Waziri Mkuu: Tumesitisha Sunday school na Madrasa, tulichoruhusu ni Ibada tu tena zifanyike kwa muda mfupi kisha waumini waondoke

Haihitaji sheria ya dunia kujua kilicho bora kwako,kama unasubiria dini ikuongeze kwa jambo la wazi kama hilo inadhiirisha tu jinsi gani ulivyo na akili ndogo au mtumwa wa dini. Abuu Dharr,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lukesam,
Tangu niwe mwanachama wa JF hii ndio point kuu. Serikali inawaheshimu watu wa dini na wao hawalijui hilo.

Serikali imeshindwa tu kuwalazimisha wafunge ibada. Wao wangejiongeza tu wakakubaliana kusitisha hadi jinamizi hili lipite.

Au wabuni njia ya kufanya ibada bila kukusanyika wengi
 
Naona hata hilo la makubaliano bado hawalitilii maanani Kwani ndoa zinafungwa kama kawa
Ibada ya misiba kama zamani hasa kwenye makanisa kufanya ibada ndefu ya msiba tu na kuruhusu maingiliano.

Serikali ingesitisha tu ibada zote
 
Abuu Dharr,
Na ndio maana serikali imewaheshimu na kuwapa waamue wenyewe lakini mbona bado. Misikitini na Makanisani ibada za ndoa kama zamani kama vile hatuko kwenye janga la kidunia. Na hasa Tanzania ndio tuna shida, mpaka serikali ituamulie kila kitu ndio tufanye
 
CityHunter1,
Mkuu inaweza kuwa walibadilishana documents au mteja kampa teller pesa zenye corona. Pia sio lazima Teller apate kirusi kutoka kwa mteja, anaweza kuwa alipata kwenye dalala, bodaboda, teksi au kaleta nyumbani kwake . Maambukizi ya Corona iko very complicated na huwezi kujudge kwa scenario moja au mbili

‘CORONA’ ni ugonjwa wa virusi (COVID-19) unaoambukizwa kwa kuingiwa na majimaji ya yatokayo kwenye njia ya hewa wakati mtu mwenye ugonjwa huu anapokohoa au kupiga chafya. Njia nyingine ya maambukizi ni kugusa majimaji yanayotoka puani (kamasi), kugusa vitambaa a nguo zilizotumiwa na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa huu.

Ugonjwa huu unaambukizwa pia kwa kugusa popote ambapo mtu mwenye maambukizi amegusa kama vitasa vya milango, meza, makaratasi, vyombo vya chakula, vifaa vya ofisini, milango ya magari, helmet za pikipiki, usukani wa magari, meli, vitufe vyote vya kompyuta, simu, mitambo nk
ELIMU KUHUSU UGONJWA WA HOMA KALI YA MAPAFU UNAOSABABISHWA NA VIRUSI VYA CORONA – COVID-19
 
Serikali itafute chakula cha kuwalisha watu wa Dar na Zanzibar kwa wiki mbili angalau halafu wote hao wafungiwe ndani
 
Kwahiyo wazazi waende wabebe ugonjwa wapeleke nyumbani kwa watoto na wafanyakazi waliobaki nyumbani? Kuombea taifa lipi sasa? Linaloenda kuambukizwa ibadani likaambukize nyumbani? Nini shida na hizi ibada? Tunataka kumfurahisha nani?
Kampeini

Odhis *
 
lembu,
Hakika watu wangekuwa na uelewa kama wako,tusingefika hatua hii iliyopo kwa sasa. Kuna badhi ya watu sijui wanajihisi wawe haiwahusu. Ila matokeo yanamfikia kila mtu.

Wengine naona wanadai sijui wana vyakula,haijalishi una nini, kumbukeni,Zaidi ya 50% ya wakazi wa Dar hupata chakula baada ya kufanya kazi zao za kila siku.

Na hao hao ndo wahanga wakubwa. Sasa hatua kali zisipochukuliwa mapema,ndo itaenda hadi miezi na miezi. Na safari zikiendelea,ndo maambukizi pia yanasambaa. Hayatadhibitiwa sehemu moja.

Covid-19 siyo siasa na chuki za badhi ya watu humu,inamhusu kila mtu. Na kabla hujaona inachokifanya,utaona kawaida tu.
 
Serikali itafute chakula cha kuwalisha watu wa Dar na Zanzibar kwa wiki mbili angalau halafu wote hao wafungiwe ndani
Ndio,kitatafutwa lakini ugawaji wake nao shida. Mi nahisi kwanzu kila mtu angeelewa kuwa hali ya sasa, kipaumbele kipewe ubinadamu tu.

Jirani yako yupo mtu mwenye hali ngumu,mjali,kula nae hicho kidogo ulicho nacho,walofikia wa kwanza wana ushahidi wa kutosha
 
Hakuna faida yeyote yaani wazazi tusali halafu twende kuwaambukiza watoto wetu nyumbani. sikubaliani na waziri mkuu hata kidogo makanisa, miskiti, baa, masoko, minada, maeneo ya kubeti, vyote vingefungwa mala moja.

Nchi ya kipumbavu sana kuwafurahisha wachungaji na mapadri uku wananchi wanateseka uzuri huu ugonjwa hauangalii wewe ni nani hata Yeye unaweza mpata.
Ila wewe jamaa si uliomba hili janga litukumbe!
 
Kwaya zimefutwa! Hakuna kuimba. NImeona hata jana parokiani kwetu. afadhaliiiiii
Wamekataza kuimba.

Ninashangaa baadhi ya Parokia kwaya zimezuiwa halafu watu bado wanaimba!

Kilichokatazwa ni kuimba: kwaya na waamini wote.
 
Unajua ulaya yote hata Vatican kwa Papa makanisa yamefungwa huko Saudi Arabia Misikiti imefungwa kwa ajili ya huu ugonjwa hatari sana unaua bila mtu kujua. Watu Ulaya na Amerika wamekufa wengi sana. tuombe Mungu ili wimbi lisifike Africa tutakwisha. Kwa maoni yangu Serikali inabidi ifunge makanisa na misikiti kwa week 12 .
 
Bukinabuza,
Kuna watu wameiga msemo wa Marwkani kwamba ni kama mafua tu. Ila kw idadi iliyopo kwa sasa,ukizingatia wapo wanaotembea na virusi bila kujitambua,na wanazidi kuambukiza,hatua zitachukuliwa wagonjwa wakifika 5,000(nawasikitikia wanaotoa huduma za afya huko walipo wagonjwa)
 
Back
Top Bottom