Waziri Murkomen aahidi adhabu kali kwa uharibifu uliofanyika kwenye barabara ya 'Nairobi Expressway'

Kenyan

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
414
313
Maandamano ya Jumatano yalishuhudia uharibifu mkubwa zaidi ikilinganishwa na ya hapo nyuma huku waandamanaji wakiharibu barabara maarufu ya Expressway, ambayo ilikuwa ndio mradi mkubwa zaidi na wa mwisho aliofanikisha Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Barabara hio ambayo watumiaji wake hulazimika kulipa ada Ili kutumia inaunganisha Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na eneo la Westlands.

Uharibifu wa leo umepelekea serikali kusitisha matumizi yake huku Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen akiapa kuwadhiibu wahusika.

Kwenye taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari, Murkomen ametoa rai kwa IGP Japheth Koome, kuanzisha uchunguzi mara moja kwa kutumia kamera za CCTV zilizoko barabarani humo, kuwakamata waharibifu. Aidha Murkomen ametoa onyo kwa Viongozi wa Upinzani wakiongozwa na Raila Odinga kuwa iwapo uharibifu wa barabara utaendelea basi watachukuliwa hatua kisheria na kushurutishwa kugharamia uharibifu.

Maandamano ya leo yamepelekea vifo vya watu 7 huku wengine wakiuguza majeraha ya risasi katika hospitali mbalimbali.

20230712_201623.jpg
20230712_170131.jpg
20230712_170135.jpg
 
Kingereza kingi akili zimeshikiliwa na mjaluo mmoja ....Bure kabisa....Kila cku wanabeba sufuria wnalilia unga.... Wakenya nani kawaroga ?
 
Back
Top Bottom