Waziri Muhongo akataa chakula hotelini aenda kwa mamalishe

Mzee bwana,naona machale ya kijita yalimcheza hakuna cha chakula ghali wala nini
 
waziri_muhongo.jpg

Profesa Muhongo
Na Jackson Odoyo

Arusha
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekataa chakula Hoteli ya Mount Meru na kwenda kula chakula cha Mamalishe.
Tukio hilo lililowashangaza watu 13 waliokuwa katika msafara wake lilitokea hivi karibu wakati

Profesa Muhongo alipokwenda Arusha kwenye mkutano wa wataalamu wa umeme wa nchi 11 za Afrika Mashariki, Kati na Kaskazini.

Waziri Muhongo aliandaliwa chakula hotelini hapo, lakini aliwashangaza wenyeji wake ambao ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na uongozi wa wizara yake.

Baada ya kufika katika mgahawa wa Pizza Point uliopo katikati ya mji wa Arusha, Waziri Muhongo aliagiza ugali na samaki kwa bei ya Sh7,000.

Tukio la waziri huyo kukataa kula chakula cha usiku katika hoteli hiyo ya kifahari, iliwashangaza hata wafanyakazi wa mgahawa huo baada ya kupata taarifa hiyo.
Ingawa haikufahamika mara moja sababu za waziri huyo kukataa kula katika hoteli hiyo kutokana na kuchukua uamuzi ghafla, lakini taarifa za ndani zinadai hakutaka kutumia fedha za walipa kodi kwa matumizi binafsi.

“Waziri aliandaliwa chakula katika Hoteli ya Mount Meru Arusha na mpaka tunatoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), ilijulikana tunakwenda kwenye hoteli hiyo lakini chakushangaza alipofika karibu na geti la kuingia hapo, akabadili uamuzi na kuamuru apelekwe mahali atakapopata chakula cha Kitanzania, huku akisema haoni sababu ya kula vyakula vya bei mbaya wakati kuna Watanzania hawana umeme,” alisema ofisa mmoja wa wizara hiyo ambaye hakutaka kutajwa na kumkariri Waziri Muhongo:

“Nipelekeni mahali nitakapopata chakula cha Kitanzania, ili tuwe sawa na Watanzania wenye hali ya chini kwani hizi fedha tunazokwenda kula huko ni jasho lao.”

Hata hivyo, Profesa Muhongo anadaiwa kuruhusu maofisa waliokuwa kwenye msafara wake ambao wangependa kula Mount Meru kuwashusha, ili akitoka kwa mamalishe awapitie kwa sababu kila mtu ana uamuzi wake.

Msafara wa waziri huyo ulikuwa na watu 13 akiwamo Msaidizi wake na Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud ambao wote walilazimika kula chakula katika banda la Pizza Point.

Mmiliki wa mgahawa huo, Grace Lyatuu alisema hakutarajia ujio wa waziri huyo na msafara wake, lakini baada ya kutambua kuwa ni Profesa Muhongo akamshukuru Mungu kwa kumfikisha hapo.

“Kwakweli ilikuwa ni usiku mgumu kwangu, kwani msafara ulikuwa mkubwa na wagafla, sikuwa na uhakika wa kupata vyakula vya kuwatosha lakini baada ya chakula kupatikana nikamshukuru Mungu kwani ilikuwa ni usiku na tulikuwa na maandalizi ya kufunga mgahawa,” alisema Lyatuu.

Profesa Muhongo alitumia Sh100,000 kwa chakula cha watu 13 na vinywaji na kuokoa zaidi ya Sh344,500.
Wakuu watu wenye mawazo aina hii ndio tunao wahitaji Tanzanaia ya sasa period!!!!
 
hapana mi nahisi kuna kitu....sasa yeye anasema anataka ale chakula cha bei rahisi ili awe karibu na watanzania wa hali ya chini wakati alikula ugali na samaki iliyocost shs 7000, je watanzania wa kawaida wanakulaga ugali na samaki kwa sh 7000? asituzingue na yeye. Ale mount meru asile bado watanzania wengi tu watakua hawana umeme
 
aliogopa watamumwakyembe...Tanzania sasa hivi hatuaminiani, hata mimi mara nyingi nikiwa bara uani naenda na taska yangu.!
 
toyota-vitz-90f34085e0_t.jpg

Smile, kama serikali ingekuwa inabana
matumiz kwa nini, hawatumie gari
aina ya Ritz.
 
Last edited by a moderator:
Akatae ufisadi na si chakula ingawa ni haki yake kuchagua wapi ale au kutokula. Nadhani ameishajua hatari inayomkabili hasa akiona watu kama Mwandosya na Mwakyembe wanavyoteseka. Isitoshe nchi yetu sasa imegeuka nchi ya manyang'au. Ukicheza na ulaji wa watu wanaweza kukutoa roho.
 
Hana lolote, anatafuta umaarufu tu na subiri watamdondosha sasa hivi? Yaani unataka kuniambia anataka kusumanga wale wananaosafiri kama Vasco Da Gama na msafari kebe kebe??!! Thubutu!!!
 
Hivi mpaka sasa hivi kwenye huu utawala wa JK mpaka sasa hivi tuko serials Drama ya ngapi?
 
HAPANA. HAIJI AKILINI. Kama ni kumkolimbalize au kum mwakembelize hawezi kukwepa kwa namna hiyo.
 
Jamani tusikuze jambo. Hata mimi mtu wa kawaida sipendi vyakula vya mahotel makubwa kwa sababu vina preservatives nyingi. Wengine tuna allergy. Chakula cha Mama ntilie siku zote huwa ni natural. Lakini pia inawezekana waziri alishtukia deal la kuwekewa kitu mbaya kwenye chakula na hii ni kawaida kwa nchi yetu kwa sasa.
 
Toa ubwege, hivyo vijisenti ndo unaongelea, acheni usanii nyinyi na kuwafanya wabongo mabwege.
 
Ilibidi afanye hivyo ili kuokoa maisha yake maana wale waliokuwa wanatengeneza mgao feki ili wauze majenereta bado wapo na hawajapenda jinsi anavyowanyima ulaji.Hongera Prof kwa kuruka viunzi.Endelea hivyohivyo
waziri_muhongo.jpg

Profesa Muhongo
Na Jackson Odoyo

Arusha
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekataa chakula Hoteli ya Mount Meru na kwenda kula chakula cha Mamalishe.
Tukio hilo lililowashangaza watu 13 waliokuwa katika msafara wake lilitokea hivi karibu wakati

Profesa Muhongo alipokwenda Arusha kwenye mkutano wa wataalamu wa umeme wa nchi 11 za Afrika Mashariki, Kati na Kaskazini.

Waziri Muhongo aliandaliwa chakula hotelini hapo, lakini aliwashangaza wenyeji wake ambao ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na uongozi wa wizara yake.

Baada ya kufika katika mgahawa wa Pizza Point uliopo katikati ya mji wa Arusha, Waziri Muhongo aliagiza ugali na samaki kwa bei ya Sh7,000.

Tukio la waziri huyo kukataa kula chakula cha usiku katika hoteli hiyo ya kifahari, iliwashangaza hata wafanyakazi wa mgahawa huo baada ya kupata taarifa hiyo.
Ingawa haikufahamika mara moja sababu za waziri huyo kukataa kula katika hoteli hiyo kutokana na kuchukua uamuzi ghafla, lakini taarifa za ndani zinadai hakutaka kutumia fedha za walipa kodi kwa matumizi binafsi.

“Waziri aliandaliwa chakula katika Hoteli ya Mount Meru Arusha na mpaka tunatoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), ilijulikana tunakwenda kwenye hoteli hiyo lakini chakushangaza alipofika karibu na geti la kuingia hapo, akabadili uamuzi na kuamuru apelekwe mahali atakapopata chakula cha Kitanzania, huku akisema haoni sababu ya kula vyakula vya bei mbaya wakati kuna Watanzania hawana umeme,” alisema ofisa mmoja wa wizara hiyo ambaye hakutaka kutajwa na kumkariri Waziri Muhongo:

“Nipelekeni mahali nitakapopata chakula cha Kitanzania, ili tuwe sawa na Watanzania wenye hali ya chini kwani hizi fedha tunazokwenda kula huko ni jasho lao.”

Hata hivyo, Profesa Muhongo anadaiwa kuruhusu maofisa waliokuwa kwenye msafara wake ambao wangependa kula Mount Meru kuwashusha, ili akitoka kwa mamalishe awapitie kwa sababu kila mtu ana uamuzi wake.

Msafara wa waziri huyo ulikuwa na watu 13 akiwamo Msaidizi wake na Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud ambao wote walilazimika kula chakula katika banda la Pizza Point.

Mmiliki wa mgahawa huo, Grace Lyatuu alisema hakutarajia ujio wa waziri huyo na msafara wake, lakini baada ya kutambua kuwa ni Profesa Muhongo akamshukuru Mungu kwa kumfikisha hapo.

“Kwakweli ilikuwa ni usiku mgumu kwangu, kwani msafara ulikuwa mkubwa na wagafla, sikuwa na uhakika wa kupata vyakula vya kuwatosha lakini baada ya chakula kupatikana nikamshukuru Mungu kwani ilikuwa ni usiku na tulikuwa na maandalizi ya kufunga mgahawa,” alisema Lyatuu.

Profesa Muhongo alitumia Sh100,000 kwa chakula cha watu 13 na vinywaji na kuokoa zaidi ya Sh344,500.
 
Eti alikuwa hataki kutumia vibaya hela za wazalendo? Si alilipwa per diem? Chakula kimeandaliwa halafu yeye anajifanya kuktaa, usanii uliochanganyika na uoga wa kwenda Apollo
 
Hakuna kingine hapa, tukubaliane tuu prof alikuwa anaruka kihunzi. Nadhani chale zilimcheza akashituka kuwa ule ndo ungekuwa mwisho wake. Ile pollonium ya mwakyembe ilikuwa tayari inamsubiri.
 
Hivi walilala Guest house gani vile? Maana pale Mount Meru per night nadhani sio chini ya $200. Hapo ndo utajua kama kweli alikuwa na lengo la kuokoa hela za waTz au alikuwa na lake jambo binafsi.
 
Jamani tusikuze jambo. Hata mimi mtu wa kawaida sipendi vyakula vya mahotel makubwa kwa sababu vina preservatives nyingi. Wengine tuna allergy. Chakula cha Mama ntilie siku zote huwa ni natural. Lakini pia inawezekana waziri alishtukia deal la kuwekewa kitu mbaya kwenye chakula na hii ni kawaida kwa nchi yetu kwa sasa.

Hivi mama Ntilie unamjua au unaongea tu, Mtu mwenye Pizza cafe unamuita mama ntilie!? kuna mama ntilie anauza ugali samaki Shs 7,000? Mama ntilie nimjuae mimi chakula chake ghali sana 2000.
 
Back
Top Bottom