Waziri Mkuu: Treni ya SGR kuanza majaribio Julai 2021

Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alipotembelea stesheni ya kisasa iliyojengwa eneo la Gerezani jijini Dar es salaam.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliupongeza uongozi wa shirika la reli nchini TRC kwa kusimamia huo mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Yapi merkezi toka Uturuki na kwamba kwa sasa huo mradi kipande cha Dar mpaka Moro umekamilika kwa 91%.

Waziri mkuu amewatoa hofu watanzania kwa kueleza kuwa kazi chini ya rais mama Samia zinaendelea na miradi yote mikubwa itatekelezwa kwa manufaa ya umma.

Awali Masanja Kadogosa ambae ni mkurugenzi wa Trc alisema kuwa walitarajia mabehewa na vichwa vya treni kuwasili mwezi Julai mwaka 2021 au mapema zaidi.

Mpaka sasa kipande cha Dar mpaka pugu kimekwama kukamilika japokuwa ni kipande kifupi
Juzi kati nimeona gari la kawaida limevishwa tairi za train linapita kwenye hiyo reli sikuelewa dhamira ilikuwa ni nini
 
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alipotembelea stesheni ya kisasa iliyojengwa eneo la Gerezani jijini Dar es salaam.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliupongeza uongozi wa shirika la reli nchini TRC kwa kusimamia huo mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Yapi merkezi toka Uturuki na kwamba kwa sasa huo mradi kipande cha Dar mpaka Moro umekamilika kwa 91%.

Waziri mkuu amewatoa hofu watanzania kwa kueleza kuwa kazi chini ya rais mama Samia zinaendelea na miradi yote mikubwa itatekelezwa kwa manufaa ya umma.

Awali Masanja Kadogosa ambae ni mkurugenzi wa Trc alisema kuwa walitarajia mabehewa na vichwa vya treni kuwasili mwezi Julai mwaka 2021 au mapema zaidi.

Mpaka sasa kipande cha Dar mpaka pugu kimekwama kukamilika japokuwa ni kipande kifupi
Majaribio tayari au?
 
majaliwa alishajivunjia heshima kwa sababu ya kauli zake za uongo zinazojirudia-rudia. He is not reliable hawezi kusema kitu, jamii ikamuamini. ni wazi kuna tatizo SGR lakini mlipakodi anayeigharamia SGR haambiwi ukweli. Muda una waumbua. Jitafakari, pima gharama za kusema ukweli vs kusema uongo kwenye jamii mnayoitumikia. Jibu mnalopata very embarrassing.
 
Back
Top Bottom