Waziri Ndugulile na Serikali ya CCM tafadhali kama mmebariki Uhuni huu unaofanywa na Makampuni ya Simu nchini mtuambie

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Haiwezekani naacha Kuungana na Binadamu Wenzangu wote duniani Kusheherekea mwaka huu mpya wa 2021 badala yake naupokea huku nikiwa na Hasira na Uhuni kama siyo Utapeli tunaofanyiwa na Makampuni ya Simu nchini Tanzania na hapa binafsi nauongelea sana huu wangu wa Morocco Smartphone Network.

Haiwezekani Masikini Mimi najipinda zangu huku nikitafuta Pesa kwa shida Kununua Vocha kisha nikijiunga tu iwe ni Kifurushi cha Kawaida au kile cha Chuo kwa GB1 ambayo ni ya Siku 3 na nawasha tu Data kwa dakika 15 nikiangalia Salio la MB nakuta limebaki 150 MB halafu hapo hapo unasindikizwa na Tangazo la Kuwa Kifurushi chako Kimeisha hivyo ufanye haraka uongeze Kingine.

Waziri mpya wa hii Wizara Ndugu Ndugulile na Serikali yako ya Chama cha Mapinduzi tafadhali liingilieni kati hili upesi mno kwani Sisi Masikini tunateseka au kama labda nyie ndiyo mmeubariki Uhuni huu labda ili muweze Kugawana Mapato ya Kuendesha vyema nchi si vibaya mkatuambia ili kama vile tuanze Kujiandaa zaidi Kisaikolojia kwa Kukamuliwa na Kukomolewa hadi tukome.

Na nilidhani tatizo hili labda ni la Mtandao wangu tu ambao nautumia wa Morocco Smartphone Network ila nimeendelea Kuwaulizia na wa Mitandao mingine kama ya Makumbusho Network, Mikocheni kwa Wariaoba Network, Posta Mpya Network na ule wa Mlimani City Network na wao wanalalamika kama Mimi hivi. Tumewakoseeni nini nyie Makampuni ya Simu Tanzania?
 
Kuna mtandao unanunua bando la 1500 ila likiisha wanakuambia kifurushi chako cha buku kimeisha. Huwa ninajiuliza ile 500 inapotea vp
 
Pole sana Ndugulile atalitatua tatizo lako!! Au piga 100 watakupa maelezo jinsi hiyo 1 Gb yako ilivyokata.
 
Mkuu hiyo itakuwa simu yako ina run apps zinazo tumia internet yako zikiwa ktk background bila ya wewe kujua zinafanya hivyo.
Zitakuwa zinafanya update bila wewe kujua.
 
Si lazma app zote zipitie play store n.k.
Zitaji update vipi bila kuziruhusu.
Alafu ndo kila siku hizo app zinajiapp date?
Mkuu hiyo itakuwa simu yako ina run apps zinazo tumia internet yako zikiwa ktk background bila ya wewe kujua zinafanya hivyo.
Zitakuwa zinafanya update bila wewe kujua.
 
mkuu mitano hii watu wa kipato cha chini tutateseka ipasavyo.
Unaijua viieitee wewe?
Hii nchi ni tajiri sana hatuhitaji pesa za mabeberu..
Uchumi wa kati....
Au nasema uongo ndugu zanguuuuu..
 
Attachments

  • Screenshot_20201231-210901.jpg
    Screenshot_20201231-210901.jpg
    80.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom