Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Viongozi nao walipe Kodi kulinganana na vipato vyao na hii itie ndani mapato yote halali ikiwamo posho na kiinua mgongo.
 
"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”

"Mimi naunga mkono dira ya Rais ya kutaka maji yapatikane kila kijiji, sasa tunafanyaje? tukasema tuchangishane, hivi unaona tunaweza kupoteza maisha ya Mtoto sababu ya maji, kisa unalia unakatwa Tsh.5?, mbona milio ya simu tunaweka na unakatwa Tsh. 100?"———Mwigulu via Clouds360

"Kuna Shule zinakusanya watoto mpaka 1500 au 1000 na Shule haina maji wanaambiwa waende Shule na kidumu cha maji, sasa tunafanyaje ili maji yapatikane? ndio maana kuna uwepo wa kukatwa Tsh. tano kila unapotuma hela kwa ajili ya huu mfuko wa mshikamano"———Mwigulu via Clouds360

"Watu wanalalamika kuhusu hela za miamala, hii ni solidarity fund, tuna mambo ambayo tunakubaliana hayapaswi kuendelea mfano ubovu wa Barabara vijijini, kama Taifa tuongeze Tsh.100 katika mafuta ili kila fedha itakayoongezeka iende kuleta maendeleo"——Mwigulu Nchemba via Clouds360

"Kwenye chungu, ni lazima bajeti, fedha zitatoka wapi ni lazima tutoe kodi, mwaka huu tumeleta kodi ya miamala, ni vizuri sana mjue hili la kwenye miamala sio tu kodi, hili tunatunisha mfuko, ni solidarity fund, huu ni mfuko wa mshikamano wa Watanzania"

"Akaunti zilifungwa kipindi kile kwasababu ya masuala ya kikodi na Wafanyabiashara wanarudishiwa fedha zao kwasababu akaunti imelipa kodi au hesabu zake zilipigwa vibaya kwahiyo kuna fedha ambayo haikuwa kodi inarudishwa"

"Kenya, Uganda, Malawi, Rwanda, Msumbiji mafuta yako bei juu kuliko sisi, ulishaona hizo Nchi waje kununua mafuta Tanzania?, nitoe rai Watanzania wawe Wazalendo kwasababu kwenye Nchi zote zinazotuzunguka Tanzania ndio Nchi inayouza mafuta bei ya chini"
huyu ndie mtu aliekuwa akitangaza nia ya kugombea uraisi tuna raisi mchumi tuna makamu wake tunawaziri pia alafu mwisho wasiku wanakuja na mawazo mufilisi kama haya juu ya namna ya kumuibia mwananchi ukiangalia hizo nchi jirani anazozungumzi kwenye uuzji wa mafuta kuongeza sh mia vip rea sjui madudu kibao wamejilimbikizia % kubwa serikli mwekezaji na mlaji hawafaidiki kwa usawa hiyo ndo ccm
 
Miwatu kama hiyo ni ya kucharazwa viboko mia moja ili akili zimrudie,

Na mbona aongea kama anatusuta vile? Tumemkosea nini sisi wananchi wanyonge
emoji23.png
Kuna pesa huwa zinakatwa miaka nenda rudi kwenye mafuta na hata kwenye magari yanayoingizwa nchini inaitwa railway levy, lakini bado utaambiwa pesa kibao zimeshakopwa kwa ajili ya SGR na bado utaambiwa hakuna pesa kukamilisha mradi wa SGR, halafu unatuletea hapa takataka nyingine, sijui solidarity fund..........yaani mnajikusanyia pesa kwa ajili ya matumizi yenu ya kifisadi mnakuja kutulaghai na maneno ya solidarity fund, hopeless....
Kwenye magari ni balaa gari ukiagiza milioni Tano,kigari kidogo tu cc 1500 andaa milioni saba ya kukomboa bandarini jamaa wanapiga pesa ndefu kuzidi hata makampuny ya kutengeza magari
 
"Kuna Shule zinakusanya watoto mpaka 1500 au 1000 na Shule haina maji wanaambiwa waende Shule na kidumu cha maji, sasa tunafanyaje ili maji yapatikane? ndio maana kuna uwepo wa kukatwa Tsh. tano kila unapotuma hela kwa ajili ya huu mfuko wa mshikamano"———Mwigulu via Clouds360
Asanteni sana CCM kwa kuendelea kutunyonya, tunawashukuru sana your time is coming.
 
Kwahio ILANI YA CCM imekosa sources of funds wameishia kurudi kutukamua tena
 
Yanamwisho huu ni uwizi ulio halalishwa lazima tuchukue hatua.
Hakuna dhambi kama kuongozwa ni viongozi wapumbavu
 
Kwenye magari ni balaa gari ukiagiza milioni Tano,kigari kidogo tu cc 1500 andaa milioni saba ya kukomboa bandarini jamaa wanapiga pesa ndefu kuzidi hata makampuny ya kutengeza magari
Na hapo bado haziwatoshi wanakuja na uhuni wa solidarity fund, hawa watu kuna namna wanatuona hamnazo, si bure......
 
Solidarity fund inatumika kulipana posho za kuzunguka na mi vieitee!!??
Yaani tunachangia hawa viongozi kula keki ya taifa peke yaoo!!?
Solidarity fund ya kuendesha viieite la madelu, ama kweli hakuna nchi rahisi kuongoza kama nchi ya wadanganyika.....
 
Upo Msemo mmoja unasema, KWA KUNWI HAKULIWI BALI KWA MWALI...

MR WAZIRI
Wazo lako ni brilliant yaani mwaaa. Tatizo ni kwamba huo mfuko hauna baraka za wachangiaji hivyo hata kama hamta chotamo ila hamuaminiki kwakuwa hamjawahi kuwa waaminifu.

Mtego wenu:
Iwapo reflection haitakuwa vivid ndicho kitakua kichinjio chenu 2025 na mkileta ujanja tutajua namna gani tutawashuhulikia ila YOU SHALL NEVER GET AWAY WITH IT. Hiyo sio ahadi bali wajibu.
 
Halafu huyu #Mwigulu Nchemba ndio
Anataka kua presidential material Kwa akili zake hizi dedeq
Hebu aweke salary slip yake hapa huyu mpuuzi kisa yeye anawekewa vocha na bundle Kwa Kodi zetu ndio anakuja na wazo la kipuuzi Kama Hilo aiseee

CCM mmelaaaniwa Kwa kutuwekea mawaziri wenye akili dizaini ya mtu pori jiwe!
 
Kwenye magari ni balaa gari ukiagiza milioni Tano,kigari kidogo tu cc 1500 andaa milioni saba ya kukomboa bandarini jamaa wanapiga pesa ndefu kuzidi hata makampuny ya kutengeza magari
mkuu unajua hili swala linanishangaza Sana yaani Kodi inazidi Bei ya gari aiseee huuu upumbavu wa serikali ya haya maCCM hauvumiliki
Hua napata hasira Sana nikifikiria Hilo swala Hivi inashindikana vipi Kodi ikawa hata million Moja raia hasa wakulima wakawa na magari ya kubebea mazao Huko vijijini yakaongeza chachu ya maendeleo?

Inaudhi Sana mkuu!
 
Wazo zuri la kuchangia ila matumizi yenu nyine kina mwigulu ni anasa sana, wananchi wapo wiling kuchanga ila nyie hamjibani ,mnazidi kununua mavx ya milioni 400 kila moja, ma perdiem yasiyo na kichwa wala miguu wakati tuna mkongo wa taifa, tuna zoom, yaani unafunga safari ya zaidi ya km 600 na msafara wa magari 20 kwenda kukata utepe? Kama kuchangia mbona nyinyi viongozi hamchangii yaani wanachangia walalahoi tu?

1.jpg
 
Badala ya kuvifuta vyeo vya kipuuzi kama vya wakuu wa mikoa na wilaya, kuondoa wabunge wa viti maalum na wale wa kuteuliwa! Kuondoa vyeo vya Ma Ras na Ma das, kupeleka mswada wa kupunguza posho nono wanazolipwa bungeni!

Yeye anakimbilia kwenye TOZO!! Kuna mijitu ni Mibinafsi, ila miana siasa aina ya Mwigulu Nchemba, imepitiliza aisee!!
Tatizo ni MTU analipa kodi zote stahiki na kubaki na hela yake stahiki!! Akitaka kumtumia mwanae ada, au kumtumia ndugu, jamaa au kulipia chochote anaambiwa lipa hela ya solidarity!! Hii ni double taxation!! Kodi inayotakiwa hapa ni gharama ya biashara ya mtoa huduma (ie Tigo au Airtel) achangie kodi kwa kuwezesha hii huduma na sio kukata hela ya Mteja!!
 
Nafikiri ni wakati wananchi wote kutozwa kodi.Ingekuwa busara na wale wa mjengoni wakatwe kodi na kuchangia kwenye mifuko ya mafao.Hapo kila mmoja wetu angejua maumivu ya kulipa kodi.Hivyo kila mtu angehakikisha hakuna hata kodi itakayotumika tofauti na mipango tuliyojiwekea
 
Back
Top Bottom