Waziri Mpango: Rais Magufuli amenipigia simu kuhusu michango ya Bashe na Nape Bungeni

serikali iamue tu upande upi ujamaa au ubepari
Hili ndio jambo muhimu sana.
Kuwa kotekote ni ngumu sana utekelezaji wa sera za kitaifa hasa kukiwa na watekelezaji/watendaji wasio na uelewa mkubwa wa dhana yeyote au mojawapo ya hizo mbili, yaani ujamaa au ubepari.

Naona China wenzetu wamejua kuchanganya hivi vitu viwili ndio maana wanaendelea kwa kasi.
 
Nape na Bashe wanacho jua ni kuropoka..... hizo tenda hutangazwa wazi na hao wawekezaji wa ndani hawabanwi kuomba ninacho waondoa ni mtaji na vigezo na si kubaguliwa.
Nape na Bashe watupe mifano ya miradi walio pewa wawekezaji wa ndani ambayo hadi sasa tunaweza jivunia .....ni mashirika na kampuni na viwanda vingapi vimekufa chini ya mwamvuli wa sekta binafsi tena wawekezaji wa ndani?

Nape na Bashe watupe mifano ya nchi ambazo hiyo miradi mikubwa imetekelezwa na sekata binafsi moja kwa moja kwa kutumia hele zao na serikali hakituoa hela kwa njia yeyote ile...

Kwa sababu wamepewa fursa ya kuwapeleka hao wawekezaji basi hiyo ni suluhu kuliko kupigizana kelele.....
baadaye hutasema walikuwa na maslahi binafsi.?
 
Dr Mpango wanafanana na Prof Muhongo wako very arrogant
Miaka ya nyuma wasomi wa kiwango cha uprofesa walikuwa hawapewi nafasi za uwaziri.

Kwa sababu ya uchache wao, lakini kuanzia awamu ya Mkapa mpaka sasa maprofesa wetu wanatuonyesha makucha halisi ya wasomi wa kiafrika, majivuno kwa wingi kwa sababu ya shida ya kufikia hadhi ya usomi walionao.

Wamesota sana kwenye utafutaji wa elimu ngazi ya chini, wanapofika ngazi za juu kile kiburi cha kuisotea elimu yao kinakuwa wazi kwa kila wanayekutana nae maishani.
 
Unajua JPM huwa amegundua yeye wa TZ niwaoga sana lkn ni watu hatari mno kwani huwa wanatenda kimya kimya!
 
kwa hiyo wale wabunge waliokuwa tofauti na mawazo hayo hasa wale wa ccm inabidi waunge mkono tofauti na mawazo yao
 
Je ni kweli growth rate inapungua kama unavyosema????na kama ni kweli unatumia takwimu za wapi???

Pili unaposema taasisi huru za uchumi ni kama zipi??? Maana kuna taasisi kama Repoa, ESRF, IMF, World Bank na AfDB huwaga wanafanya analysis za kiuchumi pia na majibu yao hayatofautiani sana na Takwimu na NBS......

unaposema ni makosa kulinganisha nchi na nchi unaweza kuwa sahihi lakini katika nadharia ipi??

Sidhani kama Dr. Mpango ni Illectual Arrogance....maana amejibu maswali kwa kadiri alivyoulizwa haja mtukana au kuonesha hoja ya fulani kuwa haifai ila ametoa maelekezo na mapendekezo

Yea! Kama ulifutilia mjadala toka mwanzo; yaani hotuba ya waziri (pamoja na michango ya wabunge Bashe na Nape), ungeona kwamba kwa mwaka huu uchumi umekadiriwa kukua kwa 6.8% badala ya 7.1%. Hii ni kwa mujibu wa takwimu rasmi. Hata hivyo, viashiria vyote vya "afya" ya uchumi kama banking performance, trade (hasa imports/exports) na stock market performance vinaonyesha uchumi unaporomoka.

Kiujumla taasisi za kiuchumi ni taasisi za kiserikali zenye jukumu la kusimamia masuala kama ya haki za umiliki mali (property rights}, uratibu (regulatory institutions), micro-economic stabilization, institutions for social insurance, institutions for conflict management na zingine zenye majukumu kama haya.

Kwa hapa kwetu tunazungumzia taasisi kama BoT, TIC, Breala, Fair Competition Commission, taasisi ya takwimu na taasisi za uratibu (Ewura, TCRA, Sumatra, TIRA, nk). Hizi taasisi ni muhimu kwa sababu utendaji wake unaoathiri mazingira ya uwekezani mitaji, teknolojia pamoja na uzalishaji wa viwandani nchini hivyo zinapaswa kufanya kazi kwa uhuru (autonomously) bila kuingiliwa kisiasa.

Hata hivyo mifumo ya kisheria ya uanzishaji wa taasisi za kiserikali (mashirika ya umma) iliyopo nchini ni ile ile ya tangu enzi za Ujamaa ambapo haya mashirika yalipaswa kuendeshwa kisiasa kwa kusimamiwa na makada wa chama. Teuzi za watendaji wakuu pamoja na bodi za wakurugenzi wa hizi taasisi mpaka leo zinafanyika kisiasa hivyo kwa vyovyote hizi taasisi haziwezi kuwa huru.

Tafiti zimeonyesha kuna uhusiano mkubwa kati ya nchi kuwa na taasisi huru za kiuchumi (of course na za kisiasa pamoja na demokrasia) na ukuaji wa uchumi. Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma hili chapisho: Political Institutions, Economic Growth, and Democracy: The Substitute Effect.

Kuhusu intellectual arrogance, waziri hakupaswa kuwaambia wabunge waende Hazima wakapatiwe lecture ya bure ya masuala ya uchumi. Hii ni kejeli na kujifanya mjuaji. Wabunge wameuliza maswali yenye misingi ya kisera, na siyo economics jargon hivyo waziri alipaswa kuwajibu accordingly. Na ieleweke kuwa waziri wa fedha na mipango ni msimamizi mkuu wa sera za fedha na mipango ya uchumi na siyo lazima awe mtaalam wa uchumi. Wataalam wa sekta husika ni wakurugenzi katika wizara.
 
Siku hizi hata kama hamna live habari zote zipo mtandaoni "the power of technology"
 
Wekeni mipango sio kila wamuone yeye...
Mumeiporomosha TIC kila kitu kiamuliwe na mtu mmoja halafu waziri anatamka bungeni ?
Kuongoza nchi ni kipaji
 
Sasa nani mshauri wa mwenzie inamaana uyo waziri na udaktari wake swala kama ilo alishindwa kuliona mpk aambiwe na wabunge na apewe msisitizo na rais upuuzi tu huu au mnataka kuleta yaleyale ya kutanguliza pongezi za dhati kwa rais hahahaaa
 
mazingira gani tena wakati kishayarahisisha?
acheni kutafutiza maneno, waambieni hao wawekezaji Raisi kaweka mazingira ya wao kwenda awape kazi.
Mkuu,issue sio amerahisisha mazingira anayo mengi ya kufanya ili kumvutia mwekezaji ikiwa ni pamoja na kupima matamko yake leo unasainiana nae kesho anakugeuka mwambie vitisho havifai wala haviwezi kumvuta mtu.
 
Kwa nn hajiulizi kwa nn wawekezaji wawe was nje ama ndani wamepotea? Nani atawekeza mahali ambapo Sera sio rafiki? Nani atawekeza.mahali ambapo sheria hazifuatwi na hazitabiriki? Nani ana uhakika mtukufu raisi atakuja na tamko gani juu ya uwekezaji? Akirekebisha haya hana haja ya kuwaomba wabunge wamsaidie kuleta wawekezaji bali wawekezaji watakuja wenyewe.
Haya ni maneno KUNTU kabisa mkuu asomae na afahamu.
 
Back
Top Bottom