Waziri Mpango: Rais Magufuli amenipigia simu kuhusu michango ya Bashe na Nape Bungeni

Jamani IPTL si ilikuwa ya CCM kuingia mikataba mibovu halafu kuiba ESCROW?? Ishu si wawekezaji, ni wanasiasa kuingilia biashara..
 
Mkuu, wawekezaji tena wa miradi mikubwa hawaletwi kihivyo ..............!!

Kama wanakubaliana na ushauri basi watangaze Expression of Interest waone ni proposal ngapi watazipata.

Sasa Nape au Bashe wakileta Watu wao ........... halafu huko mbeleni mambo yakatofautiana si lawama zitakuwa kwao kama Rugemarila leo anavyosoteshwa Lupango na IPTL yake!!
Hoja yako inakubalika sana lakini mkuu si kuna kitu inaitwa kufanya pitching business idea/product or project pitching?
Nadhani hii ipo kwa pande zote, namaanisha mwenye project anaweza kufanya pitching kutafuta wawekezaji lakini pia mfanyabiashara( kwa kesi hii ni muwekezaji binafsi) anaweza kufanya pitching ya kushawishi apate zabuni au mradi wa kushirikiana/kuwekeza na mteja(kwa kesi hii ni serikali). Kwamba mfanyabiashara anaweza kuwa na idea ya mradi mzuri kwa taifa na yeye kupata kipato ambao watendaji wa serikalini walikuwa hawana wazo zuri kama hilo, yeye anaenda kuwashawishi wanampa zabuni.

Hiyo kitu inakubalika, na serikali inaweza kukusikiliza ikafurahishwa na idea yako wakakupa mradi wa kuwekeza.
 
Nakubaliana na wewe ..............!!

Tatizo ni kuwa inaonyesha kuwa serikali hii haina sera hiyo. Ndiyo maana Serukamba kahoji na akasema serikali iamue tu upande upi ujamaa au ubepari ........... maana mpango hauelekei kutoa nafasi kwa sekta binafsi.

Pia ukiangalia image tuliyojijengea kwenye mgogoro wetu na Acacia, hata kama ulikuwa wa nia njema na outcome nzuri probably, kwa namna tulivyouhanndle tutakuwa tumepunguza shauku ya wengi. Kila muekezaji itabidi kwanza aangalie upepo!!
 
Raisi atafute wawekezaji asijibu majibu marahisi,arafu nape na bashe walikuwa wanaongea na mpango,sio magufuli kwahyo ingetosha kusema serikali badala ya Raisi,au ndio mnatafuta kuwanyamazisha wasionekane wanajishana na raisi
Raisi ni taasisi kiongozi jua Hilo . Na yeye Ndo kiongozi mkuu wa serikali jus na Hilo pia
 
Waziri Mipango akina Bashe na Nape sio watu wa kubeza wanajua 2020 CCM itakabiliana na nini kwenye uchaguzi mkuu.
Wewe ni mbunge wa kuteuliwa ndio maana machungu ya wapiga kura hujui.
 
Wawekezaji wanakuja kutokana na sera zao kuhusu wawekezaji wenyewe.

Sasa kama unamkalibisha mgeni huku umemuelekezea mtutu wa bunduki, unafikilia hatakama atafika barazani kwako lakini atakua na wasiwasi !

Yule mama tangu wamuondoe kwenye ofisi ya uwekezaji hadi leo mambo hayajakaa sawa.
Sizonje alimuomba nasikia akamjibu you are not of my type. Akamfanyia mizengwe Hadi jumfukuza. Lakini akampata Kairuki mwengine Hadi kumkabidhi madini yote
 
Hao vijana ni wababaishaji, mtu/KAMPUNI gani binafsi anaweza kudumbukiza kiasi chote kile cha fedha (~8 trion) kwenye mrefu wa sina hiyo kwa nchi za Kiafrika??
 
Raisi atafute wawekezaji asijibu majibu marahisi,arafu nape na bashe walikuwa wanaongea na mpango,sio magufuli kwahyo ingetosha kusema serikali badala ya Raisi,au ndio mnatafuta kuwanyamazisha wasionekane wanajishana na raisi
Walikuwa wanaongea na serikali. Kutoa majibu, Mpango ilimpasa kushirikisha wenzake serikalini. Na ukiona hivyo, Hilo swala limeshatazamwa na k ufuatiliwa.
 
Wewe bado kabisa, jambo lililopo hapa ni vikao vya bunge ni kwa wabunge tu hivyo kuingiza hoja kupitia simu ni kuongeza idadi ya wabunge na ukiukwaji wa kanuni za bunge na rais lazima aheshimu kanuni za bunge .
Wewe ndiye usiyeelewa vema. Waziri hawezi kuwa na takwimu na majibu ya kila kitakachoulizwa hapohapo. Swali likiulizwa kwa serikali, waziri anatumia wataalam wa sekta na mamlaka zingine ili aweze kutoa majibu yanayostahiki.

Huo ndiyo utaratibu wa kutoa majibu ya serikali.
 
Mazingira gani sasa wakati kishasema waje awape kazi?
au huwa mnaongea ili mradi mna midomo?
waambieni waende basi mliokuwa mkiwasemea. acheni manenomaneno.
Awape kazi kwa utaratibu gani? Ina maana anaingilia mamlaka zote, na hizi tenda kubwa kubwa huenda zina mkono wake!! Kwa staili hii lazima atakuja kukwama muda sio mrefu. Nadhani hiyo nafasi anaitumia vibaya, iko siku nyie mnaemshabikia mtakuja kumkataa. Nae Jenista eti anamtuhumu Mh Mbowe kuwa àheshimu madaraka ya Urais akaenda mbali kwa kutoa mfano wa Mnyeti na Kilango, nilichogundua hakuekewa kilichoongelewa na Mh Mbowe, pole yake maana analinda tumbo lake.
 
kiki zingine zinakuwa ni aibu,yeye angesema kwa niaba ya serikali sasa.watanzania wanaoitwa Ma profesa na Ma dkta wana shida kwenye bongo zao
 
Back
Top Bottom