiri wa kuendea kwenye matanuzi yenu zaidi!

Acheni dharau zenu enyi watumishi wa Umma nchini Tanzania
 
Simu ni sehemu ya kisaidizi cha mtumishi, waziri apambane na matatizo makubwa ya kiutumishi kama uchelewashaji wa mishahara, madaraja, uonevu wa kingono, etc etc, mimi mwenyewe ninashuhudia sana customs officials wetu wakitumia simu kupata informations nyingi za product's zinazoingia nchini, aachane na Kiki mfu
 
Matumia muda mwingi wa utumishi kwa mambo yenu binafsi ilhali mnalipwa mishahara kwa kodi zetu!
Mmekopa na kujenga majumba yenu kwa kodi zetu!

Mmekopa na kununua magari kwa kigezo cha kuwahi makazini kumbe ni uongo,ni usafiri wa kuendea kwenye matanuzi yenu zaidi!

Acheni dharau zenu enyi watumishi wa Umma nchini Tanzania
Huu ni uongo
 
Simu ni sehemu ya kisaidizi cha mtumishi, waziri apambane na matatizo makubwa ya kiutumishi kama uchelewashaji wa mishahara, madaraja, uonevu wa kingono, etc etc, mimi mwenyewe ninashuhudia sana customs officials wetu wakitumia simu kupata informations nyingi za product's zinazoingia nchini, aachane na Kiki mfu
Amekosa ubunifu,badala azungumzie upigaji anahangaika na vitu visivyowezekana.

Hii ni sawa na Ile ya Mwigulu kwamba Watumishi wa Umma wawe na magari binafsi.
 
Hili pendekezo ni kiki Kwa sababu binafsi sijawahi enda ofisi ya umma nikaacha kuhudumiwa eti mtu anachati.


Naunga mkono hoja 100 % watumie zile simu za ofisini ttcl landline phone ☎️ na ofisi zote ziwekewe cctv camera ili kumonitor muda wa kazi unatumiwaje kwenye ofisi za umma !! Maendeleo hayaji bila kujinyima yale tuyapendayo sana !! Kila la heri hon Simbachawene huwa nakuaminia sana sometimes !!
 
akitoa mfano wa Muuguzi au Mwalimu anaposhindwa kuwajibika, madhara yake ni makubwa na taifa linapata hasara
Kwani watumishi wa kada nyingine, taifa halipati hasara?
Nchii hii viongozi wengi wanapenda kuongelea watumishi wa kada za chini na hapo amesahau tu kusema polisi.

Wao huko juu ndio kuna mambo ya ajabu, wanatunga sera haziendani na uhalisia wa watanzania
 
Huyu niliamini ana tuakili, kumbe nae kala uji wa mgongwa.

Hakuna siku nipo class nasolve for x nikawa nachati.

Huyu waziri ni mkale, kuna app kibao za kuongeza ufanisi.

Kata simu niko site!

NB. IDARA YA USALAMA WA TAIFA MUONDOENI HUYO SIMBACHAWENE KWENYE WARITHI WATARAJIWA WA MAMA. AMEBNDA KUPANDISHA MABEGA MAPEMA ASIJE AKATULIMISHIA MENO TENA
 
Back
Top Bottom