Waziri wa nishati na madini William Ngeleja amesema serikali imeridhia Kuilipa kampuni ya Kuzalisha umeme wa gesi Dowans Tanzania tsh 95 bilion baada ya kufanya marekebisho ya madai tofauti na pesa walizokua wanadai... pia amewataja wamiliki wa Dowans kama ni Dowans costarica and spartek ya Singapore....
Source: Capital redio news saa 12:00 jioni
UPDATES:
Kutoka Tanzania Daima
===============
Serikali yasalimu amri Dowans
• Ngeleja atangaza rasmi kulipa mabilioni ya fidia
na Betty Kangonga
HATIMAYE serikali imetangaza rasmi uamuzi wa kuridhia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuilipa fidia ya shilingi bilioni 94 Kampuni ya Dowans Holdings.
Msimamo huo rasmi wa serikali unaotokana na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICC) ulitangazwa mbele ya waandishi wa habari na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Akitangaza uamuzi wake huo, Ngeleja ambaye alisahihisha taarifa za vyombo vya habari kuhusu kiasi halisi kinachopaswa kulipwa badala ya kile cha shilingi bilioni 185 zilizokuwa zikitangazwa awali, alisema wanasubiri kusajiliwa kwa uamuzi huo wa ICC katika Mahakama Kuu ya Tanzania kabla ya utekelezaji wa malipo kufanywa.
Ngeleja alisema uamuzi huo wa kuilipa Dowans umezingatia ushauri wa kisheria uliotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wanasheria wa TANESCO.
Alisema serikali imeamua kutekeleza uamuzi huo wa mahakama hiyo ili kuepuka gharama zaidi za tozo iwapo itashindwa kutekeleza uamuzi wake kwa wakati.
Habari ambazo Tanzania Daima inazo zinaeleza kuwa mara tu baada ya hukumu hiyo kusajiliwa Mahakama Kuu, iwapo serikali itashindwa kulipa itakuwa ikitozwa kiasi cha ziada cha shilingi milioni 25 kila siku.
"Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO ilishauriwa na wanasheria wake wa Kampuni ya Rex Attorneys Advocates pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali tukubaliane na hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo bila kupinga endapo itasajiliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania," alisema.
Alisema kutokana na hukumu hiyo Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development LLC haitalipwa kiasi chochote cha fedha kama ilivyokuwa ikidai fidia ya dola milioni 169 kutokana na kashfa iliyofanywa na TANESCO.
Ngeleja alisema kuwa ni vyema wananchi wakaendelea kuheshimu na kuthamini matumizi ya sheria za nchi na za kimataifa na kuamini kuwa mgogoro wa Dowans na TANESCO ni suala la kisheria na si vinginevyo pamoja na kuwa matokeo hayo yamelitia hasara taifa.
"Wakala wa usajili wa Makampuni na Biashara nchini (Brela) ndio wenye kumbukumbu za makampuni yote yaliyosajiliwa, hivyo suala la kujua wamiliki au wakurugenzi wa kampuni si hisia wala kuzusha, ni jambo linaloweza kuthibitishwa na wakala huo," alisema.
Ngeleja alitumia mkutano huo kuwataja wamiliki wa Dowans baada ya kupata taarifa kutoka Brela kwa barua yenye kumb. namba MITM/RC/58550/22 ya Januari 5, mwaka huu ambao ni Dowans Holdings S.A, yenye hisa 81 ya Costa Rica na Portek System and Equipment PTE Limited hisa 54 ya Singapore.
Alisema wakurugenzi wa Dowans wa hapa nchini ni Andrew James Tice (Canadian), Gopalakrishnan Balachandran (Indian), Hon Sung Woo (Singapore), Guy Arthur Picard (Canadian), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenyan).
Wakati Ngeleja akitaja majina hayo, wiki moja iliyopita Tanzania Daima ilikwisha kuwataja wanaomiliki kampuni hiyo.
Alisema hakuna sheria inayowataka wawekezaji wakitaka kuanzisha kampuni nchini ni lazima awepo mbia wa ndani, wanaweza kuanzisha wenyewe ikiwa wamefuata taratibu na sheria za nchi.
Alisisitiza kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya ulipwaji fidia wa sh bilioni 94 kwa Dowans na TANESCO kupandisha bei za umeme kama ilivyoamriwa na Ewura.
"Ni upotoshaji mkubwa kuhusisha mambo mawili tofauti... migogoro ya Richmond na Dowans ilipelekwa ICC mwaka 2008, sasa kwanini watu wanaunganisha haya? Labda hii inatokana na watu kupenda kuchakachua maneno," alisema.
Alisema kuwa kuna bidhaa mbalimbali zimekuwa zikiongezeka bei lakini wanashangazwa na hatua ya Ewura kupandisha gharama hiyo kwa asilimia 18.5 na kusababisha baadhi ya makundi kutaka kuandamana wakati ongezeko la bei ya umeme ni suala la kiuchumi na kibiashara kwa shirika hilo.
Alisema wananchi hawana budi kuhakikisha wanasonga mbele na si kuangalia nani aliyeliingizia taifa hasara ili achukuliwe hatua, bali ni kujua hiyo ni sheria na itabaki kuwa historia.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, William Mhando, alisema kuwa mgawo wa umeme bado utaendelea katika maeneo mbalimbali kutokana na kupungua kwa gesi inayosababisha kuwa na upungufu wa megawatts 50 katika grid ya taifa.
Alisema serikali hadi sasa inadaiwa deni la umeme kiasi cha sh bilioni 70, ambapo Waziri Ngeleja aliahidi kufuatilia madeni hayo na kuyakata moja kwa moja kutoka Hazina ili kuyapunguza.