Waziri Mpango: Rais Magufuli amenipigia simu kuhusu michango ya Bashe na Nape Bungeni

Mkuu,issue sio amerahisisha mazingira anayo mengi ya kufanya ili kumvutia mwekezaji ikiwa ni pamoja na kupima matamko yake leo unasainiana nae kesho anakugeuka mwambie vitisho havifai wala haviwezi kumvuta mtu.
Ni nani kasainiana naye leo na kesho akamgeuka? toa mfano hata mmoja.
Anachofanya Rais JPM ni kupitia mikataba ya kishenzi waliyosainiana wapiga dili huko nyuma na kuiweka sawa ili Nchi nayo inufaike.-Nyie hilo ndo mnaita RAIS kawa kigeugeu? Mlitaka tuendelee tu kuliwa maadam kuna mijizi huko nyuma ilisaini?
 
Wao wao watu binfsi ndio wametuleta hapo tulipo. IPTL ndio hii. Na sasa mnataka kuleta ujinga nwingine tuliwe. Ni hafadhali kukaza mkanda kuliko hili la wakina Nape
 
Na hizi amsha amsha za kipindi hichi. Wawezekaji wanazipenda sana! Tusiwe na shaka watakuja weeeeeengi
 
Kwa nini anaangalia bunge muda wa kazi???? Si angesubiri marudio TBC wakati wa usiku????
 
Wazuri Mpango, baniani mbaya kiatu chake dawa. Muache kuwaona wanaoongea kama wana matatizo. Ndio hulka yetu wanaadamu kusema
 
Hivi rais ameona hilo tu la uwekezaji?? Je lile la serikali kujipatia tenda yenyewe imekaeje??

Kwa mfano TBA!! Je atakua tayar kuendelea na zile taratibu za kutangaza tenda na sio stahili za sasa kisema rais amewapa TBA kujenga sehem fulan???
 
Rais John Magufuli amewataka wabunge wawili wa CCM, Nape Nnauye na Hussein Bashe, ambao michango yao bungeni imekosoa uendeshaji uchumi, wampelekee majina ya wawekezaji wanaokwamishwa ili awape kazi.

Wabunge hao wa Mtama na Nzega Mjini waliikosoa Serikali wakati wa kujadili Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka 2018/2019.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ambaye alishutumiwa na wabunge hao kumpotosha Rais, alisema wakati akihitimisha mjadala huo kuwa alipigiwa simu na mkuu wa nchi na kuelezwa hayo.

“Naomba ninong’one na Bunge lako tukufu. Mheshimiwa Rais Magufuli aliposikia huu mjadala, alinipigia simu na aliniambia hivi,” alisema Waziri Mpango.

“Waziri, mwambie ndugu yako mheshimiwa Nape na mheshimiwa Bashe kuwa nawataka sana hao wawekezaji kwenye ujenzi wa Standard Gauge Railway.

“Wawalete hata kesho niko tayari kuwapa reli ya kutoka Kaliua –Mpanda au Isaka-Mwanza au reli ya Mtwara-Mchuchuma hadi Liganga waijenge.

“Hayo ni maneno ya mheshimiwa Rais. Natumaini waheshimiwa husika will raise up to this challenge from his excellence the president (wataifanyia kazi changamoto ya mheshimiwa Rais.”

Akijibu hoja za wabunge hao na wengine, Dk Mpango alisema si kwamba Serikali imeiweka pembeni sekta binafsi bali bado haijakaa vizuri na wakati mwingine inakuja na masharti yasiyotekelezeka.
 
Back
Top Bottom