Waziri Nape Nnauye: Hakuna maendeleo, amani na furaha kama uhuru wa habari katika jamii hiyo haupo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,102
12,559
IMG_20221217_114817_629.jpeg


Waziri Nape ameyasema hayo katika Kongamano hili lenye kaulimbiu ya "Habari kwa maendeleo endelevu", kongamano ambalo limewakutanisha waandishi wa habari pamoja na wadau wengine wa habari kujadili changamoto pamoja na mafanikio kwenye sekta hii, mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Waziri Nape Nnauye katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere (JINCC) Dar es Salaam.

IMG_20221217_114817_553.jpeg

Ni kongamano la kwanza linaloshirikisha vyombo vya habari, wadau wa habari pamoja na Serikali. Kupitia kongamano hili, vyombo vya habari vitapata wasaa wa kujadili mambo mbalimbali yaliyofanyika tangu uhuru, kujitathimini utendaji wake pamoja na kuweka mpango mkakati wa kuendeleza uhuru mpana kwa wananchi kwenye nyanja zote za maisha.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari - Nape Nnauye

~ Makongamano yajayo yaanze kuitwa Kongamano la Kimataifa la Maendeleo ya Sekta ya Habari.

~ Sekta ya habari nchini imetulia na inakwenda vizuri.

~ Kupitia kongamano hili serikali itaweza kupata mkakati kutokana na changamoto zitakazopatikana kupita kongamano hili.

~ Hakuna maendeleo, amani na furaha kama uhuru wa habari katika jamii hiyo haupo ndiyo maana ni muhimu tukakihahakisha uhuru wa habari unalindwa kama msingi wa maendeleo, amani na furaha.

~ Wito kwa wanahabari kuhakikisha kuwa sekta ya habari inakuwa kichocheo muhimu kwa kukuwa kwa sekta nyingine, mfano habari za afya bora na ustawi wa jamii, sekta ya madini n.k.

~ Kama wananchi hawapati taarifa sahihi na kwa wakati sahihi unaweza kuwa mwanya wa upotoshaji kwa wananchi kuwa hakuna kinachotekelezwaa na ni kazi bure.

~ Sasa hivi mazingira ya wanahabari yako vizuri hamna watu wanaofungwa mdomo, hamna watu wanaofinywa finywanywa, wote hatutaiani majaribuni na sekta ya habari inaenda mbele.

~ Sheria na kanuni mbali mbali nchini zinaendelea kufanyiwa marekebisho nchini kwa mujibu wa sheria.

~ sheria ya uhuru wa vyombo vya habari unalindwa kwa mujibu wa sheria na siyo utashi wa viongozi.

~ Nia ya serikali kupitia sera ya habari nchini, na uwezekano wa sheria ya habari na sheria ya utangazaji kuunganishwa ili iwe sheria moja kuunganisha wote kwa pamoja.

~ Wizara itaendelea kushirikiana na wanahabari kuweka mazingira bora katika kutatua changamoto zinazowakabili.

~ 2023 kuweka nguvu za kutosha katika maslahi ya waandishi wa habari na uchumi wa vyombo vya habari ikiwemo kulipa madeni, bima za wanahabari, mikataba, kuongeza ari katika utendaji.

~ Vyombo vya habari kufanya kazi kwa kufata miiko ya nchi yetu, na serikali inawahakikishia usalama katika hilo. Tuna wajibu wa kulinda tamaduni na rasilimali za nchi zetu.

~ Vyomo vya habari viendeleze ushirikano na serikali katika kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali.

~ Kongamano hili litakuwa kubwa na litatumika kama tathmini kwenye sekta ya habari.
 
Back
Top Bottom