Waziri Mkuu: Tumesitisha Sunday school na Madrasa, tulichoruhusu ni Ibada tu tena zifanyike kwa muda mfupi kisha waumini waondoke

Roma na Maka wamesitisha ibada za mikusanyiko makanisani na misikitini lakini waswahili tunakomaa na kukusanyika. Mungu atunusuru.
Ukiwa unaendesha familia yako halafu ukataka kuiga mtindo wa jirani yako anavyoongoza familia yake, ujue wewe ni kidume suruali,

Semea nchi yako wewe unaonaje?
 
Kwahiyo wazazi waende wabebe ugonjwa wapeleke nyumbani kwa watoto na wafanyakazi waliobaki nyumbani? Kuombea taifa lipi sasa? Linaloenda kuambukizwa ibadani likaambukize nyumbani? Nini shida na hizi ibada? Tunataka kumfurahisha nani?
Ndugu yangu Michelle tunaongozwa na watu wasio na maono kabisa yaani Mtoto asimuambukize mzazi Mzazi ruksa kumuambukiza Mtoto hii ni akili au matope?
 
lukesam,
Kwani viongozi wa dini wamelazimisha watu waende nyumba za ibada? mtu anaenda mwenye kwa uamuzi wake, atakayeona akafanye ibada nyumbani hakuna shida maana hata viongozi nao ni waumini.
 
Ndo kusema Serikali inaona ibada sio tishio kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani kuna haja ya kuwakumbusha watanzania kuwa kila mmoja wetu ana ubongo na ufahamu wake mwenyewe. Kila mmoja atumie wake kufanya maamuzi binafsi.

Ukitumia wa kiongozi pia ni sawa,nao ni uamuzi. Ila tukumbushane kutumia wa mtu binafsi kwanza.

You have a brain and mind of your own. Use it, and reach your own decisions.
 
Hakuna faida yeyote yaani wazazi tusali halafu twende kuwaambukiza watoto wetu nyumbani. sikubaliani na waziri mkuu hata kidogo makanisa, miskiti, baa, masoko, minada, maeneo ya kubeti, vyote vingefungwa mala moja.

Nchi ya kipumbavu sana kuwafurahisha wachungaji na mapadri uku wananchi wanateseka uzuri huu ugonjwa hauangalii wewe ni nani hata Yeye unaweza mpata.
 
Ndugu yangu Michelle tunaongozwa na watu wasio na maono kabisa yaani Mtoto asimuambukize mzazi Mzazi ruksa kumuambukiza Mtoto hii ni akili au matope?
Ndugu yangu sisi tunafuata ushauri wa wanasayansi za jadi na dini.Anayepaswa kumlinda kiumbe aliyemleta duniani kwa maamuzi yake, anaelekezwa kumuangamiza kwa maamuzi ya viongozi.Wazazi mjue kwa watoto wenu nyie ndio mawaziri wakuu.

Fanyeni maamuzi sahihi. Hamna maono kabisa,kuna maangamizi mkuu.
 
Muda mfupi ni sekunde/dakika au saa ngapi?

Ngoja tuone labda watakuwa wanaiwahi Corona.
 
Mambo mengine haya ni kujaribu kuonesha tu kwamba nanyi mnaunga mkono mapambano dhidi ya corona kama wengine ila sioni tija kwenye makatazo.
 
Kwani viongozi wa dini wamelazimisha watu waende nyumba za ibada? mtu anaenda mwenye kwa uamuzi wake,atakayeona akafanye ibada nyumbani hakuna shida maana hata viongozi nao ni waumini.
Tafadhali soma tena ujumbe wangu kwa makini kisha upeleke ujinga wako huko nyumbani kwenu ukautulize huko kimya.
 
Kwahiyo serikali inatuhakikishia corona inaogopa wazazi lkn watoto inashambulia !

Ndg mtanzania jilinde ww wenyewe na family yako maana serikali inatapatapa tu za kuambiwa changanya na zako.

Balaa likikupata ni ww ndio utaumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom