Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,879
Hamed Bakayoko enzi za uhai wake
Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Hamed Bakayoko, amefariki dunia katika hospitali moja nchini Ujerumani, mamlaka imesema.
Bakayoko, aliyekuwa akipata matibabu ya saratani, alifariki dunia Jumatano siku chache tu baada ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 56.
Aliteuliwa kama waziri mkuu mnamo mwezi July kufuatua kifo cha mtangulizi wake Amadou Gon Coulibaly.
Rais Alassane Ouattara amemuelezea Bwana Bakayoko kama kiongozi bora, mfano wa kuigwa kwa vijana na mwenye uaminifu usio kifani".
Bwana Bakayoko alipelekwa nchini Ufaransa mnamo mwezi Februari kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na baadaye akahamishwa hadi nchini Ujerumani kwasababu afya yake ilikuwa inaendelea kuzorota.
Waziri mkuu huyo ambaye alikuwa mkurugenzi mtendaji wa vyombo vya habari alitekeleza jukumu kubwa katika maridhiano nchini Ivory Coast wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kipindi cha mwongo wa kwanza wa karne.
"Alikuwa mshikadau mkuu katika siasa na maridhiano," amesema msemaji wa upinzani wa chama cha Ivorian Popular Front Issiaka Sangare, katika shirika la habari la AFP.
Mbali na jukumu lake kama waziri mkuu, Bwana Bakayoko pia alikuwa waziri wa ulinzi nchini humo.
Patrick Achi ameteuliwa kama waziri mkuu wa muda huku Tene Birahima Ouattara, huku kaka mdogo wa rais akitajwa kama waziri wa ulinzi wa muda.
Chanzo: BBC