Waziri Muhongo akataa chakula hotelini aenda kwa mamalishe

Waziri Muhongo akataa chakula hotelini aenda kwa mamalishe

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
waziri_muhongo.jpg


Profesa Muhongo
Na Jackson Odoyo




Arusha
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekataa chakula Hoteli ya Mount Meru na kwenda kula chakula cha Mamalishe.
Tukio hilo lililowashangaza watu 13 waliokuwa katika msafara wake lilitokea hivi karibu wakati

Profesa Muhongo alipokwenda Arusha kwenye mkutano wa wataalamu wa umeme wa nchi 11 za Afrika Mashariki, Kati na Kaskazini.

Waziri Muhongo aliandaliwa chakula hotelini hapo, lakini aliwashangaza wenyeji wake ambao ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na uongozi wa wizara yake.

Baada ya kufika katika mgahawa wa Pizza Point uliopo katikati ya mji wa Arusha, Waziri Muhongo aliagiza ugali na samaki kwa bei ya Sh7,000.

Tukio la waziri huyo kukataa kula chakula cha usiku katika hoteli hiyo ya kifahari, iliwashangaza hata wafanyakazi wa mgahawa huo baada ya kupata taarifa hiyo.
Ingawa haikufahamika mara moja sababu za waziri huyo kukataa kula katika hoteli hiyo kutokana na kuchukua uamuzi ghafla, lakini taarifa za ndani zinadai hakutaka kutumia fedha za walipa kodi kwa matumizi binafsi.

“Waziri aliandaliwa chakula katika Hoteli ya Mount Meru Arusha na mpaka tunatoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), ilijulikana tunakwenda kwenye hoteli hiyo lakini chakushangaza alipofika karibu na geti la kuingia hapo, akabadili uamuzi na kuamuru apelekwe mahali atakapopata chakula cha Kitanzania, huku akisema haoni sababu ya kula vyakula vya bei mbaya wakati kuna Watanzania hawana umeme,” alisema ofisa mmoja wa wizara hiyo ambaye hakutaka kutajwa na kumkariri Waziri Muhongo:

“Nipelekeni mahali nitakapopata chakula cha Kitanzania, ili tuwe sawa na Watanzania wenye hali ya chini kwani hizi fedha tunazokwenda kula huko ni jasho lao.”

Hata hivyo, Profesa Muhongo anadaiwa kuruhusu maofisa waliokuwa kwenye msafara wake ambao wangependa kula Mount Meru kuwashusha, ili akitoka kwa mamalishe awapitie kwa sababu kila mtu ana uamuzi wake.

Msafara wa waziri huyo ulikuwa na watu 13 akiwamo Msaidizi wake na Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud ambao wote walilazimika kula chakula katika banda la Pizza Point.

Mmiliki wa mgahawa huo, Grace Lyatuu alisema hakutarajia ujio wa waziri huyo na msafara wake, lakini baada ya kutambua kuwa ni Profesa Muhongo akamshukuru Mungu kwa kumfikisha hapo.

“Kwakweli ilikuwa ni usiku mgumu kwangu, kwani msafara ulikuwa mkubwa na wagafla, sikuwa na uhakika wa kupata vyakula vya kuwatosha lakini baada ya chakula kupatikana nikamshukuru Mungu kwani ilikuwa ni usiku na tulikuwa na maandalizi ya kufunga mgahawa,” alisema Lyatuu.

Profesa Muhongo alitumia Sh100,000 kwa chakula cha watu 13 na vinywaji na kuokoa zaidi ya Sh344,500.
 
Kukataa wakati maandalizi yashafanywa na bili zishalipwa maana yake nini!
Angekataa mapema wakati hajaondoka Dar, au la asingetoa hiyo sababu ya kusema anaokoa hela ya Watanzania maana hadi hapo tayari zishaliwa!
Hii ni kama ya Pinda Kayanza kukataa V8 LA kisasa la MIL 200(Kilimo-Kwanza), wakati tayari lishanunuliwa!
Attention seeking!


Pichani: KILIMO-KWANZA
Toyota-Land-Cruiser-USC00TOS121A0101-F.jpg
 
Noted, sio kila mara kugawana keki na walio juu tu.
 
Anafanya hivyo siku zote au alikwepa polonium kwenye msosi wake! Hajanishawishi bado. Anatumia gari gani, Suzuki au Toyota v8?!
 
Kunamtu kanidokeza kwamba ni zile intelejensia za kijadi zilimlazimisha kufana hivyo kwa kuhofia kuwekewa vitu vinavyoweza kudhuru afya.
Naomba ieleweke jamani ni tetesi na hazijathibitishwa.
 
jamaa alishtukia dili, either aliogopa sumu ya mwakyembe! ci mnajua jamaa anatafutwa na mgawo maker!

wewe ni intelligent sana na umeona mbali pia una upeo,salut.machale yalimcheza siyo kusave pesa sababu pesa zilishalipwa mapema
 
Siyo kwamba ni mzalendo bali ni woga wakudhuriwa na wahasimu wake wa tanesco
 
This dude seems to be a descent guy.I wish him all the best...is really a nice guy.I have also met him some where very local having a lunch.Big up prof Muhongo....
 
Kuwadanganya wabongo ni rahisi sana...

Kuwa msanii tu utafanikiwa mambo mengi sana
 
Point muhimu hapa ni kuwa Mama Lyatuu, aliingiza Laki moja bila kutegemea. Mengine kwangu si muhimu. Wangelikuwa wakifanya hivyo mara kwa mara, ingelikuwa inasaidia sana watu masikini nao wapate chchote.

Profesa Muhongo alitumia Sh100,000 kwa chakula cha watu 13 na vinywaji

Lakini ch muhimu ni kuwa Watanzania tunataka UMEME. Kula kwa Mama Ntiliye ni uamuzi wake na si kuokoa hela zetu. Kama alitumia hela yake, sisi hatuna shida naye. Tunataka UMEME na madini yetu yatumike vizuri. Mengine si muhimu kabisa kwetu.
 
Huyo ni msanii, kama hawezi kula chakula cha bei mbaya kwa sababu wa tz hawana umeme mbona amesafiri kw ndege???, mbona anatumia gari la bei mbaya?????? AACHE USANII WA KITOTO.
 
Back
Top Bottom