Waziri Mkuu: Treni ya SGR kuanza majaribio Julai 2021

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,827
2,000
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alipotembelea stesheni ya kisasa iliyojengwa eneo la Gerezani jijini Dar es salaam.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliupongeza uongozi wa shirika la reli nchini TRC kwa kusimamia huo mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Yapi merkezi toka Uturuki na kwamba kwa sasa huo mradi kipande cha Dar mpaka Moro umekamilika kwa 91%.

Waziri mkuu amewatoa hofu watanzania kwa kueleza kuwa kazi chini ya rais mama Samia zinaendelea na miradi yote mikubwa itatekelezwa kwa manufaa ya umma.

Awali Masanja Kadogosa ambae ni mkurugenzi wa Trc alisema kuwa walitarajia mabehewa na vichwa vya treni kuwasili mwezi Julai mwaka 2021 au mapema zaidi.

Mpaka sasa kipande cha Dar mpaka pugu kimekwama kukamilika japokuwa ni kipande kifupi
 

Pan AM

JF-Expert Member
Apr 30, 2018
250
500
Kadogosa bado yupo kazini?,nilisikia naye kachota minoti kipindi jiwe anapambania uhai wake?..
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
4,995
2,000
Hicho kipande cha Dar mpaka Pugu shida yake ni nini mbona hakisogei, au hiyo ardhi wakati mwingine huwa inahama?
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
3,444
2,000
Huu mwaka wa 5 bado wanatengeneza barabara ya juu ya treni Kariakoo.
Aliyedesign ile tren ipite juu Kariakoo na chizi kabisa au alidesign kwa matakwa yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom