Waziri Mkuu: Tumesitisha Sunday school na Madrasa, tulichoruhusu ni Ibada tu tena zifanyike kwa muda mfupi kisha waumini waondoke

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
31,191
2,000
Waziri mkuu mh Kassim Majaliwa amesema kuna taarifa kuwa baada ya masomo kusitishwa kwa sababu ya Covid 19 watoto hao sasa wamekuwa wakienda makanisani na misikitini kwa ajili ya kujinza.

Mh Majaliwa amesisitiza kuwa alipokutana na maaskofu na mashehe walikubaliana kusitisha Huduma nyingine zote isipokuwa ibada tu.

Hivyo waziri mkuu amesema ni marufuku kwa watoto kukusanywa kwa kisingizio cha sunday school na madrasa na kwamba makanisa na misikiti itumike kwa shughuli za Ibada tu za kuliombea taifa tena kwa muda mfupi na baada ya Ibada waumini watawanyike mara moja.

Chanzo: Channel ten habari!
 

lukesam

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
10,695
2,000
Viongozi wa makanisa na misikiti hamuoni aibu mkatangaza kusitisha ibada zenu?

Au ndio mnataka hadi serikali iwaambie fungeni nyumba zenu za ibada?

Kupitia kauli hii ya waziri mkuu nadhani kama watu wazima mnaojali afya za watanzania na nyie pia, mnapaswa kujiongeza.

Jiongezeni!
 

Michelle

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
7,400
1,500
Kwahiyo wazazi waende wabebe ugonjwa wapeleke nyumbani kwa watoto na wafanyakazi waliobaki nyumbani? Kuombea taifa lipi sasa? Linaloenda kuambukizwa ibadani likaambukize nyumbani? Nini shida na hizi ibada? Tunataka kumfurahisha nani?
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
Angesitisha na ibada tu
Watu wasalie nyumbani

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
hata mimi naishangaa serikali. Kufunga madrasa na sunday schools ni jambo zuri lakini nadhani kuachia ibada ziendelee tutakuwa tunarudisha nyuma mafanikio na faida za kufunga madrasa na sunday school.

Je, watoto hawaruhusiwi kwenye hizo ibada ambazo serikali imeruhusu ziendelee?

..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom