#COVID19 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Tanzania tuzidi kuchukua tahadhari dhidi ya Wimbi la 4 la COVID-19

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,962
141,961
Waziri Mkuu mh Majaliwa amesema bara la Afrika kwa sasa linapambana na wimbi la 4 la covid 19 hivyo watanzania tuendelee kuchukua tahadhari.

Majaliwa amesema hadi sasa watanzania 725 wameripotiwa kufariki kwa Corona tangu ugonjwa huo uanze.

Chanzo: ITV habari
 
Kwa sasa ni mwendo wa kutangaziana mawimbi tu, naona hii biashara ya covid haielekei kufikia tamati.......naona ikiletwa chanjo nyingine ya kupambana na UVIKO part IV. Ngoja tuendelee kushuhudia viongozi wa wadanganyika wanavyodemka na hii ngoma ya mawimbi kutoka kwa mabeberu....
 
725?
Tangu Corona ianze? Ina muda gani? Urusi imerekodi vifo vingapi kwa siku wiki iliyopita? Hii namba nimeiona siku nyingi kweli, haikui?

Kama hivyo ndivyo, kwanini wasiseme tu kuwa HAMNA?
 
Hayo mawimbi ni yenu viongozi mliokula vya beberu,siye wananchi tunaendelea na maisha yetu Kama kawaida.
Barakoa, social distance fanyeni nyie ili beberu aone mnavyoteseka na hela yake.
 
Nimeona hapa kwenye taarifa ya habari VoA unanunua dozi milioni 110 kutoka Moderna na biashara hiyo imefanikishwa na ikulu ya Marekani hebu fikiria ni bilioni ngapi na ikumbukwe moderna ndo chanjo ghari zaidi.!
 
Back
Top Bottom