Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,805
- 4,481
Waziri wa Fedha amewaonya wafanyabiashara wanaowafundisha Watanzania kukwepa kodi kwa kuwapa bei mbili za bidhaa, bei yenye risiti na bei isiyo na risiti. Amesema kuna wafanyabiashara wakidaiwa risiti wanajivuta, mara wanafuta mashine vumbi, hadi anayedai risiti akate tamaa.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema idadi ya miamala ya simu kabla ya tozo na baada ya tozo inalingana, ambayo ni kati ya miamala 10 hadi milioni 11. Amekanusha madai kuwa tozo za miamala zimeshababisha kupungua kwa miamala ya fedha kwa njia ya simu.
Kuhusu anayetoa fedha na ayepokea fedha wote kukatwa tozo, Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba amesema isichukuliwe kuwa kila anayetumiwa fedha ni msaada, kwani wapo wafanyabiashara wa mtandaoni na mafundi wanaolipwa kwa simu, hivyo lazima na wao walipe.