Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 12,160
- 20,337
Akiongea na Wandishi wa habari Waziri wa Afya Nassor Mazirui (ACT wazalendo) amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ipo kwenye mchakato wa kubinafsisha Hospitali zote za Zanzibar ile ziweze kuendeshwa na watu binafsi kuleta tija.
Ikumbukwe tayari mpango huu umeshaanza kutekelezwa hasa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, ambapo huduma zote za Maabara na Vipimo vya Mionzi na Ultrasound tayari zinasimamiwa na makampuni binafsi.
Taarifa zisizo rasmi zinaonesha Lancent Labartories Ltd ndio wanaosimamia mpango huo kwa sasa. Tangu Dr. Ali Hussein Mwinyi aingie madarakani amefanya mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali kisiwani humo.
Katika Sekta ya Afya amefanikiwa kujenga hospitali kubwa za rufaa za mikoa za kisasa na kuajiri idadi kubwa ya madaktari na watoa huduma wa idara mbalimbali. Idadi hiyo inakadiriwa kuwa kiwango kikubwa kuliko awamu zilizopita.
Hata hivyo Dr. Hussein Mwinyi anapongezwa kwa usimamizi mzuri wa rasilimali za umma na hivyo kuungwa mkono na Wananchi wengi.