johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,532
- 141,334
Waziri mkuu mh Kassim Majaliwa amesema kuna taarifa kuwa baada ya masomo kusitishwa kwa sababu ya Covid 19 watoto hao sasa wamekuwa wakienda makanisani na misikitini kwa ajili ya kujinza.
Mh Majaliwa amesisitiza kuwa alipokutana na maaskofu na mashehe walikubaliana kusitisha Huduma nyingine zote isipokuwa ibada tu.
Hivyo waziri mkuu amesema ni marufuku kwa watoto kukusanywa kwa kisingizio cha sunday school na madrasa na kwamba makanisa na misikiti itumike kwa shughuli za Ibada tu za kuliombea taifa tena kwa muda mfupi na baada ya Ibada waumini watawanyike mara moja.
Chanzo: Channel ten habari!