Waziri Ngeleja: Serikali imeridhia kuilipa DOWANS Bilioni 95

Waziri Ngeleja: Serikali imeridhia kuilipa DOWANS Bilioni 95

Canada, India, Singapore, Oman, Kenya....,.does this make any sense? how come watu kutoka nchi tano tofauti wakawa na something in common in Costa rica, or Tanzania for that matter. Was it because someone in Tanzania just used their names and their nationalities? Is it kampuni ya kigeni au ni Dowans Tanzania, what makes it Dowans Tanzania wakati hakuna hata mtanzania mmoja, na haina ofisi Tanzania, nani aliyeipa hiyo tenda?

So many dots to connect, the picture will be very clear.

Kaka/Dada, na mie najiuliza maswali hayahaya, sipati jibu! Halafu sheria inasema kampuni ya kigeni lazima iwe na director atleast mmoja (kama sikosei) from Tz, mbona hajatajwa!?.
 
Ni ujinga ujinga kila mahali,uozo tu kila unapopita,watu wamekosa huruma kwa masikini wa kitanzania na hawana uzalendo kabisa,
mengi sasa yataibuka,na sasa watanzania wameanza kuelewa kwanini baraza jipya la mawziri kuna waliorudishwa kwenye nafasi zao za awali japo walivurunda ktk serikali iliyopita,
mmoja wa hao mawaziri ni ngeleja,tunaye pia mkulo na huyu mama kilaza hawa ghasia,hakika dr slaa hakukosea kusema dowans ni ya kikwete
 
Hawa ghasia shem, ujinga ni kwamba mfumo wa jamaa wa kampeni unaangalia uwezo wa kifedha wa kuwekwa ikulu wakati in 2005 alikua na uwezo mkubwa sana wa kushinda bila kuwatumia mafirauni lakini kwa kupenda quantity rather than quality namaanisha kupenda kuonekana amechagulika kwa kura nyingi badala ya zimepatikana vipi akatumia watu ambao sasa ndio matapishi. ukweli ni kuwa kwakuwa JK huwa anawadharau wataalamu na kusikiliza wanafiki wanaojidai washirika, sasa hana pa kugeukia.
 
pole sana kaka tutaendelea kuwajua kwa majina tu hakuna cha kuwafanya, kama sala nyingi tumeomba lakini wapi , ni juzi RA amerudi toka majuu kuwaleta wengine wa kuchota, eti wanaitwa wawekezaji, ao sio wawekezaji bali watwaaji wa maliasili yetu
 
Kwa kuongezea,Rostam Azim na Kampuni yake ya Caspian walipata hisa asilimia 35 Vodacom.Hivyo Rostam na Ngeleja ni maswahiba wa siku nyingi.Mswahili mwingine aliyekuwa na hisa na Peter Noni kupitia kampuni yake ya Planetel.Bw Noni ni MD wa benki ya TIB kwa sasa.So, JK hana ubavu wa kumtema Ngeleja kutoka Wizara ya Nishati.Yupo pale kulipa fadhila kwa waliomsaidia JK kwenye kampeni kama vile Kampuni ya kitapeli ya mafuta ya Glencore iliyowaliza Wakenya,Namibia na Msumbiji. Kama Ngeleja anaona ni uongo na abishe.

Mdau
 
Hii ndio Tanzania Rev Kishoka italiwa na wenye meno wengine tunabakia kutizama tu. Maana hata vya kuelezea sina zaidi ya kusikitika tu ila nawakumbushia viongozi wa Tanzania kuwa yaliyotokea Sierra Leone, Rwanda, Sudan, Kenya na sasa Ivory Coast wasije kushangaa yakatokea Tanzania. Ufisadi ukizidi mipaka ni maafa kwa taifa na ile amani tuliyokuwa tunaimba tutakuja kuikumbuka sana kwani itakuwa haipo tena!!!
 
mods wakati mwingine mnaharibu ladha za topics!! Kulikuwa hakuna sababu za kuunganisha hizi topic 2


  1. Ngeleja: You can go and p@#& yourself!!
  2. Ngeleja analipa fadhila kwa rostam aziz
 
Ngeleja ni mfanyakazi wa Rostam Aziz alikuwa wakili wa VodaCom.

Kwanini serikali ilipe DOWANS wakati wazee wa east afrika wameshinda kesi lakini hawajalipwa?

Wanafunzi vyuo vikuu hawajalipwa mikopo?

Watu wanakufa hosipitalini??

Ongezea hapo RA ni mwanahisa wa Vodacom, akamchukua Ngereja akumpa support jimboni kwake kapata ubunge na moja kwa moja kumpatia Wizara ya Nishati na Madini ili awe daraja lake. Nawaambia RA ndiyo anayeharibu mambo yote haya, anatufanya sisi watanzania wote ni mazezeta - kijana mdogo anasumbua umma wote wa watanzania - inatia hasira sana.

Lazima tuilipe Dowans, Tusimlaumu sana Ngereja kapewa maelezo na mabosi wake RA na JK, hana la kufanya sababu kazi yenyewe kapewa, akienda kinyume yatamkuta yaliyompata kaka yangu 6.
 
Baada ya kutajiwa makampuni yenye hisa na wakurugenzi wake, maswali yamekuwa mengi kuliko majibu. Nadhani sasa wakati umefika wa kusema bayana 'enough is enough'. Zile salamu za Arusha zikiingia jijini, hakuna kitakacholipwa. Wanashabikia kulipa kwa sababu wanajua malipo hayo yanapotelea hapa hapa bongo!
 
hiyo website anayo salva,wala usiumize kichwa kuitafuta.huyo ndie anaeratibu na kusimamia shughuli zote za mkwere,wako kibiashara zaidi hapo mjengoni.kweli watanzania hamnazo wanatupindua kama samaki mwanzo walisema kampuni iko costa rica sasa wanasema iko canada tuelewe lipii? Sijui hizo hela wataweka kwenye account gani coz hata atakae zi draw atakua kama chenge na rada transaction zakumwaga
 
DOWANS ofisi zao nasikia ziko pale UBUNGO PLAZA ila nimesikia kua wanazifunga na watawapa ORXY ltd. Sasa nadhani watalipana mtaani au kwakua waliotanjwa jana sio wamiliki halali (wale ni wamiliki hewa), watawalipa wamiliki wanaojulikana. Nadhani Mwanahalisi, Sitta wanamajina kamili kwani Sitta alisema ni genge la watu watatu na Mwanahalisi lilijaribu kuwataja kwa wadhifa wao (lilisema: Mmoja ni mfanyabiashara ambaye pia ni Mbunge, 2. Ni mwanasheria ambaye kampuni yake inauhusiano ya kampuni ya wingereza, 3. ni waziri ambaye kwa sasa hayuko kwenye baraza la mawaziri la JK)
Nimejaribu kusearch(google) kama ninaweza ipata compamy ya dowans siipati,
Mwenye kujua msaada please......
 
Website ya nini? Kwani kampuni zote duniani lazima ziwe na website?

Mijitu mingine bwana, ajabu kweli kweli.
 
Website ya nini? Kwani kampuni zote duniani lazima ziwe na website?

Mijitu mingine bwana, ajabu kweli kweli.

Bwana Mkubwa sana....hivi biashara halali inayojipatia $65m inawezekana isiwe na website kweli?au hujui website ni nini?uko dunia gani wewe?
 
kwa hiyo unatakubaliana kuwa data zilizotolewa, kweli tanzania kuna vilaza. Na wametoa hivyo wakijua kuna vilaza wengi kama wewe ambao wataamini.....
 
Ngeleja acha kujidhalilisha kwa kuchanganyacganya maneno,juzi hapa mpaka na waziri wako mkuu mlikuwa "hamuwajui" leo hii mnakuja na majina yasiyoeleweka...
 
Back
Top Bottom